Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,672
Kuna vijana fulani wa mjini, wamekaa kijiweni na kuyajadili maisha kwamba ni magumu, wamekata tamaa na kudai kwamba kamwe hawawezi kufanikiwa! Wengine wanakwenda mbali na kusema kwamba wao wamezaliwa na masikini hivyo watakuwa masikini milele, labda kama wazazi wao na ndugu zao.
UNAKOSEA! Kumbuka utajiri si bahati na ndiyo maana hakuna tajiri anayetajirika kwa kulala tu ndani. Ingekuwa Mengi kapata utajiri kwa kulala tu ndani, Dewji kaupata hivyo au Bill Gates kaupata kwa kulala tu ndani, ningeamini kwamba kweli utajiri ni bahati, ila kwa kuwa walipambana, basi utajiri si bahati bali ni matokeo ya yale yote uliyoyafanya, ni matokeo ya juhudi zako na ufanyaji kazi kwa nguvu.
Mwangalie mzee huyu! Mpaka amefika umri wake, bado anaendelea kupambana! Inawezekana watoto wake wapo mjini, wanakula maisha lakini nguvu ya kupambana bado inaishi ndani yake.
Kwa muonekano, ni masikini, lakini bado hajakata tamaa, sasa kwa nini wewe ukate tamaa? Kwa nini useme kwamba utajiri ni bahati tu na ukae nyumbani? Kama mzee huyo anapambana! Kwa nini wewe usipambane? Amekuzidi nini tofauti na umri? Kwa mzee kama huyo angekaa tu nyumbani na kuweka visingizio kwamba umri umekwenda basi akae asubiri aletewe chakula, lakini cha kushangaza, bado anaendelea kupambana shambani! Una sababu gani za kutoa kusema kwamba ulishindwa kwa kuwa ulikata tamaa?
Ndugu yangu AMKA! Kuupata utajiri si lelemama tu na kamwe utajiri hauji kwa kutulia chumbani ukisoma magazeti! Upo tayari kupambana kama mzee huyu?
TWENDE KAZI!