Umepata kikombe kwa babu loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umepata kikombe kwa babu loliondo

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Dindai, Mar 22, 2011.

 1. D

  Dindai Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Wa Loliondo
  Inasemekana Mzee kaoteshwa dawa ya kutibu “magonjwa yote ”. Wapo watu wanaoamini kuwa ni kweli inaponya na wapo wale wanao tarajia iponye magonjwa yanayowasibu vile vile wapo wengine matarajio yao ni kupona magonjwa wanayofikiria.
  Kupatikana kwa dawa hii tunaweza kuangalia katika mitazamo mitatu.
  1) Magonjwa yote
  2) Watibiwa ( Watu )
  3) Gharama ( Tsh 500.00 tu )
  Mogonjwa yote.
  Kama ni kweli inaweza kutibu magonjwa yote basi hii dawa ni mwisho wa utafiti wa matibabu. Hapa kuna maswali mengi sana ya kujiuliza,
  1) Nini maana ya magonjwa yote?, ni mangapi?, kuna sehemu ipo orodha ya hayo magonjwa?, ili kila anayehisi au kusikia na hata kuona kwamba anaumwa atarajie kupona. Vipi ugonjwa kama wa kusahau ( kupoteza kumbukumbu ), kuona karibu, n.k, dawa inatibu?.
  2) Babu anayo haja ya kujua mgonjwa wake anaumwa nini?, nadhani hiyo dawa ni ya aina moja tu, kwa hiyo kubwa kawake ni wewe kuwa mbele yake na hiyo Tsh 500.00 ( kazi ni kukusanya pesa tu ).
  3) Hii dawa ni lazima mgonjwa utoke popote pale ulipo na uende Loliondo ( wakazi wanaozunguka eneo la Loliondo na Arusha kwa ujumla ulaji huo = utalii.
  Watibiwa ( Watu )
  Ugonjwa wowote unaweza kumpata mtu yoyote awe Mtoto au Mtu Mzima , awe amesoma au awe hajasoma, lakini dawa hii imewafanya watu hawa wote kuwa kitu kimoja , ( hi ni Brainwashing, the attempt to change the thoughts and beliefs of another person against their will ) . Hapa usishangae kuambiwa kwamba karibu wabongo wote ni wagonjwa , lazima babu atasema hii
  Gharama ( Tsh 500.00 na 1000.00 kwa wageni )
  Babu amewafanya wabongo wanaoishi chini ya Dollar moja kwa siku kuiona Sh.500 kama bure, hapa kweli babu kafanikiwa sana kibiashara.
  Jaribu kufikiria watu 2500 wanapata kibombe kwa Babu cha Sh. 500 tu,
  Kwa siku anapata Sh. 1,25,000.00
  Kwa week Sh. 8,750,000.00
  Kwa mwezi Sh. 271,250,000 .00

  SIJUI.
  Watu wote pale Loliondo wanapata wapi huduma nyingine kama za malazi, za usafi , choo n.k.
  Wahusika ( Serikali ) lazima wanafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha matatizo ya kulipuka magonjwa mengine , vile vile wahusika ni lazima wanahakikisha watu wanapata dawa sahihi.
  Kipato anachopata babu kitakuwa shared na wakazi jirani baada ya Kamishna wa mapato kutoa kodi yake.
  Wabongo baada ya kupata kikombe tutarajie kuchapa kazi kwa bidii ( kuongeza uzalishaji ) kwani watakuwa wamepona, hii dawa inaweza kusaidia sana kukuza uchumi.
  Idadi ya Hospitali na Wauguzi zilizopo, ikiwa wahusika ( Serikali ) watabadilisha matumizi ya majengo ya hizo Hospitali baada ya wagomgwa wote kuwa mamepona au wapo kwa Babu Wauguzi (Waganga) wote watapoteza ajira zao.
  IMANI.
  Kama huna imani kupata kikombe kwa Babu huwezi kupona. Baadhi ya watu wapo wanaanza kuuliza watapata wapi dawa ya kupata imani kwanza ili wakienda kwa babu waweze kupata kikombe na kupona ?
   
Loading...