Umeunguza mboga badala ya kuzima moto unapuliza perfume kuzuia harufu isisambae

Umeunguza mboga badala ya kuzima moto unapuliza perfume kuzuia harufu isisambae

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
3,146
Reaction score
6,008
Kwa sisi wakatoliki, Unapoenda kutubu dhambi, Jambo Moja la msingi, Lazima ukiri na utamke kwa kinywa chako kwamba aidha ulizini, Uliiba, Ulisema uongo nk. Kabla ya kwenda kukiri lazima uwe umejutia na udhamirie kuziacha, na kama kutakuwa na malipizi itakupasa kukamilisha kwa ajili ya ondoleo kamili la dhambi.

Wanachojaribu kufanya serikali iliyojitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika siku ya DAMU tarehe 29 oktoba ni kuficha chanzo halisi cha maandamano na kuzunguka mbuyu kuukwepa ukweli. Hakuna msamaha wa kweli au maridhiano pasipo na 'Kukiri' wazi kwamba dhambi hiyo ya kumwaga damu za wale waliokuwa wakidai uchaguzi wa huru na haki, Na kwamba hawakuwa tayari kukubali reforms zilizoombwa na wengi waliouawa kabla hata ya uchaguzi ila walipuuzwa, Na hatimaye wakauawa kikatili.

TAFAKARI, CHUKUA HATUA.

#D9
 
Ninaweza kuwa mkatoliki lakini itakapofika kwenda kukiri mazambi yangu mbele ya mwanafamu mwenzangu ndipo nitakapokuwa nashindwa kucomply na ukatoliki
 
Back
Top Bottom