Umiliki wa NGO Tanzania

bachelor sugu

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,674
2,000
Habari za usiku watanzania wenzangu..

Naomba kuuliza hili jambo kwa wanaofahamu..

Nimekuwa na mpango muda mrefu wa kuanzisha NGO itakayojihusisha na nyanja fulani ya maisha ila nikawa nasuasua ila kwa sasa nimedhamiria kwa dhati.Ni hv miongoni mwa masharti ya uanzishaji wa Ngo lazima muwe kikundi cha watu wasiopungua 5 kama FOUNDER members mtimize na yale mahitaji mengine ya Katiba,na zile fomu zingine ,sasa maswali yangu ni haya.

Je ile tunayosikiaga kuwa mtu fulani anamiliki NGO yake inakuwaje hapa??

Je kama lazima iundwe na waanzilishi wasiopungua 5 ss hapo maamuzi ya mwanzilishi mkuu si yanakosa nguvu ya kimaamuzi hasa pale inapotokea miongoni mwa waanzilishi wenzio kuwa watata?
Hawa tunaowaita wamiliki wa hizi Ngo wanapataje nguvu ya kuwa na maamuzi ya hela wanazozipata kutoka sources mbalimbali??

Labda naomba tu mwenye uelewa mpana wa maswala ya uendeshaji wa hizi taasisi anieleweshe vizuri..

Ngo yangu mm haitategemea sana funds toka kwa wafadhili bali ada za wanachama maana najua kuna watu wataanza oooh Ngo zilikuwa enzi za mkwere n.k ss hv watu wanakufa njaa...

Naomba kuwasilisha.
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,460
2,000
Mkuu NGO kote duniani sio inamilikiwa na mtu hapana. Kwenye NGO hakuna hayo Mambo ya wewe ulieanzisha kuamua. Maamuzi yanafanya na kikao Cha Bodi ya wakurugenzi (waanzilishi)... Kwahiyo sahau kuhusu hayo mawazo yako... NGO nyingi Tanzania hufa kwa sababu hiyo , unakuta watu Hawana common interests matokeo Yake ni kupishana kwenye baadhi ya Mambo hususani hela zinapoanza kuingia...

Hakuna namna unaweza kupindua kwenye hizo taratibu kwasababu NGO ni non profit making entity ni lazima Nyie Kama timu muwe wasimamiaji wakuu wa hilo ndio maana inabidi muwe watano na kuendelea. Kinyume na kampuni inabidi hata ukiwa peke yako unafungua.

Cha msingi Tafuta watu wanne ambao unajua kabisa sio wababaishaji kivile. Na ushauri mwingine katika hao watano hakikisha watu hao ni wale ambao hawana time na wewe na Wala hata hawataki kujishughulisha na issue zako ila wako tayari kukupa ushirikiano wa kufungua NGO , hiyo ndio mbinu watu wengi hutumia. Ila ukijichanganya ukaingia mikononi mwa watu wanaojifanya kujua unaweza kushangaza hata siku moja wanakuvua uanachama na kukutoa kwenye NGO ... Katiba ya NGO imetoa hiyo room kwa member yoyote anaweza kuvuliwa uanachama Kama amekiuka baadhi ya vitu , wakipiga kura imekula kwako. Hata Kama ukienda ku-appeal kwa msajili Kama wako na justification hiyo ndio nitolee japo wewe ndio ulikuwa mwenye wazo haijalishi.

Kuhusu kusikia hii NGO ni ya mengi au flani nadhani ni hapo hapo tu kuwa hao ndio pioneers wa mawazo , na si unajua hao wana hela hata Kama members wengine wakiwa na kidomo Domo hawawez kumpindua maana wanategemea hela toka kwake , issue huwa kwenye hivi vi NGO vya kimasikini.

By the way NGO kwasasa hazina issue labda ujikite kwenye NGO za Miradi ya Afya na Kilimo. Hapo lazima uule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani sana mkuu nimekusoma vizuri sana na kukuelewa pia.

Umenipa mwanga kwa kweli yaani japo kwenye uzi huu umecomment peke yako but amini umenipa maelezo yaliyoshiba..

Ni kweli NGO zimezimika kwa nyakati hizi ila ukituliza mawazo ukabuni idea ya ukweli bado una nafasi ya kusogea mbele..
 
Wazo Langu

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
1,379

Waanzilishi lazima MSIPUNGUE watano lakini Kati tao kuna Founders na Ordinary Members.
 
Jimbi

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
3,202
2,000
Huna wanafamilia? Hakikisha hao watano mnakua wewe, mkeo, dada, kaka na shemeji.
 
October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,676
2,000
NGO mpaka leo sina elimu kuhusu hii kitu.

1)Kwanini wengi wanakimbilia?

2)Faida yake kuwa chanzo cha kipato kwangu ??

Sina uwelewa kabisaaaaa.
 
Operand

JF-Expert Member
Jan 25, 2020
277
250
Natafuta NGO iliyokufa niifufue niiendeleze.
waanzilishi kama wapo tutapeana makubaliano

Karibu pm

Nipo diguzi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom