Umewahi pata adhabu hizi??


Duh hapo kweli. Mtu akupige utasema si binaadamu au huna masikio na fahamu ya kuelewa jema na baya?!

Mie shule nilizosoma hakukuwa na bakora, adhabu kufagia au kumwagia maji bustani.

Na siku ningepigwa, mama yangu nna guarantee angewaendea huko huko. Hachukui kabisa mwanawe mtii kuonewa.

Keshawahi kuwaendea once, nipo form 3 nikagombwa mbele za wanaume kibaoo ati uniform yangu too flashy. Walijuta kumfahamu
 
hawa ni std 6 kama si 7.. wanasumbuliwa sana na balehe halafu inaonekana ni watoro sugu na wameanza kuvuta bangi. Safi sana mwalimu kwa kulijenga taifa lenye nidhamu
 
cha mtoto hizi, umeshawhi kauambiwa ufagie barabara ya Lugalo?
 
sijaona adhabu hapo!
nilipewa adhabu, yaani nikikumbuka mchozi unanitoka!
 
Adhabu kubwa zaidi niliyowahi kupata shule ni kufagia

Wewe utakua umesoma Saint Saint hizi za miaka ya juzi juzi maana sie wa Katavi kufagia ni sehemu ya wajibu wa mwanafunzi na tena usipofagia utapata adhabu sio ya kubeba matofali bali ni kufyatua matofali
 
hawa ni std 6 kama si 7.. wanasumbuliwa sana na balehe halafu inaonekana ni watoro sugu na wameanza kuvuta bangi. Safi sana mwalimu kwa kulijenga taifa lenye nidhamu



Uko sawa kabisa mkuu,kwa age group uliyoitaja mitoto mingine huwa inakuwa ni minunda afadhali ya Punda,na usipoipeleka kipundapunda namna hiyo basi ndio inaharibikiwa moja kwa moja,nasema hivyo wa sababu nimefundisha katika shule za msingi miaka mingi iliyopita na walewale niliokuwa nawapa adhabu leo tukionana huwa wananishukuru na tunacheka pamoja...
 
nyingi sana hizo enzi zetu na walimu walio toka JKT!!!!!tena siyo kuweka kichwani unaliinua kwa mikono,na magoti umepiga!!
 


kutoka kushoto
-huyu wa kwanza mwanafunzi gani hana hata shati la shule?
-anayemfuatia ni kiburi vibaya sana
-wa tatu hapo anatoa matusi ya kimoyomoyo kwa mwalimu
-wanne anajifanya amechomekea vizuri ili fimbo zisiingie
-huyu wa mwisho ndio mkuu wa hiki kikundi cha watukutu, hana shati la shule halafu ameweka mlegezo kama konda
 
hi ya matofali imezidi,mi ilikuwa yale matofali ya madogo,halafu kiwango cha juu cha fimbo nilizochapwa na mwalim zilikuwa 48,ukigusa **** anasema umefuta so anaanza upya kuchapa
 
hii ndio ilsababisha wanaume wanaojiremba kuwa wachache sana sababu ushababi ulianzia shuleni,tofauti na sasa shujaa ajue kuimba bongo fleva na kupiga viduku.

Umeona eeh..........kweli bana ndiyo maana mishoga inazidi, shule gani adhabu unayopewa eti uandike sentensi mbili au kuvunja biskuti
 
Hivi shule za english media nazo zina adhabu kama za kata!
 
Hapo bado bakora haijaanza kutembea! No kushusha mikono, aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…