Umoja wa Afrika(AU) waitaka Kenya kutuliza hali

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki ametoa rai kwa viongozi wa Kenya kutafuta mwafaka katika mzozo unaondelea baina ya serikali na upinzani.

AU imeeleza kusikitishwa kwake na uharibifu mkubwa uliofanyika tangu kuanza kwa vuguvugu la maandamano mnamo Machi 21, 2023 huku watu kadhaa wakiwa wamepoteza maisha.

Aidha Moussa Faki amewakumbusha viongozi wa Kenya kwamba Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2022 ulifanyika kwa njia ya amani na hata Mahakama ya Upeo ikathibitisha hilo baada ya kuwasilishwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi.

AU imeihakikishia Kenya ushirikiano katika juhudi za kurejesha amani na utulivu.

20230328_134544.jpg
 
Back
Top Bottom