Umoja wa vijana wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar walaani kauli za mwenyekiti CHADEMA

nyie kweli mmelishwa limbwata! kwa nini mnafikiri mtu kua ccm ni jinai? endeleeni kuropoka tu, ...mnafikiri kuendesha serikali ni sawa na kunywa mbege? kwani ccm wanapokwambieni 'mkiona vinaelea vimeundwa..' mnafikiri wanatania? hili la katiba mmeachwa kwenye mataa wacheni ubishi!
wala sio kwamba kuwa ccm ni jinai, la hasha! ila kuwa na kiongozi wa chuo ambaye ni kada wa chama tawla hakuna kitakachofanikiwa katika kuweka maslahi bora ya wanafunzi. wale wasio makada wa ccm walifnikisha mengi, mpaka leo vijana wanakula matunda yao.

kama unakumbuka miaka ya 2005-2009 pale udsm, mabadiliko makubwa sana yalitokea pale,ikiwa inaongozwa na viongoz shupavu, wasiokubali kuhongwa na ccm. (mwita chacha, mtatiro, deo, bushi(josephat buhenyenge), silinde, owawa.........to mention few. lakin vijana wa leo hata wasipopata hela ya kujikimu hakuna anaeguna coz viongozi wao ni makada wa ccm. watu wameenda field bila hela, huku ccm wakitumia mabilion kwenye bunge la katiba huku wakijua akidi haitotimia na hivo kupelekea katiba kutopatikana, enzi zetu tungepachimba fasta.
 
Hili tamko la hawa majuha lingeanza hivi" Sisi vijana wasaliti wa nchi hii ......." Wachumia tumbo tu, njaa kali. Wote ni vilaza tu wa hivyo vyuo, vijana wa madesa. Ovyo
 
wala sio kwamba kuwa ccm ni jinai, la hasha! ila kuwa na kiongozi wa chuo ambaye ni kada wa chama tawla hakuna kitakachofanikiwa katika kuweka maslahi bora ya wanafunzi. wale wasio makada wa ccm walifnikisha mengi, mpaka leo vijana wanakula matunda yao.

kama unakumbuka miaka ya 2005-2009 pale udsm, mabadiliko makubwa sana yalitokea pale,ikiwa inaongozwa na viongoz shupavu, wasiokubali kuhongwa na ccm. (mwita chacha, mtatiro, deo, bushi(josephat buhenyenge), silinde, owawa.........to mention few. lakin vijana wa leo hata wasipopata hela ya kujikimu hakuna anaeguna coz viongozi wao ni makada wa ccm. watu wameenda field bila hela, huku ccm wakitumia mabilion kwenye bunge la katiba huku wakijua akidi haitotimia na hivo kupelekea katiba kutopatikana, enzi zetu tungepachimba fasta.

Na taarifa kutoka bodi ya mikopo zinasema kuwa zaidi ya wanafunzi 20,000. Watakosa mkopo ktk mwaka wa masomo 2014/2015!.
 
Hapa tulipofikishwa na sisiemu ni mahali pabaya sana.Ili kuitoa sisiemu madarakani lazima nguvu za ziada zitumike.Wewe kama msomi nakupa pole sana,ni msomi gani ambaye analia kuhusu haya yanayotaka kufanywa na CHADEMA? acheni kutumikia matumbo yenu kwa mabaki yanayosazwa na sisiemu mwisho wa siku mtakuja kuhukumiwa na makaburi yenu kupigwa mawe na wajukuu zenu.Ni kweli tamko hilo limetolewa na wasomi kutoka kwenye vyuo vyote ulivyovitaja au ni uzushi wako?
 
