Umuhimu wa kitchen parties ni kwa mabinti tu?

Marigwe

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
228
18
UMUHIMU WA KITCHEN PARTIES NI KWA MABINTI TU?

Ndugu zangu kwa muda sasa nimekuwa ninajiuliza. Hivi hizi Kitchen parties wanazofanyiwa mabinti siku chache kabla ya kuolewa zinawasaidia kweli hao mabinti? Jibu ambalo nimelipata ni ndiyo na hapana. Ndiyo kwa sababu wananufaika na zawadi wanazopewa ambazo nyingi zinakuwa ni vifaa ambavyo vitatumika katika kuendesha jiko na nyumba atakayohamia baada ya kuolewa.
Hapana kwa sababu inapokuja kwenye kupewa mawaidha anayepewa ni yeye peke yake bila ya mume mtarajiwa. Mara nyingi binti hupewa mawaidha kama vile mume anayekwenda kuishi naye amekuwa nae kafuzu katika masuala ya kuendesha nyumba na kumwangalia na kumtunza mkewe. Kumbe sivyo. Matokeo yake baada ya muda kunatokea migongano kati yao wawili. Kwa sababu kile alichoambiwa yule binti kinahusu baadhi ya mambo ambayo mengi yanakuwa kwa upande wake kama mwanamke au mke. Walimu wake wanakuwa wamesahau ndoa japo ni ya mume na mke lakini pia yapaswa kuwa ni taasisi moja kwa maana ya umoja wa mume na mke. Na kama taasisi inakuwa na mfumo wake na mwenendo wake ambao hutokana na kuunganisha ujuzi wa mume na mke.
Nataka kusema nini. Ninachosema ni kuwa kwa kuwa mume mtarajiwa hakufanyiwa darasa wala maandalizi yoyote kwa maana ya jinsi ya kuishi na mkewe, anapoanza maisha ya ndoa kunakuwa na migongano iliyojaa mshangao kwa wao wote wawili. Kumbe mume nae angefanyiwa darasa kwa kweli ingelimsaidia kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Pamoja na kwamba sijawahi kushiriki kwenye kitchen parties ila nimewahi kuona kanda za video kuhusiana na hilo. Ambalo nimeliona ni kuwa mawaidha anayopewa binti hayana maono. Yaani hayalengi kumsaidia kwa maana ya kuiona ndoa yake ni kitu ambacho kitadumu hadi kifo.
Mawaidha mengi yanagusa juu ya namna ya kumpikia mume na masuala ya tendo la ndoa. Yaani mambo ya sasa na yenye mahusiano ya kutuliza kiu ya mwili. Kama vile msosi na unyumba. Wanasahau kuwa kwamba ndoa kama taasisi hupitia hatua kadhaa kadiri miaka inavyoenda na wakati huo huo mwanaume na mwanamke pia hubadilika kutokana na umri unavyoongezeka. Kwa mfano wanaume wengi huwa hawaelewi kuwa mkewe akiwa mja mzito hubadilika kihaiba na hata kitabia. Wanawake wengine wanakuwa wakali hata kumuona mume hawataki na wengine kila wakati anataka awe na mumewe karibu na kadhalika.
Lingine ni kuwa mke akifikia miaka ya 50 na kuendelea huanza kubadilika kuelekea menopause. Hatua hii huwapumbaza na kuwashangaza wanaume wengi hadi wengine hufikia kuwatelekeza wake zao wakifikiri wamekuwa wakorofi au baridi au hawana mvuto, kumbe the woman is undergoing biological changes in her hormones. Sasa mume huyu angekuwa alifanyiwa darasa wakati wa ujana wake kabla ya kuoa na kuambiwa juu ya haya asingeshangaa. Kwani angeweza kujitayarisha hata kisaikolojia jinsi ya kukabiliana nalo. Hata katika nafasi za uongozi tabia ya mwanamke aliyemo kwenye menopause huwashangaza hata wanajamii. Sitaki kutaja majina ya watu. Unamkuta mwanamke ana madaraka ya juu sana katika Wizara au shirika kama kiongozi wa kufanya maamuzi. Kuna wakati unashangaa kauli au maamuzi anayoyatoa mnabaki hamuelewi au mnaamua na nyie kulumbana nae kwa kumshambulia. Kumbe masikini ya Mungu yule mama hajielewi na nyie mnaemsikiliza hamumwelewi.
Sasa ndugu zangu nini maoni yenu kuhusu suala hili. Hamuoni upo umuhimu wa wanaume nao kufanyiwa siyo kitchen party labda niite Managing the House Briefing au unyago na jando au??!!!!
 
Hizo kitchen parties hazina manufaa wala maana yoyote. Ni ujinga mtupu. Kwanza kwa nini zinaitwa 'kitchen parties'? Hazina jina la Kiswahili?
 
hivi zile bachela party kwani huwa zinawafundisha nini wanaume ..?

Omega Psi Phi hiyo Kitchen party kwa kiswahili si ni mambo ya jikoni anayofundwa binti kabla ya ndoa!
 
mie naona kama una topic mbili tofauti kwenye maelezo yako.swala la wao kufanyiwa kitchen party na mambo ya mimba na kuzeeka vitu viwili tofauti.


najibu swali lako la kitchen party, je ni muhimu kwa wanaweka tu? mimi nafikiri umuhimu wake unatugusa sisi wanaume baada wao kutimiza waliofundishwa pale mengi ni jinsi ya kuturidhisha sisi wanaume wao kwahio hapo ndio tunapofaidika mkuu.kwahio jibu
umuhimu wake sio kwa mabinti tu kwani by the end of the day wote tunakuwa tumefaidika kutoka kwenye somo alilopata kule.
 
hivi zile bachela party kwani huwa zinawafundisha nini wanaume ..?

Omega Psi Phi hiyo Kitchen party kwa kiswahili si ni mambo ya jikoni anayofundwa binti kabla ya ndoa!

Ok, mambo ya jikoni sio? Ni mambo gani ya 'jikoni' anayofundwa? Kupika? Kuosha vyombo? kuetenga chakula mezani? kupiga deki? Au kukata viuno na jinsi ya kumegwa? Let's keep it real maana nimeona kwenye videos kibao hizo kitchen party na sikuona chochote kinachohusu jiko!!!!

Na bachelor party na bachelorette party na zenyewe hazina maana yoyote vilevile
 
Yule aliyependekeza kuwa mwanaume awepo kwenye kitchen party kanchekesha kinoma, especially ili kumwandaa kisaikolojia pindipo masuala kama menopouse (kwa mwanamke) yanapotokea. Menopouse hutokea baada ya miaka kumi na tano hadi ishirini katika ndoa. (kwa ndoa zetu hizi za after school)

Ninachocheka ni kuwa, hivi kweli mtu utakumbuka baada ya miaka hiyo kupita ili uwe ready kisaikolojia? kama somo la juzi tu leo unasahau, sembuse miongo miwili??
 
yani hizi zimechangia sana kuwaharibu wanawake kwani wanayofundishwa uko ni aibu tupu
 
hivi zile bachela party kwani huwa zinawafundisha nini wanaume ..?

Omega Psi Phi hiyo Kitchen party kwa kiswahili si ni mambo ya jikoni anayofundwa binti kabla ya ndoa!


hapa umeniacha njia panda mtu wangu mbona sijawai kusikia hii kitu kweli jf inamambo
 
Wewe Mundu ni dhahiri huna ndoa bado. Kama unayo basi huna vision. Unaishi kwa ajili ya leo tu. Pole sana. Kwa mtu aliye katika ndoa kama anaithamini basi hawezi kuwa na mawazo kama yako.
 
Wewe Mundu ni dhahiri huna ndoa bado. Kama unayo basi huna vision. Unaishi kwa ajili ya leo tu. Pole sana. Kwa mtu aliye katika ndoa kama anaithamini basi hawezi kuwa na mawazo kama yako.
ha ha ha you wish!
Nina ndoa imara kama chuma. Nisome, unielewe kisha ujibu hoja. Play the ball, not a man.
 
Haya mambo ni muhimu.Sisi wengine wazee wetu waliacha unyago eti kwenda na wakati.Matokeo yake now ngono imekuwa too artificial as porno sites ndiyo zimekuwa main source of information!
 
Kama sikosei huu ni utamaduni ulioanzia nchi za magharibi lakini wenyewe yao huwa ni mabinti marafiki wa yule mwanandoa mtarajiwa hukutana na kumfanyia sherehe ya kumpongeza na pia kumuaga ktk kikundi chao cha wasioolewa. Lakini kama kawaida yetu wabongo huwa tuna tabia ya kuntransform jambo na kulitia nakshi ili mradi liendane na vichwa vya watu na mind za watu wengi huwa ni starehe na kingonongono.

Nakubaliana na mtoa hoja kuwa faida kubwa wanayopata ni vyombo lakini pia nikjaribu kupima uzito naona kama hazina faida kabisa kwani gharama inatumika kubwa sana kuliko ile ya vyombo vitakavyopatikana kama lengo ni vyombo basi hiyo gharama ni bora wangenunua vyombo kwani nina uhakika vingepatikana zaidi.

Ukija katika suala zima la utoaji wa elimu ya ndoa. Mimi nadhani kitchen party huwa haimjengi sana mwanamke kuwa katika muelekeo au kumjengea uwezo wa kuishi kwa maendeleo na mume wake bali imemuweka zaidi kama ni chombo ambacho kinaenda kumfurahisha mume kimwili zaidi, yaani kitandani na mapishi yenye mvuto usiopimika wakiamni kuwa hana mchango mwingine zaidi ktk ndoa zaidi ya huo.

Mimi naamini mkanganyiko huu wa elimu za ndoa baina ya mume na mke utaondolewa pale watakapoandaliwa kutokana na imani. Mfano wakristo (ndio ninajua zaidi kuhusu wao) huwa wanakuwa na kitu wanita semina za ndoa. Kule wnafundishwa kwa pamoja kuhusu maadili hata uchumi ni vipi wajikwamue au waendelee.

Nafikri hiyo ni solution tosha na si vitchen party.

NB: Kwanza nasika siku hizi watu wanaua send off na badala yake wanaifuse na ndoa kusave gharama lakini kitchen party iko pale pale hii ni kuonyesha ni kwa jinsi gani inavyoabudiwa kwa sasa
 
Thank you very much RayB. Actually Kitchen party ni utamaduni wa Kizambia ambao sisi Tanzania tulianza kuuiga miaka ya 90 na kuendelea. Hata kule Zambia wanawake wengi walioolewa huenda kwenye hizo parties kama kuwadanganya waume zao. Akifika pale anakaa kama nusu saa halafu huyoo anaenda kwenye date yake.
 
Back
Top Bottom