Mkuu NGO kote duniani sio inamilikiwa na mtu hapana. Kwenye NGO hakuna hayo Mambo ya wewe ulieanzisha kuamua. Maamuzi yanafanya na kikao Cha Bodi ya wakurugenzi (waanzilishi)... Kwahiyo sahau kuhusu hayo mawazo yako... NGO nyingi Tanzania hufa kwa sababu hiyo , unakuta watu Hawana common interests matokeo Yake ni kupishana kwenye baadhi ya Mambo hususani hela zinapoanza kuingia...
Hakuna namna unaweza kupindua kwenye hizo taratibu kwasababu NGO ni non profit making entity ni lazima Nyie Kama timu muwe wasimamiaji wakuu wa hilo ndio maana inabidi muwe watano na kuendelea. Kinyume na kampuni inabidi hata ukiwa peke yako unafungua.
Cha msingi Tafuta watu wanne ambao unajua kabisa sio wababaishaji kivile. Na ushauri mwingine katika hao watano hakikisha watu hao ni wale ambao hawana time na wewe na Wala hata hawataki kujishughulisha na issue zako ila wako tayari kukupa ushirikiano wa kufungua NGO , hiyo ndio mbinu watu wengi hutumia. Ila ukijichanganya ukaingia mikononi mwa watu wanaojifanya kujua unaweza kushangaza hata siku moja wanakuvua uanachama na kukutoa kwenye NGO ... Katiba ya NGO imetoa hiyo room kwa member yoyote anaweza kuvuliwa uanachama Kama amekiuka baadhi ya vitu , wakipiga kura imekula kwako. Hata Kama ukienda ku-appeal kwa msajili Kama wako na justification hiyo ndio nitolee japo wewe ndio ulikuwa mwenye wazo haijalishi.
Kuhusu kusikia hii NGO ni ya mengi au flani nadhani ni hapo hapo tu kuwa hao ndio pioneers wa mawazo , na si unajua hao wana hela hata Kama members wengine wakiwa na kidomo Domo hawawez kumpindua maana wanategemea hela toka kwake , issue huwa kwenye hivi vi NGO vya kimasikini.
By the way NGO kwasasa hazina issue labda ujikite kwenye NGO za Miradi ya Afya na Kilimo. Hapo lazima uule.
Sent using
Jamii Forums mobile app