Umuhimu wa 90% ya kura kwa mgombea

Umuhimu wa 90% ya kura kwa mgombea

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
803
Reaction score
870
"Mgombea anayekubalika na zaidi ya asilimia 90 ya wapiga kura waliojiandikisha si tu chaguo la kisiasa, bali ni dhihirisho la mwafaka wa kijamii uliojengwa juu ya matumaini ya pamoja. Uhalali wake unazidi mantiki ya ushindi wa uchaguzi; unakuwa kielelezo cha maridhiano ya kitaifa, ambako uongozi hauchukuliwi kama mamlaka, bali kama dhima ya kutekeleza matarajio ya walio wengi kwa ustawi wa wote." Alloyce, P.R.
 
"Mgombea anayekubalika na zaidi ya asilimia 90 ya wapiga kura waliojiandikisha si tu chaguo la kisiasa,
Utawapata kwa njia zipi?
Ni nchi gani hiyo iliyowahi kuwa na wapiga kura wa aina hiyo?
 
"Mgombea anayekubalika na zaidi ya asilimia 90 ya wapiga kura waliojiandikisha si tu chaguo la kisiasa, bali ni dhihirisho la mwafaka wa kijamii uliojengwa juu ya matumaini ya pamoja. Uhalali wake unazidi mantiki ya ushindi wa uchaguzi; unakuwa kielelezo cha maridhiano ya kitaifa, ambako uongozi hauchukuliwi kama mamlaka, bali kama dhima ya kutekeleza matarajio ya walio wengi kwa ustawi wa wote." Alloyce, P.R.
Unaishi sayari gani mwenzetu?
 
Utawapata kwa njia zipi?
Ni nchi gani hiyo iliyowahi kuwa na wapiga kura wa aina hiyo?
Mfano mzuri Rwanda, P. Kagame alishinda kwa asilimia 99. Na hapa kwetu kuna anayekubalika yamkini idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura wanamkubali kwa 98%+ duru zinasema anaweza kushinda kwa kishindo kwa kupata 96%+
 
Dunia mkuu.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusema x% ya waliojiandikisha kupiga kura (voter turnout) na kusema x% ya waliopiga kura. Mfano: mshindi akipata 90% ya waliopiga kura maana yake amepata 81% tu ya waliojiandikisha kupiga kura. Voter turnout ikishuka, percentage ya waliojiandikisha kupiga kura inashuka geometrically!

Kuna nchi chache sana duniani zenye voter turnout ya 90% au zaidi.
 
Back
Top Bottom