Aina na sifa za mbegu mbalimbali za mahindi

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Nimekuwa nikifanya utafiti binafsi kwa kulima aina mbalimbali za mbegu za mahindi na kugundua yafuatayo.

1. ChapaTembo 719
Hii ni mbegu inayochukua muda mrefu kukomaa. Hukomaa baada ya miezi 4 hadi miezi 4 na nusu kutegemea na ukanda.

- Inarefuka sana kwenda juu hivyo si vema kuibananisha. Panda kwa sm75x30 one seed per hole.
Usiipande jirani na miti mikubwa huwa inaathirika sana na kivuli.
  • Panda mwanzoni mwa msimu kwani huchukua muda mrefu kukomaa km nilivyoeleza hapo awali.
  • Uzuri wa hii mbegu km utaitunza vzr hubeba mahindi 2 makubwa na yenye punje nene.
  • Punje zake ni nzito hivyo km utauza kwa kilo inalipa.

NB: Kwa sasa hii ndo mbegu inayopendwa sana na wakulima wa kanda ya kusini kwa mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Ruvuma,Rukwa na Katavi.Bei kwa kilo 2 inauzwa hadi 18,000,ikifuatiwa na DK 777 inayouzwa 15,000-16,000/=,na PANNAR 691.

Uchambuzi utaendelea kwa chapa tumbili 419 , 403na zinginezo.

Kilimo kinalipa km mkulima akiwa na taarifa sahihi.
 
Tembo 719.
download.jpg

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Huu Uzi mzuri sasa mboni umeishia Kati mkuu njoo uendelee basi na maelezo, usikatishwe tamaa na wanaokupinga katika utafiti wako wewe elezea kile ulichokifanyia utafiti tupo tunaopokea na kujifunza
 
Njoo uendelee na Uzi huu sio umeuanzisha alafu umeutelekeza tu hakuna muendelezo wowote Uzi unaelea tu
 
Nimekuwa nikifanya utafiti binafsi kwa kulima aina mbalimbali za mbegu za mahindi na kugundua yafuatayo.

1. ChapaTembo 719
Hii ni mbegu inayochukua muda mrefu kukomaa. Hukomaa baada ya miezi 4 hadi miezi 4 na nusu kutegemea na ukanda.

- Inarefuka sana kwenda juu hivyo si vema kuibananisha. Panda kwa sm75x30 one seed per hole.
Usiipande jirani na miti mikubwa huwa inaathirika sana na kivuli.
  • Panda mwanzoni mwa msimu kwani huchukua muda mrefu kukomaa km nilivyoeleza hapo awali.
  • Uzuri wa hii mbegu km utaitunza vzr hubeba mahindi 2 makubwa na yenye punje nene.
  • Punje zake ni nzito hivyo km utauza kwa kilo inalipa.

NB: Kwa sasa hii ndo mbegu inayopendwa sana na wakulima wa kanda ya kusini kwa mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Ruvuma,Rukwa na Katavi.Bei kwa kilo 2 inauzwa hadi 18,000,ikifuatiwa na DK 777 inayouzwa 15,000-16,000/=,na PANNAR 691.

Uchambuzi utaendelea kwa chapa tumbili 419 , 403na zinginezo.

Kilimo kinalipa km mkulima akiwa na taarifa sahihi.
Elimu nzuri sana hii, ila ni vema kuelekezana mapungufu ya mbegu husika pia, binafsi Kwa uzoefu wangu mbegu tembo 719 ni mbegu nzuri sana Kwa ukanda wote wa kusini lakini inakumbwa na tatizo la kuoza juu, hii inafanya wakulima wengi kupendelea pan 691, pamoja na DK777
 
Nimekuwa nikifanya utafiti binafsi kwa kulima aina mbalimbali za mbegu za mahindi na kugundua yafuatayo.

1. ChapaTembo 719
Hii ni mbegu inayochukua muda mrefu kukomaa. Hukomaa baada ya miezi 4 hadi miezi 4 na nusu kutegemea na ukanda.

- Inarefuka sana kwenda juu hivyo si vema kuibananisha. Panda kwa sm75x30 one seed per hole.
Usiipande jirani na miti mikubwa huwa inaathirika sana na kivuli.
  • Panda mwanzoni mwa msimu kwani huchukua muda mrefu kukomaa km nilivyoeleza hapo awali.
  • Uzuri wa hii mbegu km utaitunza vzr hubeba mahindi 2 makubwa na yenye punje nene.
  • Punje zake ni nzito hivyo km utauza kwa kilo inalipa.

NB: Kwa sasa hii ndo mbegu inayopendwa sana na wakulima wa kanda ya kusini kwa mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Ruvuma,Rukwa na Katavi.Bei kwa kilo 2 inauzwa hadi 18,000,ikifuatiwa na DK 777 inayouzwa 15,000-16,000/=,na PANNAR 691.

Uchambuzi utaendelea kwa chapa tumbili 419 , 403na zinginezo.

Kilimo kinalipa km mkulima akiwa na taarifa sahihi.
Ni Kweli hii ni mbegu nzuri,msimu uliopita niliilima na nikapata mavuno mazuri,Mahindi yanakuwa na punje kubwa na nzito hivyo Uuzaji wake hausumbui,sema shida ni tillers ndo zunakuwa nyingi,Kuhusu kuoza sio sana.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
DK 777.Hii mbegu ina punje ndogo hivyo unaweza panda eneo kubwa. Kwahiyo km bajeti inabana inakupunguzia gharama. Kwenye ekari moja badala ya kutumia vifuko 5 unaweza tumia vifuko 4.

Inazaa mahindi mawili mawili.Huchukua muda wa wastani kukomaa miezi 3.5 hadi 4 kutegemea na ukanda. Licha ya mahindi yake kuwa na punje ndogo ukiitunza vizuri inauzito mzuri. Pia ukikoboa ina pumba kidogo sana. Hata ikitokea umeipanda kwenye udongo dhaifu mbegu huzaa hata km imedumaa.

Ukiitunza vzr inaweza kukupa magunia 40-44 ya kilo 100.

Back
Top Bottom