Umewahi kuwa na rafiki mwiz/mdokozi na ulichukua hatua gani ulivyomgundua?

but why

Member
Nov 18, 2020
26
151
Nyumba tunayoishi tupo wawili ,mimi na mshikaj wangu wote mabachelor...ni nyumba ya vyumba vitatu ,sebule, jiko na choo...chumba kimoja tunakitumia kama stoo ...

Sasa yy ni mpenz wa PlayStation ila mimi hapana sanasana ni movies na mpira ..kutokana na kuwa ni mtu wa hayo magemu kuna washikaj mara nyingi wanakujaga hapa geto kucheza hzo mishe ..ikatokea mmoja miongoni mwao akazoea zaidi hata tukisepa kwenye harakat ilikuwa tunaweza kumuachia funguo na alikuwa free sana...

Sasa kwasababu tunaishi wawili tu ilikuwa rahisi kuacha pesa labda kwenye kabati tu bila kufunga au kwenye suruali ,sasa akaanza mwana kulalamika akiacha pesa chumban kwake anakuta pungufu au imetembea yote, ikawa mara nyingi analalamika hzo mishe..baada ya muda na mimi nikawa nahisi tofauti ,naacha sehemu kiasi kadhaa baada ya muda naona kama kimepungua na sikumbuki kuwah kukitumia...

Nilipocofirm ilipotea kama elfu 70 hv ambayo nilikuwa na uhakika sijaitumia ikabidi tujadili nini kinatokea hapa ndan,ratiba zetu mara nyingi zinafanana kutoka asubuh kurud jion hv,sasa kuna siku nilichelewa kutoka geto jamaa alishasepa.

Nikasikia mlango mkubwa unafunguliwa kuchungulia ni yule jamaa yetu wa magemu sasa sikushtuka kwa sababu mara kadhaa mwana anamuachiaga funguo lakin ile timing ya jamaa alipotoka na huyu kuja kulikuwa na possibility ndogo kwamba wameonana,ikabidi nimtext mshikaj kama alimuachia funguo huyu jamaa akakanusha,lakin hakuwa na uhakika kama alifunga mlango tukahisi inawezekana jamaa alipita tu alipogusa mlango akakuta haujafungwa akaingia ingawa sio kawaida kuacha mlango wazi...

Kumbe vile tumuachaga anacheki movie au kucheza game si tunaondoka alikagua kagua had akapata funguo ya ziada ya kwenye geti na mlangon akawa nazo....ile mida anajuaga hatupo home anakujaga kupiga search anatupiga na majiran hawamtilii wasiwasi kwa sababu wanamuona mara kwa mara anakujaga wakati sisi tupo ...

Tulikujaga kujua baada ya siku kutumia funguo kuingia ndan bila kujua ndan kuna mtu aliamua kubaki siku hyo...tulimkazia tukachukua funguo zetu na ushikaj wenyewe ukafa hatukutaka hata habar za kudaiana ...ni type za wale washikaj wana kichizi huwez mdhania kama ana harakat hzo za udokoz..
 
Thread yako nzuri ila kuna sehemu zimepwaya ujamlizia alivyooingia wakat ww upo ilikuwaje?
 
Mi nilimchana kimtindo but still ni mshikaji ila sio kiviile,
Ye alitufanyia umafia wa kuiba simu ambayo hata haikuwa yetu, kuna dogo alitupa tumsaidie ku-install application, simu haikurudi japo tulifight sana...
 
Thread yako nzuri ila kuna sehemu zimepwaya ujamlizia alivyooingia wakat ww upo ilikuwaje?
...alivyoingia nilidhani jamaa ninayekaa naye ndio amempa funguo akajipigisha story akasepa sasa aliporud mshikaj kumuuliza akakanusha ndio tukajua jamaa ana funguo ya ziada ndio tukamfuata akajitetea tetea ila tukachukua tu funguo zetu then ikaisha hivyo
 
Back
Top Bottom