Umeme huoooo!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Matokeo ya maamuzi ya fisadi Mkapa na Netgroup na KCM, IPTL, RIchmond, Songa na ufisadi mwingine ndiyo haya

Umeme kupanda kwa asilimia 200

2008-03-20 08:39:53
Na Joseph Mwendapole

Shirika la Umeme nchini (TANESCO), linakusudia kupandisha bei za umeme kwa asilimia 200, endapo litaendelea kupata hasara na kulemewa na madeni.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dk. Idris Rashid, wakati wa semina ya wabunge kuhusu Muswada wa Sheria za Umeme na Biashara.

Alisema gharama za uzalishaji ni kubwa sana na kwamba bei za umeme wanazotoza kwa sasa haziwezi kufidia gharama za uzalishaji huo.

Alisema shirika hilo limekuwa likipata hasara kila mwaka, hasara ambayo imekuwa ikiongezeka, na kwamba ili kulinusuru linatakiwa kuongeza bei ya umeme kwa wateja wake.

Alitoa mfano kuwa mwaka juzi Shirika lilipata hasara ya Sh. bilioni 183, mwaka jana Sh. bilioni 72, mwaka 2005 Sh. bilioni 0.9, mwaka 2004 Sh. bilioni 15.6, mwaka 2003 Sh. bilioni 177 na mwaka 2002 Sh. bilioni 72.

Alisema mwaka jana waliomba kuongeza bei kwa asilimia 40 wakaruhusiwa kuongeza asilimia 21 tu.

Alisema shirika hilo linatumia asilimia 90 ya mapato yake kununua umeme kutoka makampuni yanayoliuliza umeme shirika hilo.

Makampuni ya wawakezeji ambayo yamekuwa yakiliuzia umeme TANESCO ni pamoja na IPTL, Songas, Richmond na AGGREKO.

Kamati ya Bunge ya Richmond ilionyesha kwamba mikataba ambayo serikali kupitia TANESCO iliingia na makampuni hayo ina upungufu ambao unawanufaisha zaidi wawekezaji na kuwaumiza wananchi wanaolipia bei kubwa ya umeme.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, ilipendekeza mikataba hiyo ipitiwe upya.

``Hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi mwakani tutaomba tuongeze bei kwa asilimia 200 ili angalau wakipunguza waturuhusu tuongeze kwa asilimia 100 kunusuru shirika,`` alisema Dk. Rashid.

Alisema kama serikali haitaki shirika hilo lipandishe bei ya umeme ililipe shirika hilo fedha zinazotumika kuzalisha umeme.

Alisema hatokubali shirika hilo lijiendeshe kwa hasara na kwamba kila ikibidi watalazimika kuongeza bei kwa wateja.

Aidha, Dk. Rashid, alisema kuwa Sh. bilioni 300 ambazo Shirika hilo lilikopeshwa na benki mbalimbali hivi karibuni, zilitumika kulipa madeni ambayo shirika limeyarithi.

Alisema katika miaka mitano ijayo, Shirika hilo linahitaji mtaji wa Sh. trilioni 1.5 ili liweze kumudu kuboresha mfumo wa usafirishaji umeme na usambazaji.

Dk. Rashid alisema ifikapo mwaka 2012 shirika linakusudia liwe na uwezo wa kuwaunganishia umeme wateja 100,000 kila mwaka kulinganisha na sasa ambapo kwa mwaka ni wateja 32,000 wanaounganishiwa.

Alisema asilimia kumi tu ya watanzania ndio wanapata umeme kwa sasa na kwamba miaka mitano ijayo wamepanga kuwaunganishia umeme asilimia 25 ya wateja.

Alisema wanakusudia pia kupunguza kiwango cha umeme kinachopotea kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 23 hadi kufikia asilimia 13 mwaka 2012.

Katika hali iliyowashangaza wabunge waliohudhuria mkutano huo, Dk. Rashid alisema Tanesco inanunua nguzo kutoka Afrika kusini na India kwa kuwa zinauzwa bei rahisi kuliko zinazotoka Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Alisema wanalazimika kuagiza kutoka nchi hizo kwa kuwa shirika halina uwezo wa kununua nguzo za Tanzania.

