kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,819
Inawezekana hili jina ni geni miongoni mwa wengi, lakini naweza kumuita mkombozi wa mikoa iliyopo nyanda za juu kusini hasa wilaya za Namtumbo, Tunduru, Nanyumbu na Masasi.. amewahi kusoma na kuishi nchini Ujerumani kwa muda mwa miaka takribani 38 akifundisha vyuo mbalimbali baadae kwa mapenzi ya Watanzania wenzake hasa wanakusini akaamua kuacha raha na heshima aliyopewa majuu na kurudi kwenye ardhi ya vumbi, jua na mateso.
Aliporudi Tanzania akafikia eneo moja linaitwa Matemanga, lipo wilaya ya Tunduru,mkoani Ruvuma. Katika kijiji kinachojulikana kwa jina la Milonde hapo ndo akaamua kufanya mahali pa historia kubwa kusini mwa Tanzania.
Katika kijiji cha Milonde akaamua kutengeneza kituo chake na kukiita KIUMMA yaani Kituo cha Ufundi na Maendeleo Matemanga, na baadae kidogo ikabadilika na kuitwa KIUMA yaani Kituo cha Ufundi na Maendeleo. KIUMA ikaanza na chuo cha ufundi ambacho kilibeba fani za uwashi, useremala, ushonaji na uchomeaji vyuma kipindi hicho ada ilikuwa Tsh.50,000 tu na ukimaliza unaondoka na seti nzima ya vifaa vya ufundi kwa fani uliyosemea bure kabisa.
Kutokana na mwamko mdogo wa elimu kwenye eneo hilo la nyanda za juu kusini kukawa bado vijana hawana spidi kubwa ya kuchangamkia fursa hiyo, ndipo jamaa alipoonesha upendo wa ajabu sana, alikuwa anawafuata vijana majumbani na kuwahamasisha waende wakasome tena ukikubali unafuatwa gari na hata kama hiyo elfu 50 hauna bado haikuwa kesi, unaruhusiwa kusoma.
Mwamba huyo wa nyanda za juu kusini akaona ufundi haitoshi akaamua kuanzisha shule ya sekondari, ikaitwa Kiuma secondary school-BONITA, kama kawaida ada ilikuwa Tsh.50,000 na kubembelezwa kwenda kusoma, uwe na hiyo hela au usiwe nayo unasoma tu.
Miaka kadhaa mbele akaongeza chuo cha uuguzi kwa ngazi ya Astashahada, akaongeza chuo cha ualimu kwa ngazi ya Stashahada na miaka michache anaweka Stashahada ya Uafisa Tabibu.
KIUMA sas hivi ukienda inavutia, kama umewahi kufika Kibaha Education Centre (KEC) basi hakuna tofauti sana na KIUMA utofauti ni kuwa KIUMA inamilikiwa na mtu binafsi na KEC inamilikiwa na serikali.
Dr.Matomora ametokea kt familia maskini sana, ninaposema sana naomba uelewe sana tena sana huko kijijini Kalulu kata ya Kalulu, tarafa ya Matemanga, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Huyo ndo Dr.Matomora na mchango wake kwa wananyanda za juu kusini na Tanzania kiujumla
Kwa mwenye kuongeza chochote juu ya huyu mwamba karibu..
UKIPATA NAFASI YA KUTEMBELEA RUVUMA PITIA KIUMA, UTASTAAJABU.