Umeme Wakatisha semina Ya Wabunge!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Umeme umewakatikia wabunge leo wakiwa kwenye semina elekezi ya kikao cha Bunge la bajeti cha mwezi wa 6, na katika hali isiyo ya kawaida, wabunge wa CDM wamesikika wakiimba CCM, CCM,CCM!...
Mbunge mmoja amejieleza kuwa wao kama wawakilishi wa wananchi wanapaswa kuona aibu kwa kufumbia macho mambo ya aibu kama hayo(hoja za umeme) wakiwa ndani ya Bunge!
Ila sijasikia vizuri walikuwa kwenye ukumbi gani!

Semina hiyo imelazimika kuahirishwa baada ya tukio hilo!

cHANZO:Habari ITV saa2.00usiku.
 
Asante mkuu, ni aina fulani ya ufunuo kwa wasio amini kwamba tunaenda mlama. Bado nyengine nyingi zinakuja.
 
Helpless! Kwao sidhani kama ilikuwa ni "WELL DONE TANESCO" Inawezekana ilikuwa hitilafu ya ndani ya jengo..
 
Hizo ni mbinu kali za mafisi-adi kuwatisha wabunge ili waone suala la DOWANS halina mjadala hivyo wallegegeze msimamo(hapa walengwa cdm)na kukubali malipo.naomba wakwell tusimamie HAKI däima.
 
mie naona bora imewatokea wao na iendelee kuwatokea wao kuliko sisi walala hoi labda ndio wataharakisha kuchukua hatua za haraka kurekebisha tatizo hilo maana watu wengi wanakosa ajira kwa sasa kutokana na tatizo la umeme hasa viwandani hata wafanyabiashara wanakosa faida pia na uchumi wa nchi unayumba!

Back
Top Bottom