Sisi ni vijana wasomi wazalendo kutoka
vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko Dar es
Salaam, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM); Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU); Dar
es salaam University College of Education
(DUCE); USTAWI WA JAMII; Chuo Kikuu
cha Mtakatifu John (St. John); Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM); Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania (OUT); Kampala
International University (KIU); Dar es
Salaam Institute of Technology (DIT);
Institute of Adult Education (IAE);
Tanzania School of Journalism (TSJ);
College of Business Education (CBE), Chuo
cha Uhasibu (TIA) na Chuo cha
kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere.
Tunachukua fursa hii kulaani vikali kauli
zilizotolewa na Mh. Freeman Mbowe
ambae ni Mwenyekiti wa CHADEMA ya
kutaka kuitisha maandamano ya nchi
nzima bila kikomo pamoja na
kuhamasisha asasi nyingine za kiraia
kufanya na kuratibu maandamano kama
hayo ya CHADEMA kwa ajili tu ya kupinga
kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Tunawaambia watanzania wenzetu kuwa
tumekerwa na kusononeshwa sana na
kauli ya kibabe ya kiongozi huyu wa
CHADEMA ya kuhamasisha vurugu
ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha
umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha
vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo
huwa haviishi na hatimaye kuendelea
kulipakazia Bara la Afrika kuwa
halijastaarabika na siasa za kidemokrasia.
Tulimsikia akiahidi maandamano bila
kikomo kwa kibali cha polisi au bila kibali
cha polisi mbele ya wajumbe ambao
wengine sio watanzania.
Ndugu watanzania wenzetu, kauli kama hii
haiwezi kusemwa hata na Rais yeyote
ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu anaeongoza
kwa kufuata misingi ya sheria na utawala
bora, je Mh. Mbowe anapata wapi uhalali
na ujasiri huo? Maana Rais na Amiri Jeshi
Mkuu ambae ni dikteta anaweza kusema
lakini yule anaetawala kwa misingi ya
sheria, katiba na utawala bora kamwe
hawezi kusema kauli kama hizo.
Maneno aliyoyasema Mh. Mbowe
amejivalisha madaraka zaidi hata ya yale
ya Rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu
wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Lakini
kwa mtazamo wetu ni kuwa Mh. Mbowe
amejivalisha UDIKTETA ambao unatakiwa
kulaaniwa na kila mtanzania aliyeko
ndani na nje ya nchi hii. Uzito wa kauli
zake haubebeki na mtu yeyote kwenye
taifa hili. Hatuna shaka kuwa ametoa kauli
mbaya sana kuliko zote za kisiasa ambazo
zimewahi kusemwa majukwaani.
Watanzania kwa ujumla wetu na makundi
yetu tukikaa kimya bila ya kuzilaani na
kuzikemea vikali kauli zake, tutakuwa
hatujitendei haki sisi wenyewe na pia
hatutavitendea haki vizazi vijavyo vya nchi
yetu. Ndugu zetu watanzania, kama
ambavyo yeye mwenyewe alisema kabla
ya kutoa amri kwa watu kuandamana
kuwa anaamini watanzania wapo tayari
kufanya mageuzi ili chama chake kingie
IKULU ya Magogoni.
Hayo yatafanikiwa endapo tu vijana
wataacha uoga, maneno ambayo
yanaashiria kutaka kuchukua uongozi kwa
nguvu bila kufuata misingi ya
kidemokrasia inayosimamiwa na serikali
iliyo madarakani.
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam tunasema
kuwa uzito na ubaya wa kauli hizi
unaonesha wazi kuwa Mh. Freeman
Mbowe hafai kupewa dhamana ya kuwa
Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa
vikosi vya ulinzi na usalama na pia
amedhihirisha kuwa CHADEMA haina sifa
ya kuiongoza nchi hii kwa sasa kwa
kufuata misingi ya demokrasia na
kudumisha amani, utulivu na mshikamano
wa watanzania kwa lengo la kudumisha
umoja, na muungano wetu.Tunaomba
watanzania mkumbuke na mtilie maanani
kuwa, Mh. Freeman Mbowe katoa kauli
hizi akiwa raia tu wa kawaida.
Je itakuwaje akiwa Rais wa nchi na Amiri
Jeshi Mkuu wa Vikosi vyetu vya Ulinzi na
Usalama wa nchi hii? Kwa maoni yetu ni
kuwa kwa upeo na mtazamo wa akili yake
hakuna atakaebaki salama ndani ya nchi
hii kwa kuwa atatuingiza kwenye vita vya
wenyewe kwa wenyewe na pia atatuingiza
kwenye vita na nchi majirani. Hafai, hafai,
hafai hata mara moja kuwa Rais na Amiri
Jeshi Mkuu.
Ndugu watanzaia, hivi ni mtu gani
anaeweza kuishi kwa amani na viongozi
kama Mbowe na wenzake wanaotumia
ubabe kwenye maisha ya kawaida ya kila
siku?
Na hapa ndipo wanatuthibitishia kuwa
Mh. Freeman Mbowe na Kikundi cha
viongozi wa chama chake wote karibu
wameshindwa kuzichunga na kuziweka
pamoja familia zao na hatimaye
zimesambaratika kwa ubabe huo huo,
hivyo hawataweza kutuongoza na
kutuweka pamoja watanzania ili tuishi
kwa amani.
Ndugu watanzania wenzetu tumebaini
kuwa Mh. Freeman Mbowe na viongozi
wenzake wa CHADEMA wanatumia
maandamano na damu za watanzania
kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao
hawaitakii mema nchi yetu.
Wakiaandaa maandamano, wanapiga
