umuhimu wa check n balance bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

umuhimu wa check n balance bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Apr 23, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  Nyie Wadanganyika, mkiambiwa msiwape CCM zaidi ya nusu ya Wabunge basi mjue tuna maana ya kutabiria hali kama hii! Endapo leo hii CCM wangekuwa na viti 70 na vingine upinzani haki ya Mungu kuanzia Pinda na hata Makinda wote wangeenda nyumbani kulea familia zao! kama si Rais mwenyewe ukizingatia M4C ilivyoshika hatamu, badala yake tutaishia kuchekea chooni kwa maudhi! Uzalendo unaenda mbali zaidi ya kuongea, uzalendo unahusisha maslahi ya Taifa! Wataaalam walishaona hili tangu enzi za kale na ndo maana wakaweka dhana ya vyama vingi kwa mantiki ya kuwaweka watu wa kuvisha paka kengele! sasa hebu tujiulize kwa mabilioni yote yaale yaliyopotea Kikwete anahusika nayo vipi mpaka kuwa tayari kutetea mawaziri wake namna hii? hata kuhatarisha serikali yake? Kuna umuhimu wa kuanza kuchunguza account za kikwete nchini na ng'ambo kuona zimetuna kiasi gani tangu 2005! poleni sana Wadanganyika naanza kumfananisha Kikwete na rafiki yake mkuu marehemu Bingu wa Mutharika! Huyu Kikwete ni dictator! BTW wapi wale wapambanaji? Sita, Kilango, Sendeka na wengineo? Sita hafai kuwa Rais kama Lowassa tu...Urais ni taasisi inayohitaji ujasiri na si kuwindawinda vinafasi vya kujitengenezea sifa magazetini!
   
Loading...