Kenya ina Al-shabaab, Uganda pia wameanza kuishambulia, Tz imedhibiti IS Kusini kama ilivyodhibiti Maimai na M23 wasivuke mpaka kuingia Tz. Kenya (kama ilivyo Uganda) imezungukwa na majirani walioko vitani e.g. Somalia, South Sudan, Ethiopia, kwa Uganda DR Congo, Rwanda nako hakujatulia sana kati yake na Uganda, Burundi moto umezima lakini bado majivu yanachoma.
Sifa za Tanzania ku-host AU:
1. Amani.
2. Miundombinu (nchi nzima inafikika kwa safari za anga, barabara, majini, reli (SGR 2 na MGR iliyokarabatiwa upya na kuongezewa excel), unawezatoka South Africa hadi Tz kwa reli.
3. Vivutio vya utalii (wageni wanapenda kuosha macho baada ya mikutano).
4. Shirika la ndege lenye ndege mpya za kisasa kubwa, wastani na ndogo.
5. Ukarimu wa wananchi.
6. Kumbi za kimataifa za mikutano Arusha, Dodoma na Dsm.
7. Iliwahi ku-host Kamati ya Ukombozi ya OAU.
8. Ina-host Mahakama ya UN ICTR.
9. Ina-host EAC.
10. Inatumia lugha 2 za Kiingereza na Kiswahili (zote ni lugha za AU).
11. Iliwahi ku-host Non Aligned Movement ambayo Mwl alijenga Hoteli ya 77 Arusha ku-accommodate Marais wa nchi 77 waliokuja kuchakata wazo la Kutofungamana na upande wowote wakati wa vita baridi ya dunia.
12. Ina vikosi imara vyenye hadhi ya kulinda amani duniani; vikosi vyenye ithibati (accreditation) za UN, SADC, AU, EAC, GLR.
13. Ina viwanja vya ndege vyenye uwezo wa kuwa hub kwa wanachama wa AU.
14. Anga yake ni salama kwasababu imefunga miundombinu ya rada 3 mpya zenye uwezo wa kuongoza safari za ndege za kwenda kwa majirani, e.g. ndege zote za kiraia zinazoingia na kutoka Kigali na Bujumbura zinaongozwa na rada za Tz kasoro za kijeshi tu. Anga ya Tz ni salama kwa asilimia 100.
15. Ina hoteli zenye hadhi ya viongozi wa kitaifa na kimataifa.
16. Haina lockdown.
17. Ina Hospitali zenye huduma za kibingwa (wanaweza kutibiwa Marais na wajumbe wa mkutano).
18. Ina fursa lukuki za uwekezaji, wajumbe-wanachama wanaweza kuvutiwa kushawishi raia wao waje wawekeze kwasababu miundombinu ya usafiri, maji, nishati, usalama, amani nk vipo Tz.
19. Kuna huduma za Kibenki za kimataifa.
20. Tz inaongoza Afrika kwa uwekezaji katika sekta ya Telecom. Mkongo wa mawasiliano ya kielektroniki ya kasi kubwa na gharama nafuu umesambaa nzi nzima kasoro mikoa miwili tu ikiwemo Simiyu (ambayo nayo tyr ilishafikiwa zamani wkt ilipokuwa bado ndani ya mkoa wa Shinyanga, baada ya kugawanywa ndiyo ikajikuta iko nje ya mkongo).
21. Iliwahi ku-host ziara za viongozi wa nchi kubwa duniani kama US, UK, China wakiwemo Makatibu Wakuu wa UN.
22. Whatnot?