Umoja huu haramu wa waendesha bodaboda na bajaji! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umoja huu haramu wa waendesha bodaboda na bajaji!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiteitei, Sep 1, 2011.

 1. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,257
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  nimekuwa mara kwa ma ra naona ushirikiano wa hawa jamaa wanaoendesha bodaboda pamoja na bajaji na nimekuwa najiuliza serikali na polisi wako wapi?hawalioni hili! wamejijenga na kuwa na umoja ambao ikitokekea bahati mbaya ukamgonga kama sio kujigongesha kwenye gari lako basi cha moto utakiona, huwa wanaitana na wanaweza hata kukuumiza kama sio kukuchomea moto gari lako (hata hapa jf imesharipotiwa matukio yao) ni wazembe mno barabarani na hawafuati sheria za barabarani, juzi nimeona wanafanya fujo kwenye ofisi fulani inayoshughulikia maegesho na ushuru, barabarani nako ukiwakuta wakiwa wanaenda kuzika mwenzao huwa wanafunga kabisa barabara (nimelishuhudia maeneo ya tegeta dar) polisi/traffic huwa wanawaanngalia bila kufanya chochote, hivi jamani hawa jamaa wako juu ya mamlaka ya kisheria au? Onyo:ni bora unapopata ajali inayowahusisha ukawahi kukimbilia polisi ila ukitaka kutoa msaada unawezakumbwa na makubwa zaidi
   
 2. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  yamekukuta nn? Lakin hawa ni wavuta bange wengi ndo mana
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Polisi huwa hawawafanyi kitu kwakuwa bajeti ya mboga ya kila siku inatokana na madereva wa boda boda
   
 4. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2011
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa kweli hili ni balaa lingine, kama police hawatachukua hatua mapema basi jambo kubwa litatokea, watu wengi wanapigwa na hawa jamaa wa pikipiki, tena wengi hawana hata leseni, wanaendesha kwa fujo bila kufuata sheria. Labda wanasubili kigogo au mtoto wa kigogo mmoja atakapouliwa na hawa jamaa ndio wataona hili ni janga.
   
 5. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama IGP Mwema anajua na kuimani 'Vision na Mission' yake taasisi yake,pamoja na upuuzi na uvunjaji wa sheria kufanyika kwa uwazi kabisa Jeshi la Polisi wapo kama hawapo vile, sasa wamekuja na falsafa ya kuwafundisha Watz kutii sheria bila kushurutishwa,wapo watu ambao wameshangilia Falsafa hiyo,lakini mimi ni mmoja wa wale ambao wanaona hiyo falsafa ni 'copy and Paste' sijui toka wapi ? Sababu hapa TZ polisi hawana muda wa kushurutisha watu kutii sheria na hakuna juhudi zozote ambazo zinachukuliwa na Jeshi la polisi kushuritisha utii wa sheria,shaka yangu nyingine ni uelewa wa sheria zenyewe ambazo au wawashurutishe watu kuzitii au wawaelimishe wazitii bila kushurutishwa.
  Kwa swala la Usalama barabarani nafikiri pana OMBWE la Uongozi ambalo kulipunguza ni kuondoa uongozi wote wa Idara ya Usalama barabarani,mfano mmoja ni huo umoja wa bodaboda wa kufanya fujo barabarani na kujichukulia sheria mkononi,mwingine ni uhuru wa kuvunja sheria ufanywao na Daladala na baadhi ya madereva.
  Kulikuwa na swala la kuongeza faini ya makosa madfogo ya Usalama barabarani hadi kufikia TTshs 300000, Binafsi niliona ni moja ya mitazamo ya kipuuzi kweli kweli,sababu kwa uelewa wangu tatizo si udogo wa faini bali ni usimamizi wa sheria,hiyo faini ingekuwa inalipwa na kila afanyaye kosa la barabarani hakika makosa na vurugu zitendazwo na daladala na madereva wapuuzi wengine zingekoma kabisa,na ingesaidia hata kupunguza foleni ambazo kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na kutotii sheria za usalama barabarani. Naamini siku ambayo jeshi la polisi likirudi kazini na kusimamia sheria za mbalimbali mambo mengi ambayo yanatokea kama ajali yanaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa mno. Swala la boda boda na ushirika wa kishetani ni bomu ambalo serikali inalilea kwani hata sisi wenye magari iko siku tutakataa upuuzi wa wenye boda boda hakika hapatatosha...
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa hapa Arusha walishachoma gari maeneo ya azimio. Inasikitisha sana.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mkuu nilipo sikia gari ya wanadada imechomwa moto baada ya kumgonga mwendesha pikipiki nilichukia sana lakini nilipo enda eneo husika na kuuliza chanzo cha hiyo prado kuchomwa nilitoka na mtazomo tofauti na nilioenda nao..yule dada baada ya kumgonga aliombwa amuwahishe polisi akawajibu gari lake litachafu alipobanwa akasema anaenda polisi kwenye kituo kidogo cha azimio, ndipo walipo ichoma gar
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mimi ningependa ushirikiano huu uendelee mpaka kwa machinga, wa mama masokoni maana serikali imeshindwa kusimamia sheria watu wanaonewa watu wana viburi kama huyo dada kisa mme wake ni mwanajeshi...kuna machinga wanaonewa hawana msaa wa kisheria, wengine wanakamatwa kwa uzurulaji wakifika polisi wanabambikiwa kesi hivyo bila ushirikiano watu tutaenelea kuteseka na kubaki kulalamika acha watu waungane na inapotokea kuonewa wanachukua hatua..
   
 9. N

  Nzagamba Yapi Senior Member

  #9
  Sep 4, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hawa watu ningekuwa namadaraka ningezuia aina hii ya usafiri,ajali zimekuwa nyingi sana halafu wakimbizi na najambazi wamejificha kwenye hii biashara,kiasi hata usiku wakiwa wanaenda kufanya uhalifu ni vigumu kuwashitukia kwani utajua ni usafiri unapita kumbe majambazi.imekuwa kero tupi
   
Loading...