SOURCE: Nipashe
 
No wonder Kikwete ameamua kuhamishia nguvu zake Comoro.. nchi hii imemshinda!
 
Mwafika wa Kike ama kweli unaona mbali , maana hili liko wazi .Kasi mpya hii jamani .

Kikwete, ataishia kwenda Kenya, Comoro, na nchi zingine zote wakati raia waliomchagua kuwa raisi wa Tanzania wakiumia na kupata shida.....

shame on you Kikwete.... hii issue ya umeme ni aibu kwako na you have to be ashamed of yourself!
 
Walipa bill za umeme wapo wapi?

Wananchi wa Tanzania wanao beba mzigo wa gharama za umeme wako kimya kabisa kama vile gharama hizi wanabebeshwa Wazimbabwe.

Mapambano ya kumkomboa mtanzania kutoka katika makucha ya ukoloni mambo leo unaendeshwa kupitia makampuni ya kimtaifa yako juu ya mabega yetu Watanzania.

Wananchi wa Tanzania hatuwezi kukaa kimya na kudhani wabunge na viongozi wetu pekee ndiyo watapigana kwa niaba yetu. Tumeona wazi kwamba viongozi wetu
wako upande wa wawekezaji na kujitwalia uwakala wa Ukoloni mambo leo.

Sisi walipa bill za umeme ni lazima tuamke kutoka usingizini na kuanza kupambana wazi wazi.
Maisha Bora tunayo ahidiwa na MH Kikwete ni ndoto ya kijinamizi endapo tutawaachia viongozi waendelee kuwakumbatia wawekezaji katika sekta hii muhimu kama mishipa ya Fahamu na damu mwilini.

Gharama za kuzarisha umeme wa maji kutoka Mtera na Kidatu hazijaongezeka. Maji yanayo tiririka kutoka mto Ruaha ni ya Bure kabisa ni zawadi yetu ya asili.
Hakuna kodi yeyote inaytotozwa kuvingirisha Maparafujo ya kuzarisha umeme.
Sasa gharama hizi za kutisha za umeme tanzania zinatoka wapi?

Gharama hizi tuambiwazo na MH Dr Idrisa ni za Kuwabeba kwa mbeleko Wawekezaji wa IPTL RDC SONGAS na wengine ambao sasa hivi wanazarisha Zero 0 MW lakini wanalipwa mamilioni ya shilingi kila siku.

Mkataba unasema Wawekezaji hawa wazarishe umeme wasizarishe watalipwa fedha yote.
Mahitaji ya umeme nchi nzima hayazidi 700MW umeme wa Kidato na Mtera ni mitambo mingine ya Tanesco huzarisha zaidi ya 750MW ukijumrisha na hizi za Wazembe wa RDC IPTL na SONGAS jumla kuna kama 950MW.
Kimahesabu umeme unaozalrishwa na Tanesco unatoshereza kabisa mahitaji yote ya umeme nchini Tanzania.

Viongozi wetu wakuu wa Kitaifa wantumia matatizo ya nchi katika sekta ya nishati kujitajirisha wenyewe binafsi, badala yakutumia matatizo ya nchio kama chnga moto ya kuleta maendeleo ya kukuza uwezo wa kujitegemea kinishati.
Tangu viongozi wa Serikali ya Tanzania wajue kwamba kuna pato kubwa la kibinafsi katika kuwakumbatia wawekezaji Fake, wamekuwa wakiendeleza wimbi la kuingia mikataba ya ovyo ili mwisho wa siku Mamilioni ya $$$ yaingie kwenye mifuko yao na Mashoga zao.
Viongozi wetu wamegeuka na kuwa Mamluki,yaani Viongozi wa kukodiwa, au viongozi wanoahimizwa na mshahara kuliko kuwajibika.

Kabla hatujajua kwamba tumebebeshwa mzigo na mikataba mibovu ni kweli lilikuwa tatizo la viongozi wetu.

Sasa hivi wananchi wote tunajua wazi kwamba Viongozi wametuingiza katika mikataba inayo yapa Ruhusa ya kisheria Makampuni ya kigeni yatuibie kwa faida ya makampuni hayo na ya Viongozi wakuu wa serikali akiwemo Rais JM Kikwete.

