umeyashika na kuyazingatia haya?

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Walawi: 11: 4 -5 "Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na wale wenye kwato katika miguu; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. Na sungura, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu,…… Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu ya iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msiile nyama yao wala msiiguse mizoga yao: hao ni najisi kwenu".


Walawi: 12:1 - 2 : Mwanamke akitunga mimba na kuzaa mtoto mume, ndipo atakuwa yu najisi siku saba; kama katika siku za kutengwa kwake kwa ajili ya ya hedhi, ndivyo atakavyokuwa najisi. Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake na huyo mwanamke atakaa katika damu ya kutakata kwake kwa siku thelathini na tatu na asiguse kitu kilicho kitakatifu, wala asiingie mahali patakatifu ……..


Walawi: 15:16 – 24“Na mtu yeyote akitokwa na shahawa yake, ndipo atakoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hata jioni. Na kila nguo, na kila ngozi, ambayo ina shahawa itafuliwa kwa maji nayo itakuwa najisi hata jioni. Huyo mwanamke naye ambaye mtu mume amelala nae kwa shahawa, wote wawili wataoga majini nao watakuwa najisi hata jioni .


Mwanamke yeyote kama anatokwa na kitu, na kitu chake alichotokwa nacho mwilini mwake ni damu, ataketi katika kutengwa kwake kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atatakiwa kumgusa atakuwa najisi hata jioni”. ……Na mtu yeyote atakaye lala na mawamke huyo na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi".........

Je, umeyashika na kuyazingatia haya?:
 
Du mkuu unaijua BIBLE vizuri kweli?au unameza tu kila kitu?kuna mambo mengine yameandikwa kwa sababu ya jamii aliyokuwa anakaa mwandishi/nabii kipindi hicho.
 
Maandiko ni maandiko. lakini shida inakuja kwenye tafsiri yake, hapo ndipo wasomaji na wachambuzi/watafsiri wanapoonekana!
 
Maandiko ni maandiko. lakini shida inakuja kwenye tafsiri yake, hapo ndipo wasomaji na wachambuzi/watafsiri wanapoonekana!

Ni kweli kabisa manake hata jamaa mambo aliyoyaandika hapo ukimwambia ayatekeleze hataweza hata moja.
 
Back
Top Bottom