Tatizo kubwa la Sikonge ni unyamwezi, ubaguzi kama ule wa kenya, neda Sikonge ujionee wanataka mtumishi yeyote awe na asili ya sikonge tutafika?
M-bongo,
Hivi mtumishi unayesema ni mtumishi wa wapi? Huko hata sehemu za kufanya kazi ni chache sana. Sanasana hospital huko ndiko kuna wafanyakazi wengi na hiyo ni ya Moravian church. Zinafuata shule za secondary za Lowasa na shule za msingi. Shule ya maana ni hiyo ya Mbirani ambayo pia ni ya Moravian na ni ya siku nyingi sana (Lipumba alisoma hapo dara la tano hadi a nane). Vinginginevyo inabaki bank, Polisi, Mahakama, Posta na labda sehemu za simu na Tanesco. Sasa hizi zote sanasana zina watu watano watano.
In short ni kuwa SIKONGE hamna ajira. Hivyo kusema mtumishi atoke Sikonge sijui una maana mtumishi yupi? Kama kuna mtu Sikonge anatoa ajira basi sanasana Waarabu na vigari vyao.
Tatizo la UNYAMWEZI. Hili nakubaliana nalo sana tu. Hili la unyamwezi limechangiwa sana na watu wa pale kuona UARABU ndiyo mali sana. Haka ka-uarabu tumekapenda na tunataka tuwe Waarabu kwa kila kitu. Maadamu wao wana duka, na sisi tunataka tuwe nalo. Tusifanye kazi yoyote tuwe wafanya biashara. Biashara yenyewe ni tufungu twa karanga, kamba za miti ya Miyombo, sindano na uzi, Bangiiiiiiili, nk Huu ni upuuzi wa hali ya juu.
Tatizo la kukosa zao au biashara ya maana inaumiza sana watu huko. Tumbaku si tu kuwa inaumiza na kuzeesha afya za watu. Inamaliza sana misitu ya huko. Ukiingia Google earth, sehemu inaitwa MOLE, utaona jinsi hilo eneo lilivyowekwa sawa na miti kibao imekwenda. Kijiji ni kikubwa sana na nafikiri kinazidi hata Sikonge ambayo ni wilaya.
Kulikuwa na wazo la kuleta Mibono (Jetroph) huko ili walau watu wakilima mara moja wanabaki tu kuwa wanakwenda safishashamba na kuvuna (kama kahawa). Hili zao linazalisha mafuta ya BIODISEL. Ila sijui hata kama hizo mashine zilishafika au zitajengwa huku kwetu. Nyerere aliihurumia Tabora akajenga kiwanda kimoja cha nyuzi. Ila hiki kilijengwa kiSIASA na si kiuchumi. Kilichotokea huhitaji kujua.
Umasikini wa watu ni rahisi sana kudanganywa. Hebu ona hao watu, unafikiri ukiwapa T-shirt si watakupigia kura ingawa wewe ni fisadi? Ukifanya na mnuso wa kurudi kwenu, baada ya kukamatwa kuwa wewe ni FISADI, basi utapokelewa kwa mikono minne. Nategemea hili zao la Mibono litasaidia wengi na kubadili hali ya huko. Ila serikali inabidi kutumia VIBOKO ili kubadilisha watu wa kule. Haka ka UARABU (Ka-Unyamwezi) kanaleta sana shida. Utawaona na kakiswahili kabovu "Habari ya Usubuhi......." wakiwa ndani ya vikanzu na vikofia. Hapo usifikiri ni Waislam, utashangaa sheick kaingia hotelini kujichana wakati ni mwezi wa Ramadhani.....