Kwa kujua ukweli huo na kuendelea kukaa kimya au kunung'unika vyumbani mwetu wakati wa usiku mbele ya spouse wetu, tatizo la kulegea na kushindwa kuchukua hatua limehamia kwetu wananchi.

Wanachi ni lazima tuanzishe juhudi za wazi naza makususi za kupinga bei za umeme kwa kuilazimisha serikali kusimamisha mikataba hii ya kishetani na kusitisha kutoa malipo mara moja.

Dhambi hii ya sisi wananchi kukaa kimya na kuendelea na biashara za ubuyu na vitumbua huku tukiacha mambo muhimu ya kitaifa yakiharibiwa na viongozi wenye choyo, itatutafuna mpaka tutabakia mifupa na gozi huku macho tumetoa pima.

Watanzania tuna kazi moja kubwa sana mbele yetu.
Kupambana kufa na kupona na viongozi tulio wachagua wenyewe hadi watakaposalimu amri au kuachia ngazi na kupisha kundi jipya la viongozi wenye uzalendo na wanao jari maslahi ya taifa na kuweka utaifa mbele ya mambo yote.

Wakati wa kuwaenzi viongozi Wazembe na wala rushwa kwa Nyimbo Ngoma na Mashairi kwa mtindo ule wa Kibaraka kepteni Komba( kajinenepea kama kiwavi kwa sababu ya kula bure) umekwisha.

Tanzania ni nchi pekee kati ya nchi zote duniani tuliyo pewa tangu asili ili tuiite nyumbani,hakuna mtanzania mmoja au kikundi cha watanzania wenye haki kuliko watanzania wengine.

Tutapata majeraha,tutadharirishwa utu wetu, tutaswekwa keko, kesi zetu zitatupiliwa mbali, tutanywang'anywa urai,na pengine kupigwa na polisi hadi kufa, Lakini hatutacha kukupigania Ee mama yetu mpendwa Tanzania.
 
Mi naona hapa ili tatizo la umeme litatuliwe haraka labda wananchi wote wa tanzania tuandamane mpaka ikulu kumshinikiza rais aongeze speed ya kurekebisha mikataba yote ya umeme, ili ilinufaishe zaidi shirika la umeme TANESCO, froma that TANESCO itapunguza gharama kwa wananchi. Pia na uhakika pesa zote hizo ambazo zinalipwa iptl na makumpuni mengine zingesaidia kabisa kusambaza umeme vijijini.
 
IT NEEDS COURAGE TO BE TANZANIAN.......! (inauma)INGEKUWA ZIMBABWE WANGEFANYAJE,INGEKUWA TIBET WANGEFANYAJE,INGEKUWA KENYA WANGEFANYAJE.........Kuna mshairi mmoja ambaye baadaye alikuja kuwa rais wa nchi...aliandika shairi ambalo linashabihiina na hali ya sasa.....IT WAS ABOUT CATTLE....BOUGHT......TRANSPORTED...WORKED IN WHITEs PLANTANTIONS.......yes...! it was ARMANDO GUEBUZA....!
 
Nilishasema huyu Rashid hawezi kuwa CEO mkabisha na kuleta credentials zake hapa. TANESCO wana operating cost kubwa sababu ya Lavarage walizo nazo. Lavarage ambazo sio debt, bali ni uzembe wa wanasiasa wa nchi masikini ya Tanzania. Kuongeza cost au kupunguza production sio smart ways za kushindana na unnecessary skyrockets overhead.

Tanesco needs help, lakini sio help ya kuipa billion 30 ambazo next zinakwenda kwa Richmond wa Dowans au IPTL. We need new strategy ambazo kwanza ni kubreach mikataba yote mitatu. Sababu Richmond, IPTL na Songas wote wamesha breach mikataba kwa kutuongopea. That is end of the story, wacha wake file law suit.

Then we need smart economic engineers ambao wataingia Tanesco na kuset new strategy ambazo zitaongeza Account Receivable Turnover, then ni kudeal na how efficiency Tanesco asset can genarate cash. Baada ya hapo tu kuset long term project.

One of the long term project ni kulivunja Tanesco into zones ambazo zitakuwa independent depend na assets. Then ni kuziweka hizo Independent organization public ambazo wananchi watanunu share na kuwa na nguvu ya kuhire top management at the same time to fire them if the screw up. They can do that kwa kutumia Board of Director.

Last, ni serikali kufungua milango ya investors kwenye sector of energy, this will create competition and price will go down. Na kama Tanesco inajiendesha kwa mfumo wa mwaka 1940 wa kuongeza bei za umeme pindi overhead zao zinapopanda then watakuwa driven out of business.

That is how you lead those organization. Na sio kwa kupayuka naongeaza bei umeme 200%, while una current liability kubwa inayoongezwa na Richmond na madereva wa wakurugenzi wasio na kazi. Cost za uendeshaji ni pamoja na wafanyakazi wengi wasio na maana.

Huitaji kuwa wall street analyst kufigure out kwamba Asset za Tanesco haziwezi kutosheleza Liabilities. Na moja kati ya liabilities zao ni unnecessary payments kwa Richmond and unnecessary wafanyakazi wengi ambao kama wata out source price will be way cheaper. Sasa serikali ndio inaongoza kwa strong labor law, na wabunge wasio na leadership background ndio wanatakiwa wajadili maendeleo ya kiwanda. What a non sense.
 
Looh! ni Tanzania tu ambako shirika linaweza kuwa linapata hasara hivyo na ikawa business as usual.

Sasa hiyo hasara nani analipia? Ni tax payers, Naona kila Mtanzania ana mortgage kwenye Tanesco na inakula hela ile mbaya.

Hao Makabauru miaka yote hiyo walikuwa wanafanya nini?

Tanzania kwa kweli hatuwezi kupona. Ukijumlisha hizo pesa zote na zile za mafisadi yaani, hatuhitaji kukopa kwa mtu au kumkenulia meno Bush ili atupatie vyandarua vya dola milioni 5.

Mmmhhh!!! mimi nafikiri hata Tanesco wauzwe tu maana ni kama serikali kwa TZ haiwezi kuendesha shirika lolote. Badala ya kulipia hasara hizo, afadhali shirika liuzwe, na badala yake hizo pesa tunazomwaga Tanesco zitumike kwenye kutengeneza vyanzo vingine vya energy kwa maeneo ya vijijini
ambako uwezo wa watu ni mdogo.

Kule ninakotaka mimi Tanesco wana liofisi likubwa na wafanyakazi zaidi ya watano. Niliwahi kujiuliza hivi kweli Tanesco inahitaji watu wote hawa? Je wanahitaji lijumba lote hilo kama ofisi? Inabidi tujifunze kufanya biashara kwenye karne ya 21. Mtu huwezi kuishi kwa kutegemea baba mpaka unazeeka. Inabidi ifike mahali, kama huna uwezo, basi ukate matumizi yako yote ili uweze kujitegemea.
 
Nchi hii inaendeshwa kibabe,ndio maana wanajifanya hawasikii wala hawaoni.Nadhani JK analenga kutupeleka kwa Mugabe,hivi haya tunayoyasema hayawagusi katika nafsi zenu muone kwamba mko nje ya mstari?Ng'atukeni msisubiri Ngoyayelism

Serikali ilituambia kwamba mradi wa Songas utakapokamilika bei ya umeme itapungua,matokeo yake ni kwamba mradi huo ulipokamilika bei ya umeme ndio ilipanda hivi ni kwa nini mnatufanya sisi ni midoli yenu as if this is your own country and others we are just tenant,who is crazy among this two groups,kumbukeni cheo ni dhamana.Where is ENL.

Wizara ya sheria na katiba mkisaidiana na mwanasheria mkuu wa serikali hivi mmewekwa hapo kukumbatia hiyo mikataba mibovu mpaka lini?Mmeshinwa kabisa kuivunja hii mikataba,au mko upande wa mafisadi,kwa nini mko kimya?juu ya mikataba hii.Au na nyie mmehusika na kwa kupata katen%

Teteeni maslahi ya nchi yenu epukaneni na ubinafsi.
 
JK alishawahi kusema(ipo ndani ya JF) CCM imefanya kazi kubwa na bado inaendelea kufanya kazi ya kuleta maendeleo kwa watu lakini haelewi kwa nini maendeleo hayapatikani.

