R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali akiwakaribisha viongozi wakuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar kuzungumza na waandishi wa Habari kupinga kuhusika na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis, wakwanza (kulia) ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo Askofu Michael Hafidh na (kati) ni Katibu Mkuu Askofu Dickson Kaganga.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dikson Kaganga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo kukanusha kuhusika kwao na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyomuandikia Papa Fransis.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dickson Kaganga katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mnazimmoja.
Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Agostino Shao akijibu maswali ya waandishi wa Habari kwenye mkutano wa kupinga kuhusika kwao na Barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis. (kushoto) ni Askofu Shayo na (kulia) ni Askofu Dickson Kaganga