Umiliki wa TBC,

Wabunge wautilia shaka mkataba TBC, Star Media Send to a friend
Monday, 23 May 2011 21:54
0diggsdigg

Ramadhan Semtawa
WABUNGE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, wamehoji sababu za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuingia mkataba waliouita wa ovyo na hatari na Kampuni ya Star Media ya China wakisema kuwa ni kama kitanzi kwa shirika hilo la umma.

Wakichangia katika taarifa ya hali ya TBC na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dar es Salaam jana, wabunge hao kwa pamoja walionya kuwa mkataba huo unaweza kuwa kaburi la kuzika shirika hilo siku za usoni.
Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola aliyeichambua ripoti hiyo kwa kina huku akimbana Mwenyekiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia kuhusu kisingizio kwamba shirika hilo lilipata hati yenye shaka kutokana na mali za ubia kati yake na Star Media kutokaguliwa.

Lugola akichambua kipengele kwa kipengele, alipinga madai ya Nyachia kwamba hati hiyo ilitokana na wabia wao, Star Media na kusisitiza: "Ubia unaouzungumzia hapa ni pande mbili, sasa kama ni hati yenye mashaka na nyinyi TBC mmo. Ninyi ndiyo mliingia mkataba huu."
Mbunge huyo alisema mkataba huo hauko wazi, kitu ambacho kinaweza kufananishwa kama mazungumzo tu kati ya watu wawili wanaofahamiana.

Alisema Star Media, kwa mujibu wa mkataba huo, inao uwezo wa kuuza hisa zake asilimia 65 na kujitoa, kitu ambacho ni cha hatari endapo atakuja mbia mwingine ‘mwendawazimu.'

Alisema hata vipengele vya mkataba kumbana mbia kwa ajili ya ulipaji kodi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haviko wazi na kuongeza, hiyo inaweza kuwa kama mchezo wa baadhi ya kampuni kuingia kisha kubadili majina na mamlaka hiyo ya mapato kukosa mapato.

Akitolea mfano alisema Kampuni ya Celtel iliwahi kuingia nchini na kujitanua kwa kasi kwa kutumia miundombinu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ikitumia mgongo wa ubia kati ya kampuni hiyo ya umma na MSI/Detecon.

MSI Detecon iliwahi kununua hisa asilimia 35 za TTCL, huku ikiendesha menejimenti ya kampuni hiyo nyeti ya nchi, lakini hadi inaondoka Februari 23, 2005 baada ya kumalizika ukiritimba wa miaka minne iliacha deni la takriban Sh20 bilioni, huku Celtel sasa ikiwa imekua kwa kasi.

Luoga alisema TBC pia ilikiuka taratibu za ununuzi kwa kutumia zaidi ya Sh8 bilioni ambazo sehemu zilinunua mafuta katika Kituo cha Victoria bila mkataba wa maandishi, lakini menejimenti ikitoa sababu kwa CAG, kwamba uamuzi huo umejikita kiuchumi zaidi kwani umekwepa foleni na umbali wa kilomita kumi na moja kwenda Wakala wa Huduma na Ununuzi Serikalini (GPSA) Kurasini, ambao wana mkataba na Serikali.

Baada ya Mwenyekiti wa kikao hicho, Deo Filikunjombe kuona maswali ni mengi kuliko majibu, aliamua kusitisha kikao huku akiahidi kuwaita Makatibu Wakuu wa Hazina, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na Mtendaji mkuu wa TBC, ili kupata maelezo ya kina kuhusu mkataba huo.

Filikunjombe pia alihoji juhudi zinazofanywa na TBC kukusanya deni la Sh5.5 bilioni na kuonya kuwa kama hakutakuwa na jitihada za kushughulikia suala hilo, shirika hilo litakufa siku za usoni akisema lilianza vizuri lakini sasa linakwenda kwa kusuasua.

Awali, Nyachia aliahidi kuwa bodi yake itahakikisha hati chafu na zenye shaka hazipo tena na kuwa atasimamia taratibu za utawala bora katika ununuzi na kuibana Star Media iweze kwenda sawa na mkataba husika.

------Mwananchi------
 
Hujafanya utafiti unakurupuka tu kushutumu na kutuhumu. Unajuaje labda wana mkataba maalum wa kufanya kazi hiyo kwa malipo tofauti na hivyo unavyofikiria? Kwani kuuza ving'amuzi si ni agency ambayo ina makubaliano maalum?

Ndugu yangu yaliyowekwa kwenye mjadala ni maswali kwa lengo la kutaka kujua, sasa unaweza kupima mwenyewe nani amekurupuka bila kuelewa vizuri jambo hili. Si kila kinachoandikwa kinalenga kuchafua watu au taasisi fulani bali wengine tunahitaji kueleweshwa so ni vizuri kulielewa jambo kabla hujalitolea maoni yako.
 
