Umoja wa Afrika (AU) Hauna Maana Kwa Waafrika

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,280
310
Umoja wa Afrika ambao upo naona hauna maana yoyote wa wananchi wa Afrika kwa vile upo kwa maslahi ya viongozi wa afrika walioko madarakani.
Nasema hivyo hasa ukianagalia mambo mbali mbali yanayotokea afrika mbaya zaidi Libya ambapo Rais Gadaffi anaua wananchi wake kama KUKU na hata kutumia ndege za kijeshi kushambulia raia wake ili mradi tu aendelee kukaa madarakani licha ya kutawala kwa miaka 42. Mimi sioni tofauti kubwa ya Gadaffi na Saddam Hussein
Waafrika wenzangu kama AU iko kimya inafaida gani kwa sasa kwet sisi wananchi
 
JE, ULIDOKEZWA....Katika muda wa zaidi ya nusu saa Mwalimu Nyerere na Kwame Nkurumah waliachiwa malumbano ya mjadala wa ''Africa must unite today''....Nkurumah ''akisupport the topic'' kwa lugha ya kiingereza kigumu na cha mshindo na kejeli kwa Nyerere wakati huo huo Nyerere ''akioppose the topic'' kwa lugha nyepesi ya kiingereza lakini ikiwa na uzito wa ''philosophical terms''.

Ndani ya mkutano huo ''OAU'' iligawanyika wengine ''wakisupport'' upande huu na wengine ''wakioppose'' upandde ule na mwisho wa siku Afrika haikuungana siku ile ile na tafsiri nyepesi Nyerere aliibuka kidedea licha ya kwamba ''kusupport'' ni rahisi kuliko kuoppose.

Nataka kusema nini hapa .....''AU'' ni chombo ambacho kimewekwa na wazungu ili wajue waafrika ni kwa nini wanataka kuungana na wao watuharibie vipi na ndiyo maana kuna wawakilishi kutoka ''EU'' ili kusoma ujinga na uerevu wetu.

Kwa hiyo hata Gaddafi anaupigania umoja huo{AU} ili awe raisi wa Afrika tu kama alivyo Mseveni na EAF...nasema hakuna jipya hata mnikate kichwa na kama leo raisi wa libya anawaua walibya kesho akiwa raisi wa afrika si atawaua waafrika.

NUKUSHI: NIMEMWONGELEA NYERERE NA MTAZAZAMO WA VIONGOZI WA AFRIKA NA MALENGO YAO....NA UZURI WAKE KWANGU SIO KWAKO.
 
Hivi jamani inawezekanaje Umoja wa Ulaya una laani mauaji anayofanya Gadafi kwa raia wake, hapa barani afrika umoja wa afrika uko kimya na wala hamna hata serikali moja ya nchi moja ya afrika iliyosimama kidume na kulaani mauaji ya kikatili . hii ina maana gani???????????
 
AU n hao viongozi wake wote ni wanfiki tu hawana kitu wanchokifanya zaidi ya kutapanya tu pesa za walipa kodi wao.
 
Mwenyekiti wa AU kwa sasa ni Rais wa Equatorial Guinea Dictator Teodoro Obiang Nguema Mbasogo huyu jamaa ni katili sana kuliko hata Gadafi anaua wapinzani wake na kuweka hela za taifa lake kwenye akaunti zake binafsi. Unategemea atoe tamko gani mtu kama huyu? Sana sana atasikitika jinsi madikteta wenzake wanavyong'olewa madrakani akihofia na yeye watamng'oa!
 
Nani wa kumnyooshea mwenzie kidole? JK wakati anajua alichakachua kura? Mugabe? Museveni - anachofanyiwa Kiiza Besigye tunakijua... kila kona ya Africa ni vuru vuru........... Kimsingi tuna umoja wa majambazi safeguarding their own interests.......
 
Back
Top Bottom