Umoja wa Mataifa wakumbwa na ukata

Umoja wa Mataifa wakumbwa na ukata

Display Name

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Posts
423
Reaction score
451
Umoja wa Mataifa unakabiliwa na ukata mbaya zaidi kuwahi kutokea na iwapo nchi wanachama zitashindwa kutoa michango yao ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Oktoba, Umoja huo utashindwa kulipa wafanyakazi wake na watoa huduma.

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameziandikia barua nchi wanachama zinazodaiwa.

Tatizo kubwa linalosababisha hali hiyo ni upungufu wa kati ya Dola Milioni 200 hadi 250 ambapo wanachama waliolipa michango yao ni 181 kati ya 193.

Inasemekana kuwa Guterres tayari amezikumbusha nchi wanachama kujitoa na kushughulikia hali ya ukata inayopitia UN na wafanye hima katika kulipa madeni yao kuunusuru Umoja huo kwani hadi sasa wamekusanya asilimia 70 pekee ya michango yote.

Ukata huo umeufanya Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kutumia akiba yake yote na hivyo kuwa na hofu ya baadhi ya shughuli kutofanyika kwa sasa.

Taarifa za makusanyo ya UN zinaonyesha kuwa nchi wanachama saba ambazo ni Marekani, Argentina, Venezuela, Brazil, Mexico, Iran na Israel ndiyo wadaiwa sugu wanaodaiwa asilimia 97 ya michango.
 
Hata EAC michango ya wanachama wake imekuwa changamoto, sasa wako kwenye process ya kupunguza wafanyakazi.
 
Naona Trump kaamua kukaza nati kidogo mayowe kila mahali.
 
Israel hawez toa coz kila wakati wanampigia kura za shutuma.
Umoja wa Mataifa unakabiliwa na ukata mbaya zaidi kuwahi kutokea na iwapo nchi wanachama zitashindwa kutoa michango yao ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Oktoba, Umoja huo utashindwa kulipa wafanyakazi wake na watoa huduma.

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameziandikia barua nchi wanachama zinazodaiwa.

Tatizo kubwa linalosababisha hali hiyo ni upungufu wa kati ya Dola Milioni 200 hadi 250 ambapo wanachama waliolipa michango yao ni 181 kati ya 193.

Inasemekana kuwa Guterres tayari amezikumbusha nchi wanachama kujitoa na kushughulikia hali ya ukata inayopitia UN na wafanye hima katika kulipa madeni yao kuunusuru Umoja huo kwani hadi sasa wamekusanya asilimia 70 pekee ya michango yote.

Ukata huo umeufanya Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kutumia akiba yake yote na hivyo kuwa na hofu ya baadhi ya shughuli kutofanyika kwa sasa.

Taarifa za makusanyo ya UN zinaonyesha kuwa nchi wanachama saba ambazo ni Marekani, Argentina, Venezuela, Brazil, Mexico, Iran na Israel ndiyo wadaiwa sugu wanaodaiwa asilimia 97 ya michango.
 
Sasa Iran vikwazo kila kukicha halafu awachangie wengine hata ingekuwa mie nisingetoa,venezuela mnavyomletea zengwe Maduro halafu munampigia simu awape donee😂😂😂 Usikubali kuwachangia.
Nalog off
 
Sasa Iran vikwazo kila kukicha halafu awachangie wengine hata ingekuwa mie nisingetoa,venezuela mnavyomletea zengwe Maduro halafu munampigia simu awape donee[emoji23][emoji23][emoji23] Usikubali kuwachangia.
Nalog off
Si ndio hapo aseee
 
Back
Top Bottom