Jaji Tz
Member
- Feb 16, 2015
- 33
- 19
UMARIDADI WA MTOTO WA AFRIKA
Jicho [emoji872] Jaji_Tz. (African boy)
Wakati tunahitimisha "SIKU YA MTOTO WA AFRIKA" nitumie Maneno machache kuzungumza na Watanzania na Serikali yangu pendwa ya awamu ya sita chini ya Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Mtoto huzaliwa na kipawa/kipaji chake wapo wengi ni mwahandisi,walimu na wengine ni madaktari na umahili huo hujionesha utotoni lakini watoto wengi mazingira baada ya kuzaliwa hupoteza Vipawa vyao, Malezi ya nyumbani hufubaza uwezo wao wa kuvikuza vipaji vyao na Mfumo wa Elimu humalizia chembe za vipaji vyao iliyosalia" Mfano zipo picha zikionesha toroli la miti (ngorogojo) magari ya maboksi, majumba n.k ambazo huwa zinatengezwa na watoto kama sehemu ya michezo ya utotoni na kwa baadhi ya wazazi huwaathibu mno watoto kwa mwamvuli wa utukutu lakini ukitafakari mtoto huyo anaonesha umahili wake wa kubuni na kufaragua zana kuwa kifaa cha kurahisisha kazi, Mfano:- inatengenezwa toroli la miti kubwa ((bajaji) kuyeka)) ambalo hubeba hadi mizigo shambani.
Pia wapo watoto wanaocheza mpira Vizuri, wavuvi wazuri hasa kanda ya ziwa na pwani hubainika vyema, pia wapo wahandisi wa ujenzi wa barabara za miti, magari, nyumba za udongo kama michezo yao ya kila siku.
Nini kifanyike?
Serikali, wanasiasa, wadau na wasomi toweni elimu ya kutosha kwa wazazi juu ya vipaji vya watoto na namna bora ya kuviendeleza kuanzia nyumbani.
Serikali kama mdau Mkuu wa Maendeleo nchini iwekeze nguvu na umakini kwenye mitaala ya elimu msingi iwe inaendeleza ubunifu, kipaji na umahiri alionao mtoto ikiwezekana kuwepo na Karakana za kutosha kwa kila shule ya msingi na sekondari kulingana na vipaji vilivyopo.
Elimu iwe sekta kuu ya maendeleo nchini na iwe katika mfumo wa mwendelezo wa vipaji kuanzia msingi, sekondari na vyuoni na isimpime mtoto kwa taaluma ya darasani pekee ipanue wigo wa sehemu zingine za vipaji.
Kuwepo na mikopo nafuu kwa taasisi na watu binafsi wenye nia ya dhati kuendeleza vipaji vya watoto. mfano kuanzishwa kwa academy za michezo kila wilaya, kuwepo kwa viwanda vidogo kwa kila shule.
Kuajiri wataalmu bobezi wa vipaji husika kulingana na wingi wa watoto wenye kipaji husika.
Haya yakitekelezwa yatasaidia yafuatayo:
Kuwepo watalaamu wa ndani wabobezi katika fani husika kulingana na vipaji vyao.
Kupata ubunifu mpya kazini na maofisini kwani sifa ya kipaji huwa inajiupdate kulingana na uendelezwaji wake.
Kupunguza vijana tegemezi wa ajira kwani wapo watakao jiajiri wenyewe kwa ujuzi unaotambulika kiserikali.
Kupunguza watoto wa mtaani kwani kila mtoto anakipawa/kipaji chake na anakipenda kweli hivyo atakiendeleza na hatoacha shule.
Kupata watalamu wenye uchu na wazalendo wa kazi zao wenyewe hivyo kuzifanya kwa ufanisi Mkubwa na kwa ushindani.
Kuongeza pato la taifa kwa kuwa na vijana wengi wanaomaliza elimu zao kuingiza kipato kikubwa kitokanacho na kazi rasmi zinazowapelekea kulipa kodi kwa taifa.
Mwisho niainishe vipaji kadhaa
vinavyothibitika mapema kwa watoto:-
Ufundi
Wahandisi (nyumba, simu,barabara, magari, umeme) ,Michezo (riadha Mmiguu/mikono pete), Madaktari, walimu, Askari, wasanii, Watangazaji, waandishi ,Wachungaji, mashekh, wasusi, washonaji, Wafanyabiashara, Siasa, Uongozi n.k
Note:
Tukiwalea vyema watoto tutakuwa tumewaanda vyema vijana Waadilifu na wazalendo ikiwa ni maandalizi ya wazazi, watumishi,washauri bora wa Taifa letu.
#Mtoto- ni malighafi endelevu kwa taifa pevu.
cc. Jaji_Tz.
African boy
June''17''2021
+255758302764