Umetoka zako Ughaibuni kuja kula Krismasi... Halafu!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,809
15,417
upload_2016-12-27_11-50-24.png
 
Kuna jamaa yalimkuta, amefika air port kwanza mwenyeji hakwenda kumpokea, aliamua kutafuta hoteli na familia wakati aliahidiwa akishuka anafikia kwake fresh. Kuanza kutafuta ndugu ndiyo anaonyeshwa kiwanja jamaa alichonunua, matofali hayazidi 100.
 
Hahaha lazima uzimie kwasababu ukikumbuka ulivyobeba box ughaibuni kwa mateso
 
  • Thanks
Reactions: ibn
Kuna jamaa yalimkuta, amefika air port kwanza mwenyeji hakwenda kumpokea, aliamua kutafuta hoteli na familia wakati aliahidiwa akishuka anafikia kwake fresh. Kuanza kutafuta ndugu ndiyo anaonyeshwa kiwanja jamaa alichonunua, matofali hayazidi 100.
Hii iliwahi kunisababisha kufanya maamuzi ya kila nikirudi huku, nasimamia mijengo yangu mwenyewe aiseeee.....
Dunia ya leo, imani imetoweka
 
Hii iliwahi kunisababisha kufanya maamuzi ya kila nikirudi huku, nasimamia mijengo yangu mwenyewe aiseeee.....
Dunia ya leo, imani imetoweka
Ni afadhali udundulize zikiwa nyingi unachukua likizo ya mwaka na ikiwezekana mwezi mwingine bila malipo, miezi miwili unafanya kitu cha kueleweka mpaka pesa ikiisha unaondoka.
 
Hivi ukiingia mkataba na kampuni reliable (in terms of credibility na financial stability), wakawa wanasimamia ujenzi wa nyumba yako na wakawa wanakutumia updates kwa mtazamo wangu inapunguza risk. Kwa sababu hata kama ukikutana na hali hiyo na kampuni ni ya uhakika unaweza kwenda mahakamani; ila kwa ndugu utaishia kujichosha tu hata ukienda mahakamani.

Ukweli ni kuwa utalipia ka gharama kwa kuajiri kampuni ila at least utajiepusha na pressure kama hizi. Option zingine ndio hivyo kudunduliza zikitimia unakuja unapiga msingi kwa mwezi; unaondoka ukirudi unapandisha ukirudi unapiga paa ukirudi unafanya finishing. Sema kuna gharama za nauli pia.
 
Kama una fedha yako ya boksi:

Chukua likizo ya miezi miwili tafuta kiwanja na anza taratibu zote za ujenzi na hakikisha umefikia "lintel".

Baada ya hapo unarudi majuu na baadae tena unachukua likizo ya miezi miwili ya kuja kumalizia kupaua na "finishing" kidogo.

Nyumba unaijenga kwa mtindo wa kuwa na "two in one" kwamba wewe sehemu yako inafungwa mara nyingi, na nje unajenga kajumba kadogo ka kukaa mwangalizi.

Awamu ya tatu unamchukua dogo yoyote kutoka kijijini unakuwa unamlipa mshahara wa kuitunza nyumba na anapata kila kitu.

Au kama wazee wapo unawahamishia humo na unawaongezea au top up kwenye kiinua mgongo chao.

Ikulu yako inakuwa imekamilika kwa kila kitu na unaendeleza libeneke la kubeba boksi na pale penye udhia unakuwa unapenyeza rupia kidogokidogo mpaka hapo utakapoamua kurudi TZ kimoja.

Angalizo:

1.Ukinunua gari nunua lililotumika mpaka pale utakapoamua kurudi TZ kimoja na ndiyo unaweza kuagiza mchuma wa kueleweka.

2. Ukiwa TZ gari unatumia mwenyewe lakini ukiondoka kurudi majuu unatoa "battery" na unaizungushia kitambaa kuificha kwenye "garage".

3. Dogo unamlipa mshahara wa kutunza nyumba na pia kuangalia ustaarabu wa wazee wako.

4. Kila ndugu unaekutana nae unamweleza ukweli wa maisha magumu ya ughaibuni na jinsi unavyopiga boksi ili kieleweke.

5. Huyu dogo ndiye msaidizi wako rasmi hivyo unamwekea utaratibu wa kujindeleza kama udereva au ufundi, hivyo kama gari ni pick-up basi atafanya utaratibu wa kubeba nyanya ila kwa makubaliano maalum.
 
Back
Top Bottom