picha na kuwapelekea wafadhili wao,
wanapata fedha, wanajenga majumba na
kununua magari ya kifahari na kusafiri
ulaya, marekani na familia zisizo rasmi
kwa kujificha kwenye pazia la
DEMOKRASIA huku watanzania
wakiendelea kuathirika na maandamano.
Hapo ndugu watanzania hakuna
DEMOKRASIA bali tunaona DOMO-KRASIA
na BONGO-KRASIA, yaani wanatumia
ulimi na akili ndogo za kitoto kujinufaisha
na familia zisizo rasmi kwa siasa za
ulaghai, ghilba, fitina, majungu, choyo,
chuki, usanii wa kisiasa na uhaini
alioutangaza Mh. Mbowe.
Ndugu zetu watanzania, fahamuni kuwa
Mh. Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa,
Tundu Lissu, Godless Lema, Mchungaji
Peter Msigwa, Hezekiah Wenje na wengine
wana familia. Swali je mmeshawahi
kuwaona wake, watoto, na ndugu zao wa
karibu kwenye maandamano yoyote yale
waliyowahi kuyaandaa? Siku zote
huwaambia watu wao
hao bakini majumbani mtadhurika.
Pale damu za watanzania zinapomwagika
kwenye maandamano baadae huwa
wanajifungia na kushangilia ushindi
mkubwa wa kuvuna mabilioni ya fedha za
kigeni, kwa kuwa huwa wanapiga picha
matukio hayo na kwenda kuonesha
wafadhili wao kwa taswira kwamba
demokrasia inanyanyaswa.
Wanakinga mabilioni ya fedha za kigeni
wanatia kwenye akaunti zao,
wanagawana, na mambo yao yanaenda
sawasawa, huku watanzania wengine
wakiwa wana vilio vya kupoteza ndugu na
baba zao, waume, wake, wapenzi/
wachumba, na watoto wao na kadhalika.
Swali, kwanini hawaoni umuhimu wa
kujali utu, ubinadamu na uhai wa
watanzania wengine? Sisi umoja wa vijana
wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar
es Salaam tunapenda kuwahakikishia
kuwa thamani ya maisha ya watanzania
wote au hata kwa mtanzania mmoja ni
kubwa sana kuliko hiyo katiba mpya
wanayoidai.
Tunawaomba watanzania wenzetu
msikubali kufanywa kama mbuzi wa
kafara na watu wenye tamaa, pupa,ulevi,
na uroho wa madaraka kama hawa akina
Mbowe na kundi lake. Tusijiendee tu kama
kuku aliekatwa kichwa halafu akaachiwa
atembee, na tusishikiwe akili zetu kama za
mbayuwayu kwani “Akili za Kushikiwa,
ongeza na zako”. Tuwakataeni wanasiasa
uchwara waliofilisika kihoja na kutaka
kuwatumia ili kujinufaisha.
Wanataka kutupeleka wapi? Ni dhambi
isiyosameheka kulitumbukiza taifa hili
katika machafuko yenye majuto makubwa
kama ya Misri, Syria, Afrika ya kati, Libya,
Sudan ya Kusini na kwingineko.
Tusikubali watupeleke huko, waacheni
waende wenyewe kama wanaweza. Kwani
nchi yetu ina mgogoro wa kisiasa?!!!!!
Waulizeni wanataka nini?
Ndugu watanzania wenzetu, tunaomba
mjue kwenye nchi hizo hizo zenye
demokrasia pevu watu wa aina ya Mh.
Freeman Mbowe (hasa kwa kauli zake
alizozitoa juzi tarehe 14.09.2014)
wanaotaka kuvuruga na kuvunja misingi
mikuu ya utaifa wao (core values) kama
vile amani, usalama na umoja huwa
hawavumiliwi hata kidogo.
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam
tunaviomba vyombo vyetu vya dola
visizivumilie kauli kama hizi zilizotolewa
na Mh. Freeman Mbowe hata mara moja.
Kwani vyombo vya dola vina dhamana ya
kulinda, kutunza na kuendeleza amani na
utulivu wa nchi yetu. Umoja wetu, kwa
heshima na taadhima
kubwa, tunaviomba vyombo hivi
kumchukulia hatua kali za kisheria Mh.
Mbowe kwa kauli hii ya kutishia uvunjifu
wa amani kabla hajaiingiza nchi yetu
kwenye machafuko ya kisiasa.
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam hatutaki
kuona vijana wenzetu na watanzania wote
kwa ujumla wakiathirika kwa ujinga huo
wa maandamano yanayofanywa mradi wa
kutafuta fedha.
Kwani maandamano hayo yatawaathiri
wana vyuo wa Dar es Salaam pamoja na
kuathiri shughuli nyingine za kiuchumi, na
kijamii za wananchi wa kawaida. Kwa nini
shughuli zetu na za wananchi zisimame
kwa sababu tu ya machafuko ili Mh.
Mbowe apate picha za kwenda kuuza huko
kwa wafadhili wao?
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam tulisikiliza
na kutazama hotuba ile kwa umakini wa
hali ya juu,tunapenda kuwathibitishia
kuwa hotuba ile haikuwa ya kisomi,
ilikuwa haijengi chama chake wala ilikuwa
haijengi nchi yetu isipokuwa ilikuwa ya
kibabe, ilikuwa ya kejeli,ilikuwa ya
kichochezi iliyolenga kuvunja misingi ya
amani na utulivu wa nchi yetu.
Ni matumaini yetu kuwa hata kwa
mwanafunzi wa shule ya msingi hawezi
kujifunza kitu chochote cha maana kutoka
kwenye hotuba ile. Hotuba ya Mh. Mbowe
haiwezi kutusaidia kujenga taifa lenye dira
kwa vizazi vijavyo.
Mwisho, Sisi kama umoja wa vijana
wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar
es Salaam, tunawataka watanzania
wenzetu mzipime na kuzitafakari kwa
makini kauli za Mh.Mbowe, na kujiuliza je
anafaa kuwa kiongozi wa nchi hii?
Asanteni kwa kutusikiliza, Mungu Ibariki
Tanzania, Mungu Ibariki Afrika Imesomwa
na Mussa Omari, Mwanafunzi OUT, kwa
niaba ya umoja wa vijana wazalendo wa
Vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam.
Tarehe 17.09.2014
 
