Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,353
- 23,758
Ndugu zangu Watanzania,
Mheshimiwa Ummy Mwalimu Waziri Mstaafu katika wizara mbalimbali ikiwepo wizara ya afya amejikuta katika wakati mgumu ,wakati wa mawazo ,wakati wa sintofahamu ,wakati wa mateso Ya moyo kibinadamu baada ya Jina lake kukwaa Kisiki na kukatwa katika vikao vya mchujo kamati ya siasa ya mkoa.
Ikumbukwe kwa kanuni za mwaka huu ni kuwa kuna Vikao vya kamati za mchujo ngazi ya wilaya na Mkoa .ambapo wilaya inaweza pendekeza majina yake na mkoa nao ukapendekeza majina yake au kupitisha na kubariki yale yaliyopitishwa na ngazi za wilaya.
Lakini baada ya mkoa kuna vikao vya sekretarieti kabla ya vile vya kamati kuu ambavyo ndio vitafanya uamuzi wa mwisho juu ya majina Matatu yatakayo kwenda kupigiwa kura na wajumbe . Kwa hiyo mtu anaweza akawa alikatwa na kutokupendekezwa na vikao vya wilaya na mkoa lakini kamati kuu ikarejesha jina kuwa miongoni Mwa majina Matatu yatakayo pigiwa kura na wajumbe.
Kwa hiyo Kamati kuu ndio Mwamuzi wa Mwisho wa mtanange huu wa kukata na shoka na ambao mtu yupo tayari kufanya lolote lile kupata nafasi hii ya Ubunge.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.