Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,232
Juzi kati nikiwa nimevurugwa kwa kukosa hata thumni ya kununua walau bigijii ya kutafuna, yaani sikuwa hata na shilingi mahala popote pale (mfukoni, ndani wala kwenye akaunti) basi nikaona nisiingie kazini bali siku hiyo niitumie kuzurura (kutalii) maeneo ya mbali na ninapoishi.
Lengo la kuzurura huko lilikuwa ni walau kupunguza msongo na kutafuta wazo jipya la kujikwamua maana niliandamwa pia na madeni madeni. Basi bwana nikaamka asubuhi sana (kama saa 11 hivi) nikiwa full loaded na mawazo nikaanza kukanyaga
Basi bwana nikiwa njiani kuelekea huko niendako nikafika sehemu (kulikuwa kumepambazuka tayari) nikaona maandishi chini katikati ya barabara ambayo yalinifanya niwaze zaidi na kutafakari sana ambapo mpaka leo huwa siyapatii majibu
Baada ya mwendo kidogo mbele yangu nikagundua kulikuwa na mtu anatembea kuelekea kulekule niendako sasa akawa akigeuka anaona jinsi ninavyowahi na yeye anaongeza mwendo zaidi kwa kunihofia (maana ilikuwa asubuhi sana na ni porini kidogo pia yeye mwanamke mimi mwanaume)
Alijitahidi mwishowe alishindwa nikamkuta na nilipomkaribia nikagundua kumbe ni mwanafunzi naye kwa woga akajidai kama anataka kukatisha kuna sehemu ilikuwa na njia ndogo ya kuchepuka basi akawa amesimama tu haendelei wala hakatizi kwenye ile njia. Nikawa huku namkuta huku nawaza huyu ndiye aliyeandika maneno yale, kwanini na yeye anakwenda wapi asubuhi yote hii
Aliniamkia nikaitikia na nikamuuliza baadhi ya maswali; alinijibu kuwa anakwenda shuleni alipochaguliwa form one mbali na kijiji chao hivyo analazimika kujidamka sana maana hana baiskeli kama baadhi ya wengine, hana uniforms kwa kuwa bado hajashonewa, wengine wa hali yake walichaguliwa wakaghairi kwenda sekondari
Nikataka kumuuliza kama ni yeye aliyeandika maneno yale yaliyonikosha lakini moyo ukanizuia basi nikamuacha hapo nikampita zangu. Baada ya kumpita na nikawa na mwendo wangu uleule kama kawaida wa harakaharaka ndipo na yeye akawa na amani sasa akaendelea na safari yake
Tangu siku ile mpaka leo huwa nawaza sana mbona yale maandishi yalinilenga sana na ni nani aliyaandika na kwajili gani (maana moyoni huwa nakataa kusema ni yule binti kwavile mwandiko ukiuangalia ulikuwa ni wa kiume plus mazingira mengine mengine niliyoyakuta)
Maandishi yale yaliandikwa kwa herufi kubwa na yalikuwa yakisomeka hivi;
"UMASIKINI SI KITU CHEMA"