Umajumui wa AFRIKA na Nkhurumah

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
351
866
NI KWAME NKHRUMAH NA DHANA YA UMAJUMUI WA AFRIKA.

NA Comred Mbwana Allyamtu.

Kwame Nkrumah (1909- Aprili 27, 1972) alikuwa ni kiongozi wa Ghana aliyepigania uhuru wa taifa lake kutoka Uingereza na baadae kuchaguliwa kuwa kiongozi mwaka 1957 kabla ya kuwa raisi wa taifa lake aliwahi kuwa waziri mkuu wa nchi yake na baadae kuwa rais wa kwanza nchini Ghana.
Katika halakati za Ukombozi Nkhurumah ilikuwa na ushawishi mkubwa katika karne ya 20 katika vuguvugu la harakati za mtu mweusi kwani alikuwa ni mtetezi wa Pan-Africanism, na pia aliwahi kuwa mwanachama mwanzilishi wa Shirika la Umoja wa Afrika katika kipindi cha mwanzo ilipokuwa ikianzishwa umoja huo na baadae Nkhurumah alikuwa mshindi wa tuzo ya Lenin ya Amani na ya Nobel mwaka 1963.
Nkhurumah alipata elimu yake nchini Marekani, Nkrumah alionekana kuwa na mafanikio katika halakati za mageuzi katika Mapinduzi ya maisha hasa kwa MTU mweusi kwani aliwahi kupata shahada ya Sanaa katika uchumi na Sosholojia mwaka 1939 Katika chuo cha Lincoln kisha aliteuliwa kuwa kama msaidizi mhadhiri katika falsafa chuoni hapo. kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza na ustadi wa mazungumzo ndipo yeye alianza kupokea mialiko mbali mbali kuwa mhubiri katika matamasha na walsha mbali mbali na mgeni katika makanisa ya Presbyterian katika mji wa Philadelphia na New York huko marekani alipokuwa masomoni.

MCHANGO WA KWAME NKHRUMAH KATIKA DHANA YA UMAJUMUI WA AFRIKA.

Nkrumah alitumia muda wake mwingi juu ya maandalizi ya kisiasa. Yeye na rafiki yake Padmore walikuwa miongoni mwa waandaaji wa kuu wa Tano wa kile kilichoitwa "Congress Pan-African" iliyofanyika huko Uingereza katika mji wa Manchester. Katika mkutano Nkhurumah alifafanua mkakati na Mlengo yake wa kuweza kuzikomboa nchi za Afrika na kusema umoja ndio njia pekee inayoweza kuwa weka pamoja waafrika kwani unyonyaji na ubaguzi wa rangi kimsingi inazidi ukoloni uliopo barani Afrika.

Nkhurumah alikuwa na imani za Ujamaa wa Kiafrika (Africans Socialism) na hatima yeye na wenzake Walikubaliana kuendeleza shirikisho Umoja wa Mataifa ya Afrika ili kuweza kuikomboa AFRIKA yote kutoka mikono ya ukoloni, na interlocking mashirika ya kikanda, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia viongozi wa Ukombozi kupitia mataifa tofauti yatakayo kuwa yanadai Uhuru. Nkhurumah alipendelea na Walipanga kujiingiza katika utamaduni mpya wa Afrika bila ukabila na demokrasia ndani ya mfumo wa ujamaa au ukomunisti ikiwa ni pamoja na kuikusanya masuala ya jadi na fikra za kisasa.

Lengo lilikuwa ni kuijenga msingi ya Ukombozi katika Afrika na kwa hili kulipatikana kwa njia na mikakati ya vuguvugu za kudai uhuru pia Miongoni mwa wale viongozi maalufu waliweza kuudhuria mkutano huo na walikuwa wenye heshima katika vuguvugu la MTU mwusi kama W.E.B. Dubois, Marcus Garvey na baadhi ya watu ambao baadaye ndio walikuwa na chachu ya ukombozi na kudai uhuru kwani walichukua majukumu ya kuongoza halakati katika kuongoza mataifa yao kwa kudai uhuru, ikiwa ni pamoja na Hastings Banda wa Nyasaland (ambayo baadae ikawa Malawi), Jomo Kenyatta wa Kenya na Patrice Lumumba, aliyekuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kama kiongozi wa raia wa Kongo-DRC.

Nkrumah alikuwa na ndoto ya kuifanya Pan-Africanism ifikie katika hatua ya kuwavutia wasomi hasa wale wafrika waliokuwa wakiishi huko ughaibuni waweze kuludi nyumbani AFRIKA kuja kuongoza mapambano ya Ukombozi na ndivyo ilvyokuja kuwa baadae kwa viongozi kadhaa kuvutika kuludi Afrika kuongoza mapambano ya Ukombozi akiwemo Benjamin Nandi Azikiwe wa Nigeria, Madibo Keita wa Mali, Dauda Balewa wa Gambia, Mirtoni Malgai wa Sierra Leon, Saad Zaghuri wa Egypt, Samora Machel wa Mozambique na mengine wengi.
Wamarekani weusi wengi, kama vile Du Bois na Kwame Ture, wakiongozwa na Ghana katika kuungana naye katika juhudi zake Katika vyombo vya habari na hasa afisa wake wa habari kwa miaka Karibu sita aliweka andiko kwenye gazeti la Uingereza lilofahamika kwa jina la Grenadian alichapisha jarida la "anti colonialist" na afisa huyo aliitwa Sam Morris. Pamoja na hilo Nkrumah alitajwa sana kama mmoja ya viongozi ambao walipata mafanikio makubwa sana katika eneo hili la ushawishi wa Umajumui wa afrika (Pan Africanism) hatu hiyo kwake ilitajwa kuwa ni kubwa katika kuzinduliwa kwa Shirika la Umoja wa Afrika hapo baadae.

UHURU WA GHANA NA SIASA KATIKA UTAWALA WA KWAME NKHURUMAH.

Ghana ilipata uhuru wake Machi 6 1957. Na Nkhurumah kuwa Kama wazili mkuu wa kwanza wa Ghana huru aliye itoa nchi yake kwenye makucha ya makoloni ya Uingereza Nkhurumah alifanikiwa kupata wingi wa kura wa chama chake cha CPP katika balaza la kutunga sheria na kutengeneza utawala wa nchi ilyokuwa na uhuru, aliapishwa kuwa waziri mkuu wa kwanza katika uwanja wa independent square siku ya maadhimisho ya uhuru katika mji wa Accra tarehe 6/3/1957.

Katika siku hiyo ndio iliyotoa hotuba yake maalufu katika kutwa Dola ya serekali yake kwani kulikuwepo na wana dipromasia wa karibu dunia nzima na waandishi wa habari zaidi ya 100 na wapiga picha walioweza kuripoti matukio. Kwa upande wa mataifa makubwa kama Rais wa Marekani Eisenhower wa wakati huo alimtuma pongezi Nkhurumah na pia Makamu wa Rais wa marekani Richard Nixon, aliamua kuwakilisha taifa la USA katika shuguli hiyo kutafