Umasikini wa kipato waongezeka Tanzania - Ripoti ya maendeleo ya binadamu 2014

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Ripoti ya taifa ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2014 inaonyesha kwamba hali ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja nchini ni mbaya sana. Tanzania imewekwa katika orodha ya nchi ambazo zina maendeleo duni sana ya binadamu. Huku kwa mwaka mmoja tu kutoka 2013 had 2014 ikiwa imeshuka kwa nafasi 7 kutoka 152 hadi 159.

"... A good indicator for this is provided by the UNDP'sHuman Development Index (HDI). As an aggregate oflife expectancy, education, and income indices, HDImeasures the level of human development in a country,ranging from 0 for low human development to 1 forhigh human development.

With an HDI score of 0.488Tanzania falls into the bottom quartile of countries withthe lowest level of human development. Ranking at159 out of 187 countries, the UNDP's Global HumanDevelopment Report for 2014 has therefore classifiedTanzania as a low human development country. Whatis even more striking is that the country's position inthe HDI ranking has decreased by seven positions incomparison to the previous year"

"Tanzania's low human development ranking is furtherconfirmed by the Multidimensional Poverty Index (MPI).Similar to HDI, the MPI is a three dimensional measure ofhuman development. MPI, however, differs from HDI inone important aspect: contrary to HDI, which measuresaverage achievements in living standards, health, andeducation, MPI measures a wide range of deprivationsfaced by individuals and households.

In recent years,MPI has emerged as a strong alternative for measuringpoverty. In the Global Human Development Report(GHDR) for 2013, for example, the poverty standingsof various countries are presented according to their MPIvalues. In GHDR 2013, in which MPI is prepared bythe Oxford Poverty and Human Development Initiative,MPI features as an experimental index.

In the GlobalHuman Development Report for 2014, MPI no longerfeatured as an experimental index but rather as a coreyardstick for measuring living standards. An importantvalue of MPI is that it provides an alternative povertyincidence measurement – i.e. headcount.The difference between these measures can be extreme.

While MPI reports that 64% of mainland Tanzanians arepoor and 31.3% live in extreme poverty, the incomebasedpoverty headcount from the 2012 HouseholdBudget Survey estimates poverty and extreme povertylevels at only 28.2% and 9.7%, respectively.
Although farapart, both measures share two common implications:poverty levels are unacceptably high and the MillenniumDevelopment Goal of reaching a poverty level of 18% by2015 is unattainable" (Tanzania Human Development Report, 2014).


Soma ripoti kamili hapa: http://www.thdr.or.tz/docs/THDR2014-Main.pdf

My Take

Inashangaza sana unapoona watu kama akina Ritz, faizaFox, Lizaboni, Mwigulu Nchemba, stroke na makanjanja wengine wa Chama twawala wanavyokisifia chama chao na Kikwete wao, huku nchi ikiendelea kuumia kutokana na kushuka kwa maendeleo ya binadamu pamoja na kushuka hata kwa thamani ya pesa ya Tanzania.

Mianya mikubwa ya ufisadi iliyotokana na udhaifu mkubwa wa serikali kusimamia uchumi imewezesha watu wachache kumiliki uchumi kuliko serikali, na vilevile serikali imeshindwa kusimamia ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za ndani, na kuongeza mauzo kwenye soko la nje, ikiacha mahindi yakioza kutoka na kukosa soko, huku iki-intertain mikopo mikubwa pamoja na bidhaa za nje ambavyo vyote kwa pamoja vimechangia kwa kiasi kikubwa zimechangia kushuka kwa thamani ya pesa ya Tanzania.

Mambo haya yameanza kupigiwa kelele na wapinzani kwa muda mrefu, huku wapinzani wakibainisha kuwa deni la taifa limekuwa likiongezeka kwa kasi kubwa huku jitihada za kuwakwamua watanzania kutokana na umaskini zikiwa ni ndogo.

Kila mtu hivi sasa anajiuliza hili deni kubwa kiasi hiki la kumfanya kila mtanzania adaiwe laki sita, limetumika wapi? Kama ni barabara basi ni mbovu kuliko hata wakati wa Mkapa ambapo hatukuwa na madeni, hospitali hazina madawa, shule hazina madawati, wala vitabu, huku capitation fee ikiwa haifiki shuleni. Hii pesa inayokopwa kila kuchapo inatumika wapi?

Hiki ni kitendawili kisichojibika.
 
Hapa tumeanza na meli mbili za kulinda gesi ya wachina alafu baadaye tutaanza kuchimba gesi angani tutakapokuwa tumenunua meli za kwenda huko angani
 
Hapa tumeanza na meli mbili za kulinda gesi ya wachina alafu baadaye tutaanza kuchimba gesi angani tutakapokuwa tumenunua meli za kwenda huko angani
Na hapa ndipo kwenye shida, tunaangalia sana foreign economy bila kuangalia ni kwa kaisi gani tunalinda uchumi wa ndani. Mwisho wa siku njia kuu zote za uchumi zinamilikiwa na wageni ambao wanaamua wenyewe kama wauze bidhaa zao kwa sarafu gani - jambo linalochangia kushuka kwa thamani ya pesa, na pia kunapunguza uwezo wa serikali kulinda uchumi wake.
 
Wala sishangai ingawa uchumi wa Tanzania unakuwa zaidi ya majirani gharama za kuishi Tanzania sanasana kwenye miji zipo juu sana ukilinganisha na kwa majirani zetu.

Hili linasababishwa na mambo mengi sana mojawapo kushuka kwa thamani ya sh na kodi la pango ambalo linamwacha mwananchi katika hali ngumu sana kuweza pata mahitaji mengine, ukienda vijijini ukosekanaji wa soko la uhakika la mazao sasa sijui unatagemea mkulima atajikomboa vipi; maisha ya watu wengi kwa nchi za wenzetu sio kwamba ya kimaskini hata ayakizi definition ya mtu mwenye afya.

Nchi nyingine Ndullu na Mkuya wangekuwa wa kwanza kun'goka wameshindwa mbinu.
 
Hizi taasisi zingine kama za kilevi sijaona cha maana kilichoandikwa kipi kinachothibitisha hayo aliyosema .
 
Hapa tumeanza na meli mbili za kulinda gesi ya wachina alafu baadaye tutaanza kuchimba gesi angani tutakapokuwa tumenunua meli za kwenda huko angani
Nilidhani umedhamilia kumbe umekaa kimzaha wala huna mana cha kutuambia katika mchango wako.
 
Hizi taasisi zingine kama za kilevi sijaona cha maana kilichoandikwa kipi kinachothibitisha hayo aliyosema .

Nilidhani umedhamilia kumbe umekaa kimzaha wala huna mana cha kutuambia katika mchango wako.
Wala uhitaji hiyo tafiti kukwambia ukienda kwenye website yeyote yenye takwimu za market basket ukafanya we mwenyewe converts za purchasing power parity ya EAC in dollars capital city yetu is the most expensive to live with that there bound to be many of us in poverty.

Na usishangae kwanini wanadai kiwango kimeshuka badala ya kupanda baada uchumi kukua, kikubwa the cost of living is going up quickly than in our neighbouring states wakati mishahara aiendi sambamba: matumizi ya dollar ni nuksi kwa uchumi wa ndani Tanzania.

Muda muafaka wa Mkullo na dada Mkuya kusema tu hii ngoma si size yao wajipime tu kwenye nafasi zao.
 
Ndio maana wakaleta sheria ya Takwimu ili ripoti kama hizi zisiweze kutolewa tena hadharani bila kufanyiwa usanii
 
Kwa wakereketwa na wafia chama mara zote tumewaeleza tafsiri sahihi ya maendeleo sio vitu bali ni watu. Jengeni chochote lakini bila kuwajenga watu ni kazi bure.
 
Wanasemaga uchumi unapaa
Ni kweli uchumi wa jumla unaonekana kukua kwa asilimia kati ya 6 na 7, lakini kipato cha mtu mmoja mmoja kinazidi kushuka. Lakini utashangaa kwamba hili linatokea huku serikali ikiwa haina pesa kabisa. Kwa msingi huo unagundua kuwa huo uchumi unaokua, kimsingi unatokana na watu wachache waliomiliki uchumi wa nchi na si kwa watanzania wote. Maana serikali ni bankrupt, yet umaskini wa kipato unaongezeka. Pesa ipo wapi? Ukimsoma vizuri P60 utaelewa kwamba uchumi upo mikononi mwa mapebari wachache ambao ndiyo wanashikilia market price, na kuwafanya watanzania wa kipato cha chini, wasiomiliki uchumi kuwa na hali mbaya sana. Na hapa mianya ya ufisadi imechangia sana.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: P60
Back
Top Bottom