Jamani tuume na kupuliza! lakini ukweli siyo huo
Iko hivi
Star Media ya Nje Imeungana na TBC ya tanzania wakazalisha kitu kinaitwa Star Times ili kutoa huduma za Digital broadcasting kwa TZ hivyo TBC ina share Star Times ,Ni ngapi kwa ngapi hilo sina takwimu kwa sasa.

Kwa lugha nyinge ni kuwa Star Media+TBC=Star Times

Kazi njema.

Ndugu yangu sikio la kufa halisikii dawa. Jamaa ni watu wa kutuhumu bila hata ya kuwa na ukweli na wanakera sana. Unakuwa na watu mbumbumbu ambao hawajijui kwamba ni mbumbumbu na hao ndiyo Mods wanawapa nafasi ya kushinda humu JF huku wakitoa utumbo wao!
 
Ndugu yangu yaliyowekwa kwenye mjadala ni maswali kwa lengo la kutaka kujua, sasa unaweza kupima mwenyewe nani amekurupuka bila kuelewa vizuri jambo hili. Si kila kinachoandikwa kinalenga kuchafua watu au taasisi fulani bali wengine tunahitaji kueleweshwa so ni vizuri kulielewa jambo kabla hujalitolea maoni yako.

Huwezi kujifanya unataka kujua na huku tayari umeshahukumu kwamba kuna mchezo mchafu. Ungekuwa unataka kujua unge-pose swali lako katika namna ambayo haitoi conclusion kwamba tayari kuna ujanja wakati hujui lolote.
 
Kusema kwamba swali limeshahukumu na limetoa conclusion hiyo ni tafsiri yako binafsi ambayo si ya kweli, aliyetoa wrong conclusion ni wewe.
 
Ndugu yangu sikio la kufa halisikii dawa. Jamaa ni watu wa kutuhumu bila hata ya kuwa na ukweli na wanakera sana. Unakuwa na watu mbumbumbu ambao hawajijui kwamba ni mbumbumbu na hao ndiyo Mods wanawapa nafasi ya kushinda humu JF huku wakitoa utumbo wao!

Acha ubabaishaji hakuna aliyetuhumu hapa yaliyotolewa hapo ni maswali, na kutokuwa na ukweli ndio hupelekea mtu kuuliza, ndio maana hata wewe ulichokifanya ni kuquote jibu la Mr.Byabato ungekuwa sio mbumbumbu ungetoa ukweli unaoufahamu wewe binafsi.
 
Huwezi kujifanya unataka kujua na huku tayari umeshahukumu kwamba kuna mchezo mchafu. Ungekuwa unataka kujua unge-pose swali lako katika namna ambayo haitoi conclusion kwamba tayari kuna ujanja wakati hujui lolote.

Me nnadhani binaadamu ameubwa na hisia ndani yake,kisaikolojia alichokihisi mtoa mada ni mambo yaliyopo adharani(mkataba baina ya TBC1/na Star times)haya yamepelekea kutaka kujua na humu jamiiforum pengine wapo wenye data kamili watujuze tuelewe ,na pia kumbuka TBC1 ni Mali ya Watz wote sbb inaendeshwa na kodi zetu wananchi.
 
siyo ustaarabu kuhusisha kila jambo baya na ccm, huo ni uvivu wa kufikiri na ujinga uliopitiliza katika upuuzi wa mawazo ya mwanadamu

usitake watu tukutukane asubuhi yote hii "shx$$$$$%+&//$$$'@zi" we muone kwanza masabri yako.!!!
hivi hata kama ulikuwa unafeli darasani hata mame na mabaya hujui kutofautisha? anayeteua mkurugenzi wa hiyo TBC ni nani? si ni huyo zoba wako aliye DC saa hizi? serikali inayosain mikataba ya wizi ni ya nani na imeundwa na nani kama si CCM na kupitishwa na huyohuyo mtalii wenu? ...... bana ee usitutoe ktk mudy this mrng pls!
 
Hujafanya utafiti unakurupuka tu kushutumu na kutuhumu. Unajuaje labda wana mkataba maalum wa kufanya kazi hiyo kwa malipo tofauti na hivyo unavyofikiria? Kwani kuuza ving'amuzi si ni agency ambayo ina makubaliano maalum?

Huo ndiyo utafiti wake huyu Izack Mwanahapa katika kutaka kujua umiliki wa TBC. Ingekuwa ameshutumu ama amehukumbu asingeweka maswali hayo ili aeleweshwe. Anachohitaji yeye ni kueleweshwa tu nadhani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom