Umekumbuka kuchukua zile fedha toka benki?

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Ni tangazo la biashara linalooneshwa kwenye tv na linaibua hisia za mahusiano
kati ya mume na mke, na ndio maana naweka hii thread hapa na si penginepo.
Maudhui ya tangazo yako hivi:
Mume anaingia nyumbani akiwa taabani kwa uchovu. Anajilaza kwenye kochi lililosheheni
mito ya kujipumzisha. Mara anatokea mwanamke (bila shaka mkewe) na bila hata ya kumpa
pole wala nini, anamkumbusha: "Umechukua zile fedha toka benki?" Jamaa anakurupuka
kwenda benki kwa mbio za kimarathon kufuata hela.Anakumbana na madhila ya kunyeshewa
mvua na hela hapati kwani alikuta benki zimefungwa.

Kwa maoni yangu waliobuni tangazo hili, hawakuzingatia uhalisia wa mahusiano kati ya mke na mume.
Mume alipowasili nyumbani nilitarajia mkewe ampokee kwa bashasha ambayo ingehitimishwa
angalau na juisi au kinywaji kingine kidogo. Lakini eti mwanamke anamkaribisha mumewe kwa kumkumbusha
akafuate hela.
Tangazo hili limekosewa sana na watangazaji wa hiyo biashara ya fedha, na ninapata hisia kwamba
they are gender insensitive.

Mlioliona tangazo hili mwasemaje?
 

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,570
2,000
Cha muhimu hapo ni theme ya tangazo......na pengine walitaka kufikisha pia ujumbe kwamba huduma hiyo itakurahisishia transaction kiasi itapelekea hata ndoa yako kuwa tamu and the viceversa ni kwamba hata ndoa haitanoga,hutapewa maneno matamu..hahahaa (joking)
 

mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,472
2,000
Unaelekea uko sensitive sana kwenye swala la mapenzi, anyway ukiongelea uhalisia wa mapenzi ntakupa mfano wangu, mimi na mume wangu muda mwingi tunachat kwenye simu kiasi kwamba hata tunapokutana nyumbani baada ya saa za kazi hatuna habari za kusalimiana maana tushawasiliana sana tu, ikitokea siku akaja mtu asietujua akaona hali ile anaweza akahisi hawa wana ugomvi
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
tangazo liloenda skonga ni hili la joti na fb yake. hapo kweli walifikiri....excellent creativity
Kweli mzabzab. Mahusiano yalizingatiwa kwenye tangazo la joti.
Mzee alikaribishwa kwa heshima zote alizostahili na kuelekezwa jinsi ya kuingia fb.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom