Umasikini na siasa

Mathew A

Member
Jan 9, 2018
57
50
Kama kichwa kinavyojielekeza ninakusudia kueleza ni kwa namna gani umaskini ambao umekua ndio nyenzo muhimu katika kukamata nyazfa muhimu Serikalini na jinsi unasababisha umaskini kuongezeka badala ya kutumika kuupunguza.

Tutakubaliana sote Kwamba viongozi wengi wamekua wakijipambanua kuwa wanaujua umaskini na kwamba waliuishi hii ni kutuamisha kwamba wanauchungu na umaskini wa watu na kwamba watahakikisha wanaupunguza na hatimae kuisha kabisa.

Jana tu wakati mheshiwa Rais akihutubia alieleza namna ambavyo miradi mingi inakwamishwa na urasimu na watu waliopewa nyazfa za juu serikalini na Miradi hiyo ingekuja kuondoa tatizo la ajira na kupunguza umaskini wa watanzania.

Umaskini mbaya sana ndio maana naupinga kuwa kama nyenzo ya kumpata kiongozi wa Serikalini, hapana kwa upande wangu maana wengi wao hutumia kujipatia utajiri bila hata ya kujali angetatua umaskini wa watu wangapi

Mwisho lakini sio kwa umuhimu ni vyema sasa tukatumia sifa za kiutendaji kuanzia chini mtu alipoajiriwa ili kupima uwezo wake na uzalendo wake ambao utatuamisha kwamba hata akipewa nyazfa nyeti hatajinufaisha mwenyewe na kuachana na stori za naujua umaskini maana kuna tofauti ya kuujua na kuutatua.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Niwatakie jtano njema
 
Chanzo kikuu cha umaskini nchini ni Ccm na Serikali yake. Siku Watanzania tukiamua kuwaweka pembeni, naamini nchi hii itapiga hatua kubwa sana kiuchumi.
Hao wahuni wote unaotegemea wataleta mabadiliko ni kina nani wote ni ccm hao piga kazi ujiletee maendeleo ,hayatakuja bila ya kazi!
 
Watu huko juu wanipiga pesa kizembe sana...
Wanachelewesha malipo makusudi...
 
Back
Top Bottom