Umeshiriki lipi kati ya haya?

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2012
Posts
3,598
Reaction score
1,545
Salaam,

Mara kadhaa nimeshiriki/inawezekana nawe pia umeshiriki katika mjumuiko wa watu wenye kueleza/kutoa maoni, majadiliano, elimu n.k lakini hasa inakuwa shida kutambua nini hasa ulichoshiriki(nilichoshiriki), Ningependa kusaidiwa tofauti au matumizi ya maneno haya;

-Kongamano.
-Warsha.
-Mkutano.
-Kikao.
-Semina.
-Mdahalo

Kwa msaada wa kamusi bafo inakuwa ngumu kutofautisha, je, todauti hasa ni ipi?
Nataraji majibu yatakayojenga zaidi kuliko kubomoa.
Shukrani.
 

Ingawa sio mtaalam wa kiswahili nachangia kama ifuatvyo:-

Kongamano=Jumuiko la watu wenye ufahamu wa fani moja katika kubadilishana uzoefu wao.
Warsha/Semina =Jumuiko la watu katika kupata melekezo ya kiutendaji juu ya jambo/kazi fulani
Mkutano=ni kutaniko la watu mbali mbali
Kikao= ni mkutano wa watu wachache miongoni mwa mwengi (wawakilishi)
Mdahalo= mvutano wa pande mbili zenye mitazamo tofauti katika kupata lengo la jumla(pamoja)





 

Mkuu, ahsante sana ...nadhani wewe ni mtaalamu.nimekuelewa vyema na nashukuru kwa ufafanuzi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…