Acheni utani, JF imekuwa ya msaada sana kwangu.
Nakumbuka zilikuwa zimebaki siku chache sana nifunge ndoa. Bestman wangu akawa haeleweki. Nikiwasiliana naye kuhusu mipango ya kwenda kufanya manunuzi (tena kwa ghalama zangu) ananikwepa. Nilipomkumbusha siku ya kwenda rehearsal na kubaini hatuko ukurasa mmoja nikachanganyikiwa. Haraka sana nikamkumbuka mtu mmoja aliyewahi kuniomba mchango wa harusi kwa PM hapa JF. Huyu mtu japo nilimchangia, hatukuwa tumewahi kukutana na wala hatukuwa tunajuana. Roho ikanituma kuwasiliana naye. Jibu lilikuwa, USIPATE SHIDA. Hivyo ndivyo ilivyokuwa JF ikawa imenipa Bestman and Best-friend. Asante sana JF, Udumu Milele
Wapo waliopata wachumba na kuoana hapahapa JF, wapo wanaofanya biashara na kufanikiwa kupitia hapahapa JF, wapo wanaopata mawazo ya biashara na kijasiriamali.
Kuhusu elimu ndio usiseme, JF ni shule tosha. Marafiki pia wanapatikana kwa sana tu hapa mtandaoni, je wewe binafsi JF imekufanyia nini ambacho unaona ni kikubwa?
Ninapoteza muda kujadiliana na ghost names hapa! Sijawahi onana na MjF hata mmoja...ngoja nisepe
nilichojifunza
1.kutoogopa kufa zamani nlikuwa mwoga wa kifo,lakini toka nijue jf siogopi
Swali zuri sana buji buji .. Binafsi sijajifunza lolote zaidi ya kugundua -
1) kuna wa tzn ni wavivu wa kufikiri.. wengi mno humu JF mfano mchungaji REV au MZEE Mwanakijiji . akianzisha thread na kuandika HAHAHAHA "watamwaga thanks nyingi sana" wapo hao watu humu JF
2) kuna watu wanajifanya wajuaji wa mambo na wakibanwa wanatelekeza thread na kuingia na new user name
3) kuna watu ni wapumbavu kiasi kwamba wanaweka kinyongo na avatar yenye jina flani, lakini ni swahiba wa avatar ya jina flani wanashindwa kufikiri kwamba inawezekana zile avatar mbili ni ndugu! its a mater of reading btwn lines
4)Nimegundua wa tzn wengi wana mawazo ya kizinzi
5) Nime gundua wa tnz wengi they are afraid kutoa mawazo yao wenyewe kama yalivyo akiogopa wana JF watakuo kuja na kumuandikia "crap"
6) Nimegunduwa kwamba as long mbongo akiwa na NET + TIME basi anadhani ni lazima a replay kila thread katika jukwaa la siasa la JF mfano mzuri ID ya kings of kings .. topic ikiwa out of his thinking capacity atakopi thread nzima na kutoa conclusion na kuandika crap. au kuweka picha.
7) Nimegunduwa wana JF wanapenda sifa za kijinga "kujianzishia thread" na kujipa hongera!
8) Nimegundua kwamba wana JF wengi they are afraid of being different
9) Nimegundua members wengi wa JF wanadhani ukiwa mwana JF lazima uwe mfuasi wa chadema na kwamba watu wote walio JF basi ni chadema
10) Sijajifunza lolote humu JF but nashukuru napata updates kinachoendelea ndani ya TZN
Wapo waliopata wachumba na kuoana hapahapa JF, wapo wanaofanya biashara na kufanikiwa kupitia hapahapa JF, wapo wanaopata mawazo ya biashara na kijasiriamali.
Kuhusu elimu ndio usiseme, JF ni shule tosha. Marafiki pia wanapatikana kwa sana tu hapa mtandaoni, je wewe binafsi JF imekufanyia nini ambacho unaona ni kikubwa?