Mpepata zile chenji siyo! Vijana WAZALENDO au WAJAAPUMBA TU?!! Nyie pigieni magoti BOOM basi. ili litoke.
 
Siamini kama hao ni wasomi kweli. Kama hao ndio wasomi wa Tanzania, basi nchi ina hali mbaya!
 
Wana ccm wanaojifanya kuvaa joho la wasomi. Wasomi hawana ujinga huo na uoga huu. Nilisha sema, watu wa dizaini hii walikuwepo wakati vijana akina Nyerere, Kawawa na wengine wengi wakipoanza vuguvugu la kudai uhuru wakwanza. Walikua anasema Tanganyika bila ukoloni yaiwezekani. Walikua wasaliti wakubwa, ila baada ya uhuru walifaidi. Hata wakati huu, wakudai uhuru wa pili, wapo na watajitikeza kama wasomi, wanaharakati, kukatisha watu tamaa. Nawengi wanakua wapewa rushwa ya vijisenti vya kununua viroba na wanawuza utu wawo kwanamna hio. Wapuuzeni tuu, babazao wana taabika kutafuta ada a ya chuo, hali zao mbaya, wakuja hapa wamelewa viro na kuanza kuropokaropo.
 
Kama vyuoni siku hizi sanaviongozi wa stahili hii basi nchi hi ndo mana inarudi nyuma kila siku
 
wajinga washapata mikopo wajesahau. kuna wenzao wapo mitaani wamekosa mikopo hiwapo bunge la katiba lingesimamishwa walu labda wangepata zakuanzania
 
quote: tutakuwa
hatujitendei haki sisi wenyewe na pia
hatutavitendea haki vizazi vijavyo vya nchi
yetu.

reply:KAMA USOMI WENU UNATHAMINI NA KUTAMBUA MUSTAKABALI WA VIZAZI VIJAVYO,BASI KUTANENI TENA MTOE TAMKO KUHUSU MAPITIO ANGAVU YA MIKATABA YOTE YA RASILIMALI ZA UMMA,UPUUZWAJI WA MAONI YA WANANCHI KATIKA BMK,PENGO KUBWA KATI YA ULIE NACHO NA NISIE NACHO,UMASKINI ULIOTUKUKA KWA MAJORITY KATIKA NCHI YENYE UTAJIRI MKUBWA NA MENGINEYO AMBAYO WASOMI WETU NYIE MNAYAONA ILA HAMYAKEMEI KWA MASLAHI YA MNAYEMJUA.

conclusion:Ifike kipindi kuhudhuria madarasa katika vyuo vikuu kutofautishwe na usomi.
 
Vyuo vyote vilivyo tajwa ni vimeo na angalia wahitumu wao wa sasa hivi. Yote msomi hupambana kudai haki, na maendeleo yakweli. Walio andika huo waraka, unaona kabisa uwezo wao nimdogo mno waku dadafua mambo. Amakweli nitatizo unapokua na wana chuo wasio jitambua.
 
Back
Top Bottom