Umoja wa vilabu: Ubadhirifu mkubwa utpc

dira

Member
Jun 8, 2012
18
1
DIRA


Umoja wa vilabu nchini, utpc, umeingia katika kashfa kubwa ambapo rais wake keneth simbaye, mkurugenzi wake abubakar kasan na bodi nzima wanatuhumiwa kufuja fedha za umoja huo.


Habari kutoka vyanzo mballimbali ikiwemo ndani ya utpc yenyewe na baadhi ya vilabu vya mikoani, fedha hizo zinazodaiwa kufujwa na umoja huo, ni zile zinazotolewa na wafadhili kutoka nchi mbalimbali ikiwemo nchi ya Sweden ambayo ni moja ya wafadhili wakuu wa wanahabri hapa nchini kwa miaka mingi iliyopita.


Vyanzo vyetu vinazidi kueleza kuwa ukaguzi unaoendelea kwa vilabu vya mikoa yote nchini ndiyo umekuwa chanzo cha ugunduzi wa ufujaji na ubadhirifu huo na kwamba mbinu kubwa ambazo zimekuwa zikitumiwa ni kutumia stakabadhi zenye kuonyesha malipo ya uongo tofauti na gharama zinazotumika.


Mmoja wa wakaguzi ambao wanaifanya kazi hiyo ambao wanatembelea vilabu vyote kukagua huku wakiandamana na baadhi ya maofisa wa utpc wamesema ubadhirifu huo ni ufisadi ambao hauwezi kuvumiliwa kabisa haswa na wafadhili wenyewe ambao ukweli ni kwamba fedha wanazofadhili ni kodi kutoka kwa wananchi wao wanazokatwa kutokana na mishahara yao huko nyumbani kwao, mishahara ya jasho lao.


Baadhi ya mikoa ambayo inadaiwa kuhusika na ubadhirifu huo ni pamoja na tanga, Mbeya, Kilimanjaro, Morogoro na arusha. Ili kukabiliana na hali hiyo ambayo inadaiwa kuwapa kiwewe viongozi wa utpc mkurugenzi wa utpc kasan ameanza kuvitembelea vilabu hivyo na kukutana na viongozi wake ili kuweka mambo sawa hasa kwa vile mukutano mkuu wa utpc umekaribia.

Akiongea kwa uchungu jijini arusha mmoja wa wakaguzi hao ambae ameamua kuitoa siri hiyo kutokana na uadilifu wake tena baada ya kukataa kishawishi cha rushwa kutoka kwa maofisa wa utpc, amesema kuwa uongozi wa juu wa utpc kwa kushirikiana na vilabu mbalimbali ambao ni wanachama wake wamefikia hata hatua ya kudanganya malipo ya kodi za mapango ya vilabu hivyo ambapo utpc kupitia mkurugenzi wake kasan ameagiza viongozi wote watafute risiti zenye kuonyesha idadi kubwa ya malipo tofauti na yale wanayotozwa na wenye nyumba.


Hata hivyo hatua hiyo inadaiwa kuleta mtafaruku kati ya kasan na rais wa utpc keneth simbaye na baadhi ya waratibu wa vilabu vya mikoani ambao hawaafiki hali hiyo kutokana na uadilifu wao ambapo habari zingine zinaeleza ya kuwa tayari kasan ameanza mpango wa kumng’oa simbeye kwenye cheo cha urais.


mtoa habari huyo anazidi kudai kuwa pale penye mashaka kasan amekuwa awahakikishia waratibu ya kuwa swala hilo halina wasiwasi maana risiti hizo za malipo ya ukweli hazitawafikia wafadhili wala wakaguzi wa mahesabu badala yake ni zile za feki ndiyo zitatumiwa na utpc kuwasilisha kwa wafadhilli na kwamba hata aliekuwa waziri wa habari emanuel nchimbi na waziri wa habari wa sasa fenela mkangara wanaujua mchezo huo ambao unalenga kuvijenga vilabu na kuinua hali za kimaisha ya waandishi Tanzania.


Mmoja wa wakaguzi hao anazidi kuonyesha wasiwasi wake ni kwanini viongozi wa juu kama mawaziri na ambao wanachaguliwa na rais wanashiriki na kubariki uchafu kama huo wakati kuna mwenzao profesa mahalu yuko mahakamani hadi sasa kuhusiana na mchezo mchafu kama huo.


Tayari kasan anakabiliwa na tuhuma nyingine ya chinichini ambapo anadaiwa kuchochea migogoro kwenye vilabu ili pate nafasi ya kutumia fedha za utpc kwa wingi kwa madai ya kwenda kutatua migogoro hiyo. Pia anadaiwa kuzuia au kusababisha viongozi wenye misimamo ya dhati kuhusu matumizi ya fedha wasichaguliwe na wale walioko madarakani huwa nawatengenezea mazibgira waenguliwe kupitia chaguzi au migogoro ili wabaki wale wanakubaliana na ubadhirifu wake huo.

habari zinazidi kueleza ya kuwa baraza la habari mct limechoshwa na ubadhirifu anaoufanya kasan ambapo walishavionya vilabu vya habari hapa nchini kuhusu tabia chafu ya mkurugenzi huyo wa utpc lakini kasan amekuwa akiwatuliza viongozi wa vilabu kwa fedha ili waendelee kumuunga mkono, pia amewaamrisha viongozi wa vilabu vyote kuhakikisha wanakuwa na mahesabu aina mbili ya kwenda utpc kwa ajili ya kuwasilisha kwa wafadhili na mengine kwa matumizi ya ofisi. Taarifa ni kwamba baadhi ya waratibu wamepania kuandika barua za kujiuzulu kazi zao wakati wowote kuanzia sasa ili kulinda heshima zao.


Sasa kunamadai ya kuwa kasan amekuwa akishirikaina na baadhi ya waandishi wa habari kumchafua katibu wa mct mkajanga na hata kutafuta njia za kumng’oa madarakani kwa madai kuwa mkajanga anamfuatafuata.

Uchunguzi unaendelea.

DIRA NI CHANZO KIPYA CHA HABARI ZA UFISADI NA UBADHIRIFU, AMBAPO TUNAKARIBISHA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA UFISADI AMBAZO MAGAZETI YANASITA KUZITOA ILI ZIWEKWE WAZI MAMLAKA HUSIKA IZIFANYIE KAZI, SI HAPA DAR ES SALAAM TU BALI NCHI NZIMA. TUMA KWENDA dira1000@gmail.com
 
Nachelea kusema DIRA inaweza kuwa kama magazeti mengine ya udaku kinyume na lengo! Anyway, hongereni kwa ubunifu.
Lakini yaonekana dhahiri mwandishi una conflict of interest na rais wa utpc...

Isitoshe chanzo ulichotoa, mkaguzi si chanzo reliable kwa kuwa maadili ya taaluma hayaruhusu kuripot kwa asiyestahili, wewe ni nani unayereport uozo huo? Uliwahi kuckia CAG karopoka kokote madudu ya serikali kabla ya kufikisha report kwa rais?
Kama si uzushi, huyo mkaguzi kaenda kinyume na maadili ya taaluma yake na anastahili adhabu!

Taaluma ya ukaguzi ina misingi yake na kama ingekuwa wote tupo kama huyo aliyetajwa pasingekalika!
 
Back
Top Bottom