Umeshawahi ku-date msichana anayejifanya 'high class'...?

Umeshawahi ku-date msichana anayejifanya 'high class'...?

D 007

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2012
Posts
206
Reaction score
147
Wanaume wenzangu, Umeshawahi kupata Msichana, mnadate lakini yeye ana sheria kama anaishi Europe wakati wazazi wake wanakaa NGALE LO O?? Msichana anaku-ektia maisha hadi wewe Boyfriend wake wakati unamjua fika A-Z kwa kujifanya High Class.

Kila kitu anataka high class,kuanzia nguo,hadi sehemu ya kula,ukitaka kumpeleka kwa khani chips anakwambia mi nimezoea Naura Springs huko ntaumwa tumbo…Tumbo?? Wakati mamako anakula kishori home na ananenepa vizuri tu…Huwezi kuwa serious!

Mathalani, umemnunulia zawadi maskini ya Mungu, umepata vijisenti kidogo ukaamua kum-surprise bebi nini ,umemnunulia Kiatu kizuri… Sikia sheshe lake na maswali yake ya kalunguyeye,"Baby wow,thanks for Shoes,Designer gani???OOh Em G(kwa ile sauti yao ya swagga za kwenye Series za ITV),Chu Tang Huang,oh no please…

I only wear Italian Designers,kama Sio LV basi iwe angalau Prada,Versace,D&G au Givenchy,ukikosa saana,labdaRoberto Cavalli au Jean pauul Galtier…Hivi viatu rudisha tu baba,they are so cheap…Linakushuka Shuu!Maskini,unakuwa umejisapraiz!
 
Kama umempenda msichana wa namna hiyo kwa ajili ya ndoa nakushauri utafute Kanisa la Kiroho lililopo jirani kwa ajili ya kuombewa kutolewa hao pepo wachafu kwanza baada ya hapo ufahamu wake utamrudia na atajitambua na kila kitu kitakuwa safi.
 
mmh,hv kumbe na wa vile wapo!!!! basi mwenzenu huwa napokea tu ht bila kuuliza hbr za designer wala nn.......ninachojua mm ni kupokea,kushukru na kuanza kutumia.
 
Ukikutana na huyo You Ever Forward,,
wanaishiaga kuolewa na sisi akina pangu pakavu
 
Duuu.Teh teh.Kwanz hii inachekesha.Inawezekana ni kosa lako mkaka.Ulivoanza kumtongoza ulijifanya matawi ya juu kumbe underground na sasa yeye anaendeleza tu mashauzi yako
 
nop..ni ulimbukeni tu .. and sio kwamba you cant take her huko anakosema but yupo dramatically zaidi
 
Tatizo huwa mnaingia na gia kubwa,verrosa ya uncle,outing kibao mwanzo mwanzo
bana bana sasa kibao kimegeuka
 
hayo mambo hata ki shule yapo,hasa shule za sec.mtu anakupa story na kwao wanavyoishi kumbe uongo mtupu.kuna dada mmoja wakati nasoma,siku aliumbuka.alikuwa anaishi k'ndoni shamba,ila ki story zake akawa anatupa picha tofauti na anapoishi.siku alifiwa,wanafunzi tukaenda kwao,uwiiiii.aliumbuka mwenyewe.tangu siku hiyo,mashauzi hakuwa nayo tena
 
yaani hapo kama ndo mm naanza mbio za masafa marefu nikafie mbele!!!!ya nini kuanza kujifunza kipaji cha wizi kumfurahisha mtu????mwambie unachomudu kama anaona we si wa viwango vyake kimbia fasta.
 
Hadi mnafika kote huko ni kwamba ulikua huoni au??? haya mapenzi ya kuiga hayapendezi kabisa
 
Hiyo inatokana na watu kuishi katika maisha magumu, hivyo wanapopata pakujishika hawachezei bahati.
 
Hadi mnafika kote huko ni kwamba ulikua huoni au???

Eti atakwambia alikua anajua yatakwisha tu!!!
Kama kauli ya Dr. Dhaifu isemayo "Janga la njaa Tz ni upepo tu, utapita"
 
Tatizo huwa mnaingia na gia kubwa,verrosa ya uncle,outing kibao mwanzo mwanzo
bana bana sasa kibao kimegeuka

Ukimuuliza kwanini anaingia na Gear kubwa namna hiyo anadai ilikuwa ngumu kwake kunikubali kwa hivi nilivyo.
Hivyo wanaume tunatakiwa tujiamini kwa jinsi tulivyo.
 
watz kwa kucopy ? wewe mleta thread mbona hujasema umetoa wapi hili desa ?
 
hayo mambo hata ki shule yapo,hasa shule za sec.mtu anakupa story na kwao wanavyoishi kumbe uongo mtupu.kuna dada mmoja wakati nasoma,siku aliumbuka.alikuwa anaishi k'ndoni shamba,ila ki story zake akawa anatupa picha tofauti na anapoishi.siku alifiwa,wanafunzi tukaenda kwao,uwiiiii.aliumbuka mwenyewe.tangu siku hiyo,mashauzi hakuwa nayo tena

usinichekeshe !mpenzi wangu!
forodhani kuna mkaka bonge ya mutu sasa hiv
alikuwa anasema anakaa masaki!kumbe anakaa mwananyamala
si alikuwa anapanda mabasi ya posta masaki anashukia palm beach af anapanda ya uswahilini kwetu!lol
ahahahhahahhah wapi mheshimiwa fulani!sikutaji mzee nimekumisss tu popte ulipo lol!
 
hayo mambo hata ki shule yapo,hasa shule za sec.mtu anakupa story na kwao wanavyoishi kumbe uongo mtupu.kuna dada mmoja wakati nasoma,siku aliumbuka.alikuwa anaishi k'ndoni shamba,ila ki story zake akawa anatupa picha tofauti na anapoishi.siku alifiwa,wanafunzi tukaenda kwao,uwiiiii.aliumbuka mwenyewe.tangu siku hiyo,mashauzi hakuwa nayo tena
umenikumbusha mbali sana shosti lol!
mwingine kila mkipiga story ye analeta za uncle wangu alivokuwa newyork,sijui mamdogo ameenda SA enzi hzo tukitajiwa hayo maeneo macho yanatutoka walahi wenzangu na mie hata arusha tu ilikuwa maujiko kwenda mweeh!
sasa sipati picha hiz mtu ukiwa unadate nazo
chezeya kuvaa nguo ya designer wewe!
 
Back
Top Bottom