Umuhimu wa First Lady mwenye hekima

Umuhimu wa First Lady mwenye hekima

Naunga mkono mkuu. Ni usaliti. Watanzania tunasalitiana. Kumbe tunazisaliti nafsi zetu pia. Mapambano yataendelea mbele.
 
kuna video ya serena imetoka ya cctv akisindikizwa na watu wa Kitengo.....yaani kaumbuka vibaya pamoja na mwakyembe
 
Jamani mwenzenu nashawishika kuamini kabisa mheshimiwa rais wetu
ENL anaonewa saaaaana lakini wamuoneao hawajui kuwa ndiyo wanampandisha
juu na kumfanya hata waliokuwa wana chuki binafsi wabaini ukweli!!!!
Mungu ana maksudi na ndg Lowasa,anampitisha katika nyakati hizi za kudhihakiwa
na kuonewa ili utukufu wa Mungu ukainuliwe machoni pa Watanzani october 25
asubuhi! Asante sana rais wangu Lowasa kwa kuwa na hekima ya kutokuwajibu
wala kuwanyooshea kidole.Tupo pamoja ktk kuufikia ukamilifu wa dahari kupitia
mabadiliko ya kweli!! Viva Ukawa! Twende na mabadiliko 2015!!!!!!
 
Regina ni mke mwema ana kila sifa ya kuitwa first lady. Regina sio tu mzuri wa sura ila ni mwanamke mcha Mungu, mpole, mwenyw hekima na muelewa. Watanzania hatutajuta kuwa na first lady kama yeye.
 
Mtoa Mada Mbona Umeconnect Dot Na Comma?Unazungumzia Hekima Ya First Lady Kwa Upande Mmoja Tu Lakini Kwa Upande Wa Pili Instead Ya Kumuongelea Mama Magufuli,unamzungumzia Magufuli Kuwa Ni Dikteta Balance Mambo Na Uzungumze Kwanin Mama Magufuli Hafai Kuwa First Lady Na Ueleze Umejuaje Kua Hana Hekima Kama Mama Regina!!Na Magufuli Hakua Dikteta Alikua Anafuata Sheria Kama Mtu Kajenga Barabarani Unafanyaje Kama Serikali??
 
Mke wa rais ana jukumu kubwa la kumtia moyo mumewe. Awe ni mama ambaye katulia na mwenye moyo wa upendo na uvumilivu. Asiwe mtu wa kumtawala mumewe.

Tunataka rais anapoenda nyumbani, basi apokelewe na kutiwa moyo. Rais ni binadamu anahitaji leisure and support. Sivema kuwa na first lady anayemnunia mumewe au kumtolea mabegi nje.

Tukiangalia mapito aliyopita Edward Lowassa tunaona kwamba Regina Lowassa ni mama ambaye amekuwa bega kwa bega na mumewe katika kipindi kigumu na kirefu. Huyu anafaa kuwa first lady.

Lowassa ametukanwa sana. Kiasi kwamba watawala walitaka tusiangalie ESCROW,twiga waliopelekwa Qatar, madawa ya kulevya yanayoenda South Africa na China, Tembo wanaouawa kila siku, mabehewa mabovu yaliyonunuliwa, vivuko vibovu vilivyo nunuliwa, n.k. Sisi tuimbe wimbo wa Lowassa fisadi wakati wao wanatafuna nchi.

Sisi ambao ni waumini wa kanisa katoliki, ukienda kuungama kwa padre, hauna tena jukumu lakwenda kwenye umati kuwaeleza dhambi zako. Na yule muungamishi wako anapofungua pazia la maungamo, basi yote uliyoyasema yatabaki pale. Hawezi yapeleka nje. Lakini hiyo ni sheria ya kanisa, kama zilivyo sheria nyingine. Mfano, padre haruhusiwi kuwa na kimada au mke. Ndo maana wakati wa kupadirishwa tunalala kifudifudi ikiwa ni ishara ya kuufia ulimwengu na Bwana wetu ni Yesu. Kwa mapadre wasiowaaminifu utoa siri ya maungamo ya muumini. Wengine uwa na vimada. Wengine utoka kwenye upadre lakini ukiangalia umri wa watoto wao unagundua watoto walizaliwa akiwa bado padre.

Edward Lowassa alishiriki Richmond kwa namna moja au nyingine. Lakini huyu ni mtu ambaye ameadhibiwa kwa miaka minane. Katika huo muda, ametukanwa sana tena na vijana ambao walipo mtukana walipewa vyeo. Kwakuwa huyu EL ni binadamu, basi amejifunza na akipewa nafasi ata prove kwa umma kwamba yeye ni mwema.

Pombe Magufuli naye siyo msafi. Kauza nyumba za serikali n.k. Kuna kipindi alitaka kubomoa nyumba za watu bila kuwalipa fidia wakati barabara ilikuwa imefuata makazi ya watu. Viongozi wake wa juu walimwambia aache ubabe. Sasa ukimpa urais, akipitisha uamuzi wa kibabe, sisi wananchi tutaenda wapi kuomba msaada?

Wanakigamboni waliambiwa wavuke bahari kwa kupiga mbizi. Huyu hana ubinadamu.

Katika hawa wawili tuliopewa yaani Pombe na Lowassa, bora LOWASSA. Mama Lowassa zidi kumtia moyo mzee na ukiwa first lady jiepushe na tabia za watangulizi wako. A first lady should be role model for other ladies.

Aisee,
Siku nikiwa na kesi ya ufisadi lazima nikutafute.
Maana kwa namna hii lazima kesi yote ifutike ghafla
 
Back
Top Bottom