Umezuka ugonjwa unaoshambulia mimea ya mahindi

chilamanyika

JF-Expert Member
Nov 20, 2016
405
272
addc522a90dc16718297b0636585b81d.jpg
e7f119df9d1c43e3f7616391f19c3533.jpg


Ndugu zangu wakulima umezuka ugonjwa mbaya unashambulia mimea ya mahindi kwa kasi sana,
ugonjwa huu uta waathiri sana wakulima wa mahindi mkoa wa Rukwa iwapo haitadhibitiwa mapema.
 
addc522a90dc16718297b0636585b81d.jpg
e7f119df9d1c43e3f7616391f19c3533.jpg
Ndugu zangu wakulima,

Umezuka ugonjwa mbaya unashambulia mimea ya mahindi kwa kasi sana,
ugonjwa huu uta waathiri sana wakulima wa mahindi mkoa wa Rukwa iwapo haitadhibitiwa mapema.
Mkuu huo siyo ugonjwa bali ni funza anayeingilia hapo juu ya mmea na kutoboa, anaitwa maize stalk borer. Zamani tulikuwa tunamwangamiza kwa kutumia dawa ya unga inaitwa Thiodan powder 1%. Siku hizi naona wabatumia Mupocron, Duducron, Farm guard n.k
 
Huu ugonjwa ni hatari sana, hata mimi umeniathiri sana, Nilitumia dawa mbalimbali - duduba, thiodan, na dawa fulani hivi ya unga lakini bado ugonjwa uliendelea japo kasi yake ilipungua kidogo.
Wasi wasi wangu mkubwa ni kuwa hizi dawa tunazouziwa yawezkana ni fake, nilishangaa kuona thiodan bila kuweka maji mdudu huyo anakaa zaidi ya dakika 10 kabla ya kufa! Sasa ukiweka maji - si ndiyo hatakufa kabisa!
 

Attachments

  • DSC04393.JPG
    DSC04393.JPG
    222.5 KB · Views: 99
  • DSC04394.JPG
    DSC04394.JPG
    233.2 KB · Views: 93
Nasikia na mikoa ya kanda ya ziwa hawa funza..wanatafuna mazao sio mchezo..serikali iingilie kati angalau kwa kuwafahamisha wananchi na kutoa dawa kwa punguzo la bei..ili kulinusuru zao la mahindi.
 
Majivu kivipi maana hata mie umeathiri mahindi yangu sana

Baada ya kukoka kuni yanabaki majivu.
Miaka yote nalima shamba na wazee wangu nawaona wanaweka majivu kwisha habari.
Hata hivyo naamini wale wakulima wakubwa wanajua dawa yake.

Hii ni uzoefu wangu wa kienyeji.

KARIBU MBEYA.
 
Hili tatizo limewakumba wakulima wengi waliopanda msimu huu, hata kilimanjaro na arusha hili tatizo limeliona.
 
Nilipanda mahindi aina 4 lengo langu lilikuwa ni kujua aina ipi inafaa katika mazingira yangu kwa malengo ya kulima mahindi kwa kumwagilia wakati wa kiangazi. Kama nilivyoeleza kwenye post yangu hapo juu namba 9 nilishambuliwa na hao wadudu.
Jana 14.1.2017 nilienda tena shambani kuangali maendeleo; nimeona kuna aina ambazo zilistahimili wadudu hao. Aina ya kwanza ni Pioneer (picha DSC04516) na Lubango (picha Dsc04521)
 

Attachments

  • DSC04516.JPG
    DSC04516.JPG
    287.8 KB · Views: 87
  • DSC04521.JPG
    DSC04521.JPG
    451 KB · Views: 91
addc522a90dc16718297b0636585b81d.jpg
e7f119df9d1c43e3f7616391f19c3533.jpg
Ndugu zangu wakulima,

Umezuka ugonjwa mbaya unashambulia mimea ya mahindi kwa kasi sana,
ugonjwa huu uta waathiri sana wakulima wa mahindi mkoa wa Rukwa iwapo haitadhibitiwa mapema.
Mkuu! Huu ugonjwa upo karibu kila mahali! Mpaka sasa hakuna majibu ni dawa gani inasaidia kuwamaliza! Kama kuna mtu ametumia dawa iliyosaidia tafadhali atueleze wakulima ili tuitumie
 
Back
Top Bottom