Umeshawahi kuiba???

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,188
3,360
Sidhani kama nitakuwa mwizi peke yangu humu, Nakumbukuka mara ya kwanza kuiba ilikuwa shilingi 10 miaka ya 90s kwenye chenji za mboga, wizi wangu ulifikia stage hadi nikachonga Funguo za vyumba vya nyumbani ili niwe naiba bila presha watu wakiondoka, Pia nakumbuka boarding secondary nliiba elfu 30 na wala sikutishika na biti la kurogwa, kwa ufupi nimewai kuiba ila sio kwa kiwango cha juu sana na hii Tabia nashukuru niliiacha
 
Ndiyo,
Nilipokuwa Form 3 nilikuwa sifui mashati, nilikuwa nasubiria madogo wakishafua naliiba kisha nalihifadhi kesho yake navaa likiwa safi kabisa.

Bahati mbaya siku moja nimeiba shati la dogo, asubuhi nikavaa. Nipo Class mademu wananicheka, duuh kumbe shati lina chawa.

Nilikoma kuiba kuanzia hapo. Sijawahi tena.
 
Wakati niko mdogo uswahilini kwetu kuna mama alikuwa anakaanga viazi na chachandu ya pilipili sasa nilitamani sana na mkwanja sina nikarudi nyumbani nikakuta dada yangu kajiwekea Mia mbili zile za noti nilicho fanya nikapita nayo nikaenda kugonga viazi sasa kumbe aligundua mimi ndio nimechukua akamweleza baba ile narudi nyumbani nikakuta fimbo za mifurusaji zimeandaliwa nilichezea bakora za kutosha toka siku hiyo hadi utuuzima wangu huu naogopa sana kuiba.
 
Ndiyo,
Nilipokuwa Form 3 nilikuwa sifui mashati, nilikuwa nasubiria madogo wakishafua naliiba kisha nalihifadhi kesho yake navaa likiwa safi kabisa.

Bahati mbaya siku moja nimeiba shati la dogo, asubuhi nikavaa. Nipo Class mademu wananicheka, duuh kumbe shati lina chawa.

Nilikoma kuiba kuanzia hapo. Sijawahi tena.
 
Chakula:
Nimedokoa sana mm mboga na mabaki ya ubwabwa. Mpaka sasa nafanya ila nafanya kijanja. Nikiwa ntumbani namwambia mama kua ninachukua mboga basi anajua kua ninachukua.

Hela:
Mara ya kwanza nimechukua sh nikaenda kuitoa sadaka Sunday. Zilizobaki nimechukua 50 nyingi kwa mama ili niende banda la video.

Mtaani:
Huku sasa ndio usiseme. Tulikua na kikundi chetu kabisa tunakiita TMK WAIZI tulikua tunajifunga vitambaa kichwani kabisa vikiwa na jina la kundi letu. Tumeiba mahindi, karanga, mapera, njugu, Maembe, vigazi/chikichi, mashindwi, condom ili tukatengenezee mipira ya kucheza.

Yote hayo nimeyafanya bellow 13yrs. Namshukuru MUNGU sijakwenda nayo hadi ukubwani.
☆☆☆☆mondray
 
Chakula:
Nimedokoa sana mm mboga na mabaki ya ubwabwa. Mpaka sasa nafanya ila nafanya kijanja. Nikiwa ntumbani namwambia mama kua ninachukua mboga basi anajua kua ninachukua.

Hela:
Mara ya kwanza nimechukua sh nikaenda kuitoa sadaka Sunday. Zilizobaki nimechukua 50 nyingi kwa mama ili niende banda la video.

Mtaani:
Huku sasa ndio usiseme. Tulikua na kikundi chetu kabisa tunakiita TMK WAIZI tulikua tunajifunga vitambaa kichwani kabisa vikiwa na jina la kundi letu. Tumeiba mahindi, karanga, mapera, njugu, Maembe, vigazi/chikichi, mashindwi, condom ili tukatengenezee mipira ya kucheza.

Yote hayo nimeyafanya bellow 13yrs. Namshukuru MUNGU sijakwenda nayo hadi ukubwani.
☆☆☆☆mondray
 
Sidhani kama nitakuwa mwizi peke yangu humu, Nakumbukuka mara ya kwanza kuiba ilikuwa shilingi 10 miaka ya 90s kwenye chenji za mboga, wizi wangu ulifikia stage hadi nikachonga Funguo za vyumba vya nyumbani ili niwe naiba bila presha watu wakiondoka, Pia nakumbuka boarding secondary nliiba elfu 30 na wala sikutishika na biti la kurogwa, kwa ufupi nimewai kuiba ila sio kwa kiwango cha juu sana na hii Tabia nashukuru niliiacha
Umenifanya nikakumbuka ule usemi wa wahenga "jasiri haachi asili:
 
Niliiba shillingi elfu moja mwaka 1996 ,mama alikua ameiweka juu ya kabati

Nikaenda kashai bukoba mjini kucheki movies asubuhi asubuhi

Niliangalia filamu kama tatu, nikala bago na vijana wengi yani nilikua don siku hiyo then chock stick nyingi sana

Nikarudi nyumbani na pipi nyingi nikagawa kwa ndugu na wenzangu kibao

Mama akashtuka akajua ni mimi niliyechukua nikapewa kipigo heavy kunisachi nimebakiwa na mia sita sabini na tano

Akaniacha na uvimbe mwili mzima kama wiki hivi na vidonda

Bata nililokula sitakuja kula tena enzi hizo shilling tano inafanya kazi sawa na mia tano this time

R.I.P mukandala rufufu
Movie zile Tatu nazikumbuka mpaka kesho sababu nilienda kashai kufuata jinsi anavyotafsiri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom