CYBERTEQ
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 7,341
- 4,074
Ni takribani mwezi mmoja umepita nilikuja JF kuomba msaada baada ya kuibiwa simu yangu pale Darajani kuelekea mataa ya Changombe. Kwa bahati nzuri nimeipata jana baada ya mtu kuipeleka I-store Mlimani city apate msaada ya kuifungua (Istore n dealers wa Apple product Authorised agents), wahudumu walipoiunganisha na computer zao wakakuta iko locked na ujumbe wangu kwamba simu ile ilikua imeibiwa, atakaeipata anipigie simu kwa number nilizokuwa nimeweka pale, wakanipigia simu wakanieza stori nzima waiomba niende na ID card. Alikua kijana mdogo (sitoweka number yake hapa wala jina lake but kwa maelezo ya wahudumu pale istore, simu hiyo alipewa na kaka yake. Asanteni kwa wale mlionipa moyo kuwa itapatikana na wale waliokuwa wanaitafuta kimya kimya. Kwa ambao walikua hawajaona, hii link ndio niliotoa siku nimeibiwa. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/608175-zawadi-nono-iphone-5-a.html
Safi sana mkuu, wengi huwa wanapuuzia kuwasha ile option ya "find my iphone". Apple wako strict sana kwenye product zao mpaka wanaboa, kuna simu nilisahau password mpaka leo ni useless, na juhudi za kuwasiliana nao wareset zinagonga mwamba wakati vielelezo vyote vya umiliki vipo!! Halafu iStore sidhani kama ni "authorized" dealer wa apple, ni reseller tu wananunua na kuuza.