Hii ndio maana maamuzi mengi ya maendeleo wameacha yanapangwa, yanaamuliwa na kutekelezwa na wafadhili ama wawekezaji kwa manufaa yao, km, mikataba feki ya TANESCO nk, na hivi karibuni mkataba wa kukabidhi Mchuchuma kwa 'middleman'.

Huku Walalahoi wanatulizwa na CCM kwa viandarua vya Bushi ama misaada ya visima nk., wakati CCM inaombea misaada hiyo pamoja na wa Bush usikatwe haraka, ili ingalao kuvuta siku.

Hata hivyo yaelekea mpaka leo, JK na CCM kwa ujumla hawajajua wanashindwaje kudeliver kwa wananchi. Hata tatizo la uadimu na ughali wa umeme hawaoni impact yake kwa maendeleo ya wananchi. Wao wanachojali ni kuiweka CCM madarakaini tu, walahoi watajijua wenyewe.
 
Hivi hao watanzania wanaopandishiwa gharama kila siku wanapandishiwa mishahara kila siku au ndio kuibiana na kudhalilishana?

Nafikiri hizi gharama zikipanda na watanzania wakaendelea kulipa, itabidi tuanze kufanyiana research kuona kama kweli tunafikiri sawa sawa.

Mtu analopoka tu halafu kesho gharama zinapanda na tuendelee kulipa tu wakati inajulikana pesa tunalipa mikataba hewa na zinayoingia kwenye mifuko ya wajanja?

Watanzania inabidi watoke usingizini ikibidi sijui IPTL, sijui Dowans sijui Agreko, sijui Mkapa and Co. wafungashe vilago.

Kuna haja ya wananchi kuiambia serikali iyachukue makampuni yake iyarudishe yalikotoka basi.
:(
 
Kwa mtazamo wangu inaonekana hii mikampuni ya IPTL,SONGAS,AGRREKO na akina Richmond ndo wanaoletea matatizo yote ayo.
Kwani hatuwezi sitisha malipo kwa kutumia vifungu fulani fulani vya sheria.Kama iyo kampuni waliyoreport ya marekani ambao wanalipwa zaidi ya bil 50 kwa mwezi kusupply umeme mpaka leo bila bila na bado twawalipa!

Am sure kuna namna ya kunususru hii hari ingawa inaonekana itaongeza mbinyo kwa watu fulani fulani but it has to be so.

Na uyu Idrisa siyo Mtz nini daily kashupalia kuongeza umeme hajui ilo ni sawa na suicide kwa watz?
Atupe altenative kama anayo sio kukomaa na bei tuuu.

Isije ikawa kisa yeye halipiii huo umeme thats why haipati joto ya jiwe.
Common lets do something else sio kuongeza bei hayo maisha bora yatakujaje jamani?????????????????????
 
Jamani watanzania tuamke tuache kuwa na mawazo mgando, nchi ina resource nyingi amabazo zaweza kuwa ni nyenzo mbadala kwa kuzalisha umeme tukaacha kuwa tegemezi na nguvu za maji (hydro electric power) kwanini tufikirie kutumia upepo ama kule mikoa ya wafugaji tukawa na big plants za biogas, ama kutumia nguvu za jua? hapo awali kuna mwanaJF mmoja aliisha liandika hili..

Nadhani wakati umefika tutumie uranium tuliyonayo nchini kuzalishia umeme, mimegoogle nimeona kuna resource nyingi za uranium Tanzania, lakini kama kawaida yetu makampuni na wageni ndo wanaonufaika hebu angalia hii

In Tanzania, uranium prospection and exploration is being performed by Deep Yellow Ltd, Goldstream Mining NL, Uranex NL, Omegacorp Ltd, Mantra Resources Ltd, Uranium Resources plc , Western Metals Ltd, Sabre Resources Ltd , Uranium Hunter Corporation, Trimark Explorations Ltd., Gambaro Resources, Douglas Lake Minerals Inc, Canaco Resources Inc., Sub-Sahara Resources NL, Tanganyika Uranium Corp., Troll Mining Ltd, African Eagle Resources PLC, Globe Uranium Ltd, Atomic Minerals Ltd external link, Universal Power Corp., International Gold Mining Limited

Source : http://www.wise-uranium.org/upafr.html#TZ

Nadhani nchi yetu inautajiri sana sisi wenyewe ndo maskini na wavivu wa kufikiri,
 
Mimi binafsi sina ubishi na TANESCO kutaka kupandisha bei ya umeme, sina ubishi kabsaaaaaaa! Ila nasema hivi, hicho kiasi wanachokadiria kukipata kwa kupandisha bei ya umeme (ili kufidia hasara wanayopata) wachukue kwa Daudi Balali sh. bilioni 133 zetu, halafu bilioni 50 wachukue kwa Sumaye oh! sorry Lowassa. Hizo zitatosha kwa mwaka huu mzima. Halafu change zetu zitakazobaki kwa Lowassa zitatosha kutusukuma kama miaka kama miwili hivi. Halafu sasa baada ya hapo ndo tutaanza kutoa zetu za mfukoni.

Lakini najua tu hata wakati huo tutakuwa tayari tumepata waziri mwingine wa kumdai. Tukikosa kabisa si tunarudi kumkaba koo Ben? (Mkapa) atupe na yeye alizochukua.
 
``Hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi mwakani tutaomba tuongeze bei kwa asilimia 200 ili angalau wakipunguza waturuhusu tuongeze kwa asilimia 100 kunusuru shirika,`` alisema Dk. Rashid.
.
.
.
.Alisema wanakusudia pia kupunguza kiwango cha umeme kinachopotea kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 23 hadi kufikia asilimia 13 mwaka 2012.

Katika hali iliyowashangaza wabunge waliohudhuria mkutano huo, Dk. Rashid alisema Tanesco inanunua nguzo kutoka Afrika kusini na India kwa kuwa zinauzwa bei rahisi kuliko zinazotoka Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Alisema wanalazimika kuagiza kutoka nchi hizo kwa kuwa shirika halina uwezo wa kununua nguzo za Tanzania.

SOURCE: Nipashe
Tutakoma ubishi!

Hii ni kweli, au nguzo hizo ni zao la magogo yaliyovunwa hapa hapa bongo na kupelekwa S.A?
Na je, nguzo hizi zinapoingizwa nchini, kuna kodi yoyote inalipwa au ndio yale mambo yetu yale ya "wizi, sorry, ....misamaha ya kodi?"

Nataka kuagiza kamera toka Marekani. Pamoja na vikorombwezo vichache tu, thamani inafika $2000 (Sina hamu ya kuagiza mgizo wenye thamani zaidi ya hapo).
Sasa nikifikiria kukatwa kodi napatwa na hasira isiyo kifani, maana ni vigumu kuhamasika kulipa kodi za Jamuhuri ikiwa kuna wizi wa mabilioni tena wa wazi wazi nchi hii.

Kwa electronic gadget ya $2000 nitalimwa kodi kiasi gani wajameni? (Kamera itapitishwa airport imebebwa mkononi)
Naombeni mnijibu ili nijiandae; nisije nikamng'ata mtu uwanja wa ndege bure!
 
Last edited:
Hivi ni lazima ku quote article yote jamani? Si wote tumeiona na kila ukurasa inajirudia kwenye post ya kwanza:confused:
 
Viongozi wetu hasa hawa waserikali bill zao za umeme hulipwa kwa gharama za walipa kodi hivyo umeme ukipanda hauwagusi.Ni sawa askari wa jwtz akilia njaa kwa afande ambao huwa wanapewa mlo wa bure afande atamwelewa???.

Viongozi wetu hawana uchungu kwa wananchi kwani hawabebi mzigo mwananchi anaobeba.

Pili wananchi wanavuna kile wanachopanda tunapochagua viongozi fake wakiingia madarakani nao pia huweka wapambe wao ambao ni fake kama wao.hilo ndo tatizo linalotukabili labda kadri maisha yatakavyokuwa mazito yatawaamusha siku moja.
 
uongozi mbovu tatizo na mikataba yao mibovu ya hizo kampuni.wao si wanabebana kuimaliza nchi? waendelee wataona mwisho wake.
 
Can anybody get those agreements with IPTL, Songas etc here?
We may be able to propose solutions once we know exactly what has been agreed / or not agreed in those agreements.
I am sure there are clauses that could be used to let us B-R-E-A-T-H freely!
 
Back
Top Bottom