FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,422
Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 19:18Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
Mithali 22:15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Wakolosai 3:21Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
1 Timotheo 3:4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
Hayo mambo yenu ya kukanya watoto utafikiri unalea nao utaambulia vibaka na wavuta bangi, Mtoto ukimwazibu kwa kosa alilofanya shida iko wapi, Tatizo lenu mnaweka wazazi wanaotiisha watoto wao kwenye kundi moja na child abusers! Huwezi kumchoma moto mwanao hata iwe kwa kosa gani, huwezi kumtia pilipili machoni kwa kisingizio cha kumadabisha huko ni kum-abuse
Kawaida sana kwa mama na mtoto! They always see their mothers not that intimidatingMtoto akikosea na nikiudhika sana ninamchapa. Ila huwa nashangaa baba yao hawachapi hata siku moja lakini wanamtii yeye kuliko mie mchapaji! Mie naweza kukataza jambo kwa kusema na kurudia lakini baba yao akiwaangalia tu kwa jicho la kukataza unaona mara moja wameacha. Duh! Itabidi na mie niache kuchapa.
kwa kuitumia cartoon kama punishment then unaipa sifa ya kuwa ni kitu cha thamani!matokeo yake unaweza kujikuta anakua akiamini hivo!Kwanza nikifikilia tu Kitendo cha kumchapa mwili wangu unaogopa..
1.Pale napoona amekosea nitamwita muda huo na kumwambia kosa lake na kumwambia asirudie
Na atajua kabisa mama amechukia leo
2.Kama alivyosema Superman watoto wanavyopenda cartoon sitamruhusu kuangalia na atajua kabisa hapa leo hali si shwari .
Nk Nk
Malezi yanaweza kuwa bora kwa kumchapa mtoto au kutomchapa...
inategemea sana....
wapo waliochapwa ikawasaidia
na wapo waliochapwa ikawaa athiri...
so sio jibu moja tu simple ....
it works for some,it doesn't for some..
Tatizo utajuaje adhabu ya kuchapa au kutokuchapa now, kama itamsaidia mwanao in the future?
Mtoto akikosea na nikiudhika sana ninamchapa. Ila huwa nashangaa baba yao hawachapi hata siku moja lakini wanamtii yeye kuliko mie mchapaji! Mie naweza kukataza jambo kwa kusema na kurudia lakini baba yao akiwaangalia tu kwa jicho la kukataza unaona mara moja wameacha. Duh! Itabidi na mie niache kuchapa.
Asante..... Umemaliza kila kitu.Mithali 13:24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 19:18Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.
Mithali 22:15Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Mithali 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Wakolosai 3:21Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
1 Timotheo 3:4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
Hayo mambo yenu ya kukanya watoto utafikiri unalea nao utaambulia vibaka na wavuta bangi, Mtoto ukimwazibu kwa kosa alilofanya shida iko wapi, Tatizo lenu mnaweka wazazi wanaotiisha watoto wao kwenye kundi moja na child abusers! Huwezi kumchoma moto mwanao hata iwe kwa kosa gani, huwezi kumtia pilipili machoni kwa kisingizio cha kumadabisha huko ni kum-abuse
Kawaida sana kwa mama na mtoto! They always see their mothers not that intimidating
Mimi nilivyokuwa mdogo nilikuwa mdokozi wa hela na kuku wa watu mtaani. Yaani kuku akipita tu nimepiga tukio! Ukiacha hela tu,kwenye maandazi na vim.bama. Maza akaninivalia njuga nilianza kulambwa stick mpaka nilinyooka na shule nikawa muhudhuriaji mzuri. Namshukuru kwa kuninyoosha ila huwa namlaumu kwa kuniachia makovu mengi miguuni. Mtoto anatakiwa achapwa kwa matukio ya kujirudia rudia lakini isiwe ni schedule.
wakati nasoma primary rafiki zangu walikuwa watoto wa matajiri (kule kwetu enzi hizo ilikuwa mtu akiwa na kaduka nyumbani kwake ni tajiri, lol!). wale watoto walikuwa mabinti tu wawili. walikuwa wakikosa wanapewa adhabu ya kuuza duka....... hiyo siku muuza duka ataambiwa asije anauza binti....... sasa huko ni bonus za pipi na biscuti, hii nayo ni adhabu?kwa kuitumia cartoon kama punishment then unaipa sifa ya kuwa ni kitu cha thamani!matokeo yake unaweza kujikuta anakua akiamini hivo!
unakumbuka wakati tunasoma boarding tulikuwa tunapewa adhabu ya kulima mashamba!matokeo yake mi ukinitajia tu shamba najionea adhabu!hiyo ndo theory ya punishment na reinforcement inavofanya kazi!