Umuhimu wa Biashara yako kupatikana kwenye Directory

kinye

Member
Mar 14, 2009
38
11
Directory ni Sehemu ambayo inaorodhesha majina ya biashara mbalimbali za eneo husika.

Mara nyingi hizi Directory za biashara huonesha Sehemu biashara yako ipo, namba za Simu na tovuti yako.

Directory husambazwa Sehemu nyingi tofauti tofauti na hutumiwa na Wafanyabiashara kutafuta wateja na wateja pia kutafuta huduma mbalimbali.

Directory huorodhesha biashara kubwa na ndogo za Sehemu hio hivyo kufanya biashara yako kuonekana Sehemu nyingi na kujulikana pia.
Moja ya eneo muhimu ambapo Directory husambazwa ni kwenye Airport na mabalozi mbalimbali ambapo wawekezaji na wageni wengi hutembelea na kupenda kujua huduma zinazotolewa eneo husika.

Siku za karibuni pia Directory zimekuwa zikipatikana Online ambapo kwa sasa dunia ndipo inapoelekea.

Kuwepo kwa biashara yako kwenye directory ambayo ipo Online kunakusaidia kuonekana kwa biashara yako duniani Kote kwa urahisi kwani ni rahisi zaidi mtu kutumia Directory ya nnchi husika ili kupata aina fulani ya biashara anayo itafuta.

Kuonekana kwa biashara yako kwenye directory kunawajengea uaminifu wateja wako kuwa biashara yako ni ya uhakika.

Pendelea kuonekana kwenye eneo kubwa la Wafanyabiashara ili kupata ubora na uhalali zaidi sokoni.

Directory pia ni eneo jingine zuri la kutangaza biashara yako kwa Wafanyabiashara wenzio na wateja wako wanao tafuta huduma zinazofanana na za kwako.

Asante.

IMG_20210314_183929.jpg
 
Back
Top Bottom