Umeishia wapi mchakato wa vitambulisho vya taifa?

Umeishia wapi mchakato wa vitambulisho vya taifa?

Ndiyo maana nikakwambia sio kila taarifa lazima wewe uione kwa urahisi. Taarifa nyingine zimekuwa coded, labda kukusaidia tu kama una kitambulisho hicho sasa hivi geuza upande wa nyuma.

Utaona maandishi: THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA CITIZEN IDENTINTY CARD, chini ya hapo kuna tarakimu 20. Tarakimu 8 za kwanza zinaonesha mwaka wako wa kuzaliwa.

Kuhusu kutokuwa na jinsi, sio kweli usipotoshe umma kwa kuwa mara baada ya "jina la mwisho" pale chini, jinsi ya mmiliki wa ID ipo.

uko sahihi kabisa mkuu, huyu KUKU anabisha vitu asivyovijua kabisa.
 
Wadau hivi huu mchakato wa viatmbulisho vya taifa ambao ulizinduliwa kwa mbwembwe na tukashudia viongozi waandamizi wa serkali wakigawiana umeishia wapi? Mara ya mwisho ulikuwa Dar na Zanzibar baada ya hapo ikawa kimya kulikoni?
Tusaidieni kufahamu kwa mnaojua kinachoendelea.

Hili neno'MCHAKATO'nnalichukia sana,hili neno limeshawapumbaza wananchi wengi sana.
 
nadhani kumeundwa tume ya kuchunguza ucheleweshaji wa vitambulisho vya taifa.
serikali ya tume hii....!
 
Mkuu mbona zoezi la ugawaji linaendelea, kama uliandikishw na bado hujapata kuwa mvumilivu tu zamu yako itafika. Kwa sasa wameanza na watumishi wa umma hasa wa DAR ES SALAAM.

Kama watumishi wa Dsm imechukua zaidi ya miaka miwili maana yake ni kwamba itachukua miaka angalau 20 kumaliza wafanyakazi wa nchi nzima na miaka 100 watanzania wote kupata hivyo vinavyoitwa vitambulisho vya taifa!
 
Ni kuharibu tu hela,mtu kama ana leseni ya udereva ana pass ya kusafiria,vitambulisho vya kazini na hicho sijui cha uaraia ama makazi ni cha nini,kwani ni hati ambayo mtu anaweza kuchukulia mkopo bank
 
Ndiyo maana nikakwambia sio kila taarifa lazima wewe uione kwa urahisi. Taarifa nyingine zimekuwa coded, labda kukusaidia tu kama una kitambulisho hicho sasa hivi geuza upande wa nyuma.

Utaona maandishi: THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA CITIZEN IDENTINTY CARD, chini ya hapo kuna tarakimu 20. Tarakimu 8 za kwanza zinaonesha mwaka wako wa kuzaliwa.

Kuhusu kutokuwa na jinsi, sio kweli usipotoshe umma kwa kuwa mara baada ya "jina la mwisho" pale chini, jinsi ya mmiliki wa ID ipo.

uko sahihi kabisa mkuu, huyu KUKU anabisha vitu asivyovijua kabisa.
Hahahahahahahaha... Mkuu tumsamehe tu maana hakujua alitendalo, alifikiri wote humu ni mbumbumbu wakati tayari watu wanamiliki hizo nyaraka.

Cha muhimu ni kuiomba serikali kuharakisha utoaji wa vitambulisho hivyo na kwa wengine.
 
mkuu grafani, nimecheki nambari za mwanzo ni kweli ni mwaka wangu wa kuzaliwa ila umeandikwa kinyumenyume, year,month,date. thanks kwa maelezo yako.
Mkuu ni kweli kabisa. Tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom