Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Kuna dada alinihadithia alivyokutana na mume wake. Walisoma wote shule ya msingi enzi zile za ujamaa hakuna English Medium wote tulikuwa St Kayumba. Mume wake alikuwa anakuja shule na deli la Ice cream, nyumbani hali haikuwa nzuri sana na kila mtu alichangia alivyoweza. Mama aliuza maandazi na watoto wengine walipewa karanga.
Enzi hizo dada anashushwa shule na STG na akitoka shule inamsubiri. Hawakuwahi kuzoeana. Walikutana chuo kikuu, wakati huo kijana nae ana boom. Walikumbukana na wakaanza kupiga stori. Kutokana na maisha aliyopitia kijana alikuwa mshauri mzuri kwa bi dada.
Walianza kuwa wapenzi wakiahidiana kufunga ndoa. Bidada alipomkaribisha kwao kijana alikosa kabisa amani ya kumpeleka kwa mama yake ambae ni single mother wa watoto watatu, wamepangisha vyumba viwili.
Dada alielewa hali walikubaliana kufanya harusi ndogo tu ya katikati ya wiki mradi kijana atoe posa kwao. Madada wakubwa wa msichana walimshauri aachane na kijana masikini atabeba mtatizo ya ukoo. Huyu dada anasema si mapenzi tu,?heshima aliyopewa na kijana alikua hataipata kwa mwanaume yeyote yule mwingine.
Walifunga ndoa na kuanza maisha. Mama walimjengea nyumba, mama mwenyewe ni muelewaji wa hali anajiongeza sana. Anauza maji mtaani kwake wala si wakuomba pesa ya kula.
Dada ana amani na ndoa yake, mume wake ameahidi kumpeleka ofisini asubuhi na kumchukua jioni kama ile STG ilivyo mhudumia wakiwa shulevya msingi.