SoC01 Umeumbwa kushangaza dunia

Stories of Change - 2021 Competition

Mfuta_machozi

Member
Aug 5, 2021
16
21
Watu wengi hawaamini kuwa wameumbwa kushangaza dunia. wengi hawajui kuwa ndani yao wamebeba kitu cha thamani kinachoweza kushangaza dunia. Kama nikishikilia mbegu ya chungwa mkononi mwangu na kukuuliza "unaona nini?".bila shaka utasema "naona mbegu ya chungwa".ndio ni kweli lakini kiuhalisia huo sio ukweli uliokamilika ,ukweli uliokamilika ni kwamba nimeshika mbegu ya chungwa ,mkononi mwangu nina mti wa machungwa uzaao machungwa yenye mbegu za machungwa ndani yake,nina shamba la machungwa mkononi mwangu,msitu wa miti ya machungwa. Inashangaza sana! Mungu ameficha hatima kubwa ndani ya kila kitu alichokiumba duniani.angalia kifaranga,ndani ya kifaranga kuna kuku wengi mno.

Unaona mtoto mdogo wa kiume ndani yake kuna mwanaume mwenye mbegu ambazo wengi wetu huziita "mbegu za kiume" mbegu hizo humfanya mwanaume lijari kuwa baba vivyo hivyo kwa mtoto mdogo wa kike ndani yake kuna mwanamke mrembo wa kuvutia aliyebeba umama ndani yake.mwanamke na mwanaume wakiungana hutengeneza familia,ukoo,uzao kizazi na kizazi.mpendwa wewe ni kama mbegu ya mchungwa umeumbwa kushangaza dunia.jinsi mwanadamu anavyokutazama ni tofauti kabisa na Mungu akutazamavyo mwanadamu anaweza kukuona upoupo tu hujielewi, huna lolote la maana lakini Mungu anaona kitu kikubwa ndani yako kinachoweza shangaza dunia.

Ruhusu zawadi uliyonayo ishangaze dunia.
Ndege hajawai tamani kuruka angani,kuruka angani ni kitu kilichoko ndani yake,ndege anapenda kuruka angani,anafurahia kuruka angani watu wanafurahia kuona ndege akiruka angani.maua yameumbwa kuchanua na kushamili,yanafurahia kuchanua na kushamiri, nyota zimeumbwa kuwaka na kumelemeta usiku sijawahi ona nyota zinawaka mchana,vivyo hivyo kwa samaki wa baharini, samaki hajawai tamani kuogelea samaki wameumbwa kuogelea ,kujua kuogelea ni kitu kilichoko ndani yake.

samaki anafurahia kuogelea, sababu ameumbwa kuogelea. watu wanafurahia kuona samaki akiogelea wengine hutoa pesa zao kwenda kuangalia samaki anavyoogelea.Ukimchukua samaki ukamweka nchi kavu ili ajifunze kuruka angani kama ndege hatostahimili atakufa. ni sawa na ndege umlazimishe aingie baharini ajifunze kuogelea hatoweza kuogelea atakufa.chochote unachokiona duniani kina kusudi.

Hata wewe ulipoumbwa uliwekewa kusudi ndani yako.hukuja duniani kwa bahati mbaya upo hapa duniani ili utimize kusudi la Mungu .Kila mtu ana kusudi lake alilowekewa kulitimiza duniani.usimdharau mtu yoyote hujui kusudi alilowekewa na Mungu ndani yake.Utafanikiwa kutimiza kusudi endapo tu utatambua zawadi ya kipekee iliyoko ndani yako. Sote tumepewa zawadi na Mungu ili kusudi la Mungu litimizwe.unaweza jiuliza nimepewa zawadi gani na Mungu?.

Kujua zawadi ulizopewa na Mungu ni rahisi sana embu kwa dakika chache fikiria, ni kitu gani ukikifanya kinakupa raha,unafurahia na kuburudika sana ukikifanya,kitu gani kinaleta hamasa na kinachochea moto ndani ya mishipa ya damu yako,kitu gani unaweza ukakifanya masaa 24/7 bila kulipwa au hata mwaka mzima bila malipo yoyote na bado usiache kukifanya,yani kinaweza kufanya usilale ukae macho usiku kucha usahau hata Kula, je kitu hiko kinaweza saidia jamii?

Kama jibu ni ndio hiyo ndio talanta au zawadi uliyopewa na Mungu. Ruhusu zawadi hiyo uliyopewa ishangaze dunia.

Raha katika kujua kusudi lako duniani.

Asikwambie mtu kuna raha ya kipekee sana katika kujua kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.ukiona mtu hafurahii anachokifanya duniani jua bado hajatambua kusudi.Mtu anayejua kusudi lake ana raha sana.unaweza kuta mwalimu anafundisha hachoki kufundisha,anatamani wanafunzi wamtafutie muda wa ziada ili aendelee kufundisha. akianza kufundisha wanafunzi hawaboreki huwezi ona mwanafunzi anasinzia darasani na wanafunzi hao wanapata matokeo mazuri sana ,unashangaa inakuwaje ndivyo alivyoumbwa hilo ndio kusudi la yeye kuwepo duniani. unapoishi katika kusudi lako unakuwa na raha sana.kwanza,kwasababu unapenda kile unachokifanya maisha yako yanakuwa na furaha yani huchukii jumatatu unafurahia jumatatu , pili kwasababu unapenda unachofanya watu wanavutiwa na unachokifanya na wanazidi kukupenda wewe zaidi, tatu kwasababu watu wanavutiwa na unachokifanya basi wanaweza kukutunza pesa na kukufanya utajirike

Fikiria ni raha iliyoje yani unalipwa pesa kwa kile unachopenda kukifanya na kinachokupa furaha kwenye moyo wako.mwangalie msanii wa muziki maarufu Diamond Platnumz yeye anapenda kuimba,muziki ni sehemu ya maisha yake nimesema sehemu hapana muziki ni maisha yake, anafurahia kuimba watu wanapenda na kufurahia muziki wake mimi pia napenda muziki wake watu wanamlipa diamond pesa Ili wapate kuburudika na muziki mzuri.

Diamond Platnumz amewekwa duniani kututumbuiza na kutuburudisha Diamoond Platnumz anaishi katika kusudi lake. watu wengi kama Oprah Winfrey,Millard Ayo,Ellen DeGeneres,Gayle King,Nandy,Alikiba,Samatha,Salama Jabir,Mc Pililipili,Flaviana Matata,Elizabeth Michael na wengine wengi maarufu unaowajua walijua kusudi lao mapema wakaishi na kutumikia kusudi sasa wanafurahia kuishi maisha wanayoishi. hata wewe mpendwa bado hujachelewa.ishi katika kusudi lako ili uweze kushangaza dunia

Wazo ulilo nalo likashangaze dunia
Anza na hilo wazo liloko akilini mwako.kama wazo ulilo nalo ni zuri linaweza saidia jamii inayokuzunguka na kushangaza dunia usiogope kuthubutu anza!. usifikirie watu watakavyosema usikatishwe tamaa na watu ambao hawajui maono uliyopewa na Mungu ushangaze dunia.angalia vizuri mazingira yanayokuzunguka umeona nguo uliyovaa, viatu,mswaki,kitanda,kabati runinga,redio,mwiko vyote vinavyokuzunguka ni mawazo ya watu.

Mtu aliona vyakula vinachacha na kuharibika akajiuliza hivi siwezi nikatengeneza kifaa kikachoweza kugandisha vyakula visichache? friji likatengenezwa leo hii mabilioni ya watu wanatumia friji kuhifadhi vyakula.Taulo za kike zinazowasitiri wanawake na kuwafanya wajisikie huru wakiwa kwenye siku zao za hedhi ni wazo la mtu, umeona biashara inayovutia wateja wengi mtaani kwako ni wazo la mtu,utaongea nini kuhusu mabasi ya mwendokasi angalia tena kwa makini vyote vinavyokuzunguka utagundua ni mawazo ya watu.chochote unachokiona duniani ni wazo la mtu. nilitaka kusahau simujanja (smartphone) nayotumia kuandika nakala hi kwa raha mustarahe bila kuumiza vidole vyangu ni wazo la mtu. Fikiria mwanzilishi wa jarida la jamii ( jamii forums). jarida linalo elimisha,burudisha na kujenga jamii ni wazo la mtu. binafsi kupitia jarida hili nimejifunza vitu vingi ambavyo awali nilikuwa sijui.huenda kuna mtu kimoyomoyo anasema nilivyo mvivu napenda kulala sidhani Kama naweza buni kitu chochote cha maana.

Nikwambie watu wenye hulka ya uvivu wanasifika kuwa wabunifu wazuri sana .sina maana uendekeze uvivu hapana ila nachotaka ujue hata wewe una nafasi ya kushangaza dunia ni vile tu hujaamua. Billgate bilionea maarufu duniani anakwambia "anapenda kuajiri watu wavivu anachojua wavivu wanajua kurahisisha jambo".ukiangalia ni kweli mvivu anaweza kukwambia "yani natamani nioge nimelala","kupanda hizi ngazi tatu Kila siku inachosha natamani kungekuwa na ngazi za umeme","natamani hizi nguo zijifue, zijianike ikiwezekana zijinyoshe na zijiweke zenyewe kabatini"mvivu anawaza jinsi ya kurahisisha mambo mawazo ya mtu mvivu yameweza kuvumbua vingi vya kushangaza.

Leo hi tuna majokofu (mabafu ya kulala), tuna ngazi za umeme (lift),tuna machine za kufulia ( washing machine), roboti na vingine vingi vya kushanganza. Mpendwa tunasubiri wazo lako lishangaze dunia.

Jitahidi usiondoke duniani kabla hujashangaza dunia.
Wanasema utajiri na urithi wa mali nyingi sana upo makaburini.ni huko kuna nyimbo Kali Sana zenye midundo mzuri ambao hatujawahi sikia,Kuna mashahiri mazuri,maandishi mazuri hatujawai soma,kuna vichekesho vya kukuchekesha mpaka mbavu zikauma hatujawahi sikia, Kuna viongozi wazuri wenye hekima na busara hatujawahi kuongozwa nao,kuna mawazo mazuri sana ya biashara na ubunifu mwingi hatujawahi ona hazina nyingi zimejificha makaburini. kwasababu ya watu kuogopa kuonyesha mawazo waliyonayo na zawadi zao walizopewa na Mungu.

Jitahidi usiondoke kabla hujashangaza dunia. tunatamani kuona zawadi uliyopewa na Mungu ili utushangaze usiogope hujachelewa bado una nafasi usisite,amini mawazo yaliyoko ndani yako unaweza shangaza dunia.hakuna mtu anayeweza kutuonyesha mambo mazuri hatujawahi ona duniani zaidi yako.unaondoka vipi bila kutuonyesha ulichopewa na Mungu? usikubali kuondoka kabla hujashangaza dunia.

Kuwa makini na watu wanaokuzuia kushangaza dunia.

Mpenzi,ndugu, jamaa,marafiki na watu wako wa karibu wanaweza kuwa daraja la kukufanya wewe ushangaze dunia au ukuta wa kukuzuia wewe kushangaza dunia. nachokijua tabia ya mtu huwa haijifichi. Mwalimu wangu wa hesabu alikuwa anapenda kusema "ogopa mtu mwenye mamlaka", siku zote nilikuwa nachukulia huo usemi wake Kama masihara mpaka yaliponikuta yakunikuta na huyo mwalimu. unashauku ya kujua kilinikuta nini na mwalimu wangu wa hesabu? ,usijali nitakuhadithia mwisho wa nakala hii.

Nachotaka ufahamu ni kuwa watu wakikuonyesha tabia zao waamini papo hapo bila kupepesa macho nakwambia utakuja nishukuru baadae, hakuna mtu anayejijua zaidi ya yeye ajijuavyo mwenyewe unakuta wenyewe bila kulazimishwa wanakwambia maneno kama haya; "oya mwananangu Mimi ni mnafiki balaah ","wasela mimi ndo kibenteni mwenyewe hapa mtaani natoka na wake za watu mjue","shoga yangu mimi nimekuja chuo kula Bata,"wahuni msinione hivi mimi mkorofi vibaya mno alafu sinaga huruma na wanawake","Mimi mchoyo","Mimi na wivu","huwezi amini shoga nimemwekea limbwata mume wa fulani hapa kwangu ndo kafika" na maneno mengi zaidi ya hayo.

Wenyewe hawana shida yoyote kwasababu wanazijiua vizuri tabia zao. chochote kitokacho ndani ya kinywa cha mtu ndicho kilichojaa ndani ya moyo wake. rafiki yako anayetukana sana jua moyoni mwake amejaza kamusi ya matusi, rafiki yako anayeongea hekima amini moyoni mwake Kuna hekima nyingi sana.kitokacho ndani ya kinywa cha mtu ndicho kilichojaa kwenye moyo wake.wewe ndiyo mwenye tatizo. Tatizo lako wakikwambia hivyo na kukuonyesha tabia nyingi zaidi ya hizo unaona kama wanatania vile yani huamini kabisa.

Hapo ndipo unapokosea kujifanya unajua watu sana zaidi ya vile wanavyojijua wao.utakuta wewe mwenyewe unawaambia "acha utani bwana","embu acha zako izo asiyekujua nani","unajua mkuu una masihara Sana huku unacheka ","yani unamatani ya ngumi kabisa","shoga una vituko balaah". Mpendwa unapochukua muda mrefu kuamini tabia zao kuna siku watakuvunja moyo utabaki kushangaa na kusema" kwanini lakini umenifanyia hivyo rafiki yangu","wewe si jamaa yangu kabisa","wewe sio wa kunifanyia hivi".labda hujui rafiki anayesema watu vibaya wakiwa hawapo ni vile amekosa nafasi ila akipata mwanya kidogo na wewe hashindwi kukuzungumzia vibaya kwa watu nyuma ya mgongo wako, tahmini kwa uangalifu tabia za hao watu ambao wewe unawaita marafiki wachunguze vizuri kwa makini.

Angalia unaotakiwa kukomaa nao,unaotakiwa kuwachuja ,kuwapunguza na kuwaondoa kabisa kwenye safari ya maisha yako.Rafiki mzuri ni yule anayependa mafanikio yako hachukii kufanikiwa kwako,rafiki mzuri hakukatii tamaa,anakutia moyo ukichoka,haogopi kuwambia ukweli ata uwe mchungu kiasi gani, rafiki mzuri ni yule anayekupa ushauri na mawazo mazuri.

Chagua rafiki sahihi, usikubali kukosea kufanya maamuzi katika kuchagua mwenza wa maisha. kumbuka ni mwenza wa maisha unayechagua bora ukosee kuchagua mchepuo wa masomo ukiwa shule unaweza badilisha fani ukifika chuokikuu au bora ukosee kuchagua kazi unaweza ukafungua kampuni yako na kujiari kuliko kukosea kuchagua mke au mume.hakikisha watu unaowachagua wanakusaidia kung'ara na kushangaza dunia. Tai hana urafiki na kuku hutokaa kumwona tai anaomba ushauri kwa kuku. maono ya tai ni makubwa kuliko ya kuku.wewe pia tambua watu wenye maono sawa na wewe, ambatana nao ili uweze shangaza dunia.

Kuwa wewe Ili ushangaze dunia.
Nyota zipo nyingi sana angani zaidi ya bilioni ziko nyingi mno zote zinawaka,zinang'ara na kumelemeta. Kila nyota inatoa mng'ao wake. nyota fulani inavyowaka ni tofauti na nyota nyingine inavyowaka. Mara nyingi napenda kushangaa nyota angani zinavutia kutazama.

Huwa naamini Kila mtu ni kama nyota angani sote tumeumbwa kung'ara na kushangaza dunia. Kama vile kila nyota inatoa mng'ao wake na sisi pia kila mtu anamng'ao wake wa kuvutia na kushangaza.cha kusikitisha tamaduni zetu hazituonyeshi hili, tamaduni zetu zinakwambia "unaona nyota fulani inavyowaka na wewe unatakiwa uwake vilevile umesikia" ,tamaduni zetu hazitaki tuonyeshe ming'ao iliyoko ndani yetu, tamaduni zetu zinataka tuigilizie nyota fulani vile inavyowaka.Ni huzuni kwakweli,mpendwa usikubali kuwaka kama fulani amini ndani yako una mng'ao wako wa kushangaza dunia.kuwa wewe ili uweze shangaza dunia kwa namna yako.

Usiruhusu dunia ishushe thamani yako.
Mpendwa natamani ujue kuwa wewe ni wa thamani sana ndio sana zaidi ya vile unavyofikiria mimi naamini katika uzuri ulioko ndani yako nimetoa moyo wangu wote,nguvu zangu zote nikaacha vyote nivifanyavyo kuandika nakala hii kwa ajili yako ni kwasababu nakupenda na naamini thamani na uzuri ulionao.

Natamani ningekuwa karibu yako kwa moyo mkunjufu uliojaa furaha na tabasamu nikwambie "WEWE NI WA THAMANI SANA!!!".thamani uliyonayo ni zaidi ya mamilioni ya pesa. mpendwa unastahili kutunzwa,kupendwa,kuthaminiwa,kuheshimiwa chochote kilicho bora unastahili kukipata.hutakiwi kuchukuliwa poa,usimruhusu mtu yoyote akudharau, kwanza anakudharau yeye kama nani?.

Nachokijua unaposhusha thamani yako dunia inashusha thamani yako zaidi. Dunia haijawahi kuwa na huruma kujiimbia Bahati Bukuku "dunia haina huruma jamani nasema".yani kutegemea dunia ikutendee mema kwasababu wewe ni mtu mwema ni sawa na kutegemea kuokota embe chini ya mnazi haiwezekani kabisa dunia kukuonea huruma. dunia lazima ikuchokoze, utakaa zako umetulia huna neno na mtu, dunia hiyo itakuja ikukorofishe,ikuyumbishe,ikuchanganye ikupatie changamoto na majaribu ili utikisike kidogo.

Kamwe usiipatie nafasi dunia ishushe thamani yako.mtu anayeuza almasi hawezi shusha bei ya almasi eti kwasababu hana soko. Thamani ya almasi iko palepale iwe na soko isiwe na soko almasi itabaki kuwa na thamani yake. wewe pia changamoto uzipitiazo kwenye maisha yako zisikufanye ushushe thamani yako kumbuka umeumbwa ushangaze dunia.

Hauwezi shangaza dunia mpaka utakapoamua kujikubali,kujithamini na kujipenda.

wewe ni wa pekee umeumbwa kwa namna ya pekee, umezaliwa na vina saba vya kipekee(DNA) ambavyo vinakutofautisha wewe na mtu mwingine ndani yako una talanta,zawadi,uwezo na ujuzi wa kipekee tofauti na mtu yoyote hapa duniani, hakuna anayefanana na wewe,majani mawili hayafanani, hata mapacha tunaodhani wanafanana hawako sawa angalia alama za vidole (fingerprints) ni tofauti na mtu yoyote hapa duniani.

Wewe ni wa pekee.acha kujilinganisha acha kujinyima furaha kwa kufurahisha watu wengine. usifikirie wanadamu watanionaje, waache wakufikirie watakavyo haikuhusu na wala haikubadilishi wewe utabaki kuwa wewe, hauwezi shangaza dunia mpaka pale utakapojikubali na kujipenda. unaweza kusema wewe hujui tu mapito yangu,hujui stori ya maisha yangu ndio sijui chochote kuhusu mapito yako lakini kama historia ya maisha yako inakuzuia kung'ara na kushangaza dunia basi sihitaji hata kuisikiliza.sisi sote tuna mapito, kuna watu wana mapito magumu zaidi yako,wengi wamenyanyaswa wametendewa ukatili na wazazi wa kambo,wengine na wazazi wa kuwazaa kabisa,wengi wametelekezwa na kukataliwa na kupitia magumu mengi zaidi. lakini katika yote waliyoyapitia haikuwazuia wao kutokung'ara na kushangaza dunia .mimi na wewe ni nani tushindwe kung'ara?.

usisite anza Sasa kujikubali kumbatia mapito yako yamekufanya uwe hodari, makosa uliyowahi kuyafanya nyuma pengine sekunde chache zilizopita ni kwasababu ya wewe ujifunze, wanasema tunajifunza kupitia makosa. jithamini ,anza kujipenda, kula vizuri,vaa vizuri pendeza,nukia vizuri,kuna sehemu nzuri unatamani kwenda kutalii nenda katalii, furahia maisha cheka mpaka mbavu ziume, chochote kinachokupa raha fanya ilimradi hakivunji sheria ya nchi wala hakiathiri amani ya wengine.kuna uhuru mkubwa katika kuwa wewe, anza kuwa wewe jipende mpaka watu wavutiwe na wewe. ngoja nikuibie siri unajua unapojipenda sana moyo wako unaujaza upendo yani moyo unafurika upendo mpaka unamwagika.watu wanavutiwa na wewe kwasababu ya upendo uliofurika ndani ya moyo wako. chochote kinachotoka ndani ya moyo wako iwe ni salamu,tabasamu,mazungumzo,matani na chochote kile kinaambatana na upendo.wewe ni shahidi Kuna baadhi ya watu unatamani wawe rafiki zako wa karibu au unajikuta unawapenda tu bila sababu, ukiwaona tu kimoyo kinarukaruka unapata hamasa, ni kwasababu wanasambaza upendo uliofurika ndani yao huwezi kumpenda jirani yako Kama hupendi nafsi yako.anza kujipenda mpendwa, mara nyingi tunavutiwa na watu wengi maarafu na kukubali kuwa wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii kwasababu tunafurahia jinsi wanavojipenda na kujikubali, hata wewe unaweza vutia na kushangaza dunia kwa namna yako.mimi na wengine wengi tukawa wafuasi wako.

Ahadi niliyokuhaidi.
Nilikuahidi ntakuhadithia kilichonikuta mimi na mwalimu wangu wa hesabu ,haya ngoja nikuhadithie kiufupi; nikiwa mwanafunzi wa chuokikuu wakati wa kipindi cha likizo usiku moja nikiwa nimelala nilipigiwa simu alikuwa ni mwalimu wangu wa hesabu nilipopokea akaniambia "Nina idadi ya watu nane(8) ambao zimepelea maksi chache wasipate (sup) na wewe ni miongoni mwao tunafanyaje?" kwa haraka unaweza usielewe neno "tunafanyaje" linamaanisha nini kwa sauti ya chini nikamwomba mwalimu "tafadhari niondolee sup" akaniuliza "uko wapi?","tunaweza kukutana" kiutu uzima unaweza elewa mazungumzo haya yalikuwa yanaelekea wapi.usiku mzima nililala natafakari hivi kweli mimi nihatarishe afya yangu,ndoto zangu,usichana wangu ili tu niwekee matokeo mazuri ambayo hata sistahili. n

Nakumbuka asubuhi azana juu ya alama nilimtumia mwalimu ujumbe mfupi kumwambia "mwalimu Mimi tangu naanza chekechea mpaka nimefika chuo sijawahi kuwa mzuri kwenye hesabu ,sikumbuki kama nilishawahi pata A ya hesabu,sijui hesabu, siwezi hesabu chochote nilichokipata ninastahili nimejiandaa kufanya mtihani wa (SUP)".

Tangu siku ile sijawahi jutia maamuzi niliyoyafanya. sikutaka napotafakari historia ya maisha yangu hichi kipengele kiwepo "nililala na mwalimu kuwekewa alama A ya hesabu".natambua akili yangu inaweza masomo yapi siwezi kuwa mzuri kwenye masomo yote kuna masomo nayoyaweza na ambayo siyawezi , najijua mimi ni nani , natambua thamani iliyoko ndani yangu. labda nizikwe lakini ningali hai siwezi ruhusu kitu chochote, mtu yoyote anivunjie heshima.

Ombi langu kwako.
Mpendwa unaweza sahau yote niliyoyaandika kwenye nakala hii lakini nakuomba usisahau thamani yako.

wewe ni wa thamani Sana!!!
Ninaimani na thamani iliyoko ndani yako.

umeumbwa kushangaza dunia.Anza Sasa kushangaza dunia!!.
 
MUNGU AKUBARIKI ULIYE ANDIKA MAKALA HII
 
Aisee sijawahi Soma uzi mzuri kama huu, na wewe kwa nafasi yako, endelea kushangaza dunia kwa uzi wako
 
Ulipokubali sup ni ujasiri mkubwa sanaaaaa
 
sikutanii km hujaolewa wasiliana na mimi!! nikuunganishe na kaka yangu!!....... basi km umeolewa uwe rafiki yangu bure tu!
 
Back
Top Bottom