Nashukuru kwa kutukumbusha kukagua daftari za watoto.Aidha napenda nitoe ushuuda kuwa vyema na very Good pamoja na Excellent nyingi kwenye daftari za watoto si mara zote zinaashiria maendeleo mazuri kwa watoto, kwani mara nyingine ni vichocheo kwa wazazi wazidi kutoa Ada kubwa hasa katika baadhi ya shule za serikali.Binafsi bila kumumunya maneno nasema wazi kuwa nimeyabaini kwenye shule moja ya sekondari pale Dodoma inaitwa DORETA ( Dodoma Retired Teachers Association ) secondary school. Nlikuwa nikigua nakuta alama na masifa kibao kama good na Excellent kwa mdogo wangu baadaye nilistukia ilikuwa nidanganya toto kunilidhisha kuwa mtoto anaendelea vizuri nizdi kutoa ada
Kwa hiyo wazazi na walezi tuweni makini kwa hilo, vinginevyo tutaendelea kusingizia miujiza na kushutumu baraza la mitihani kwa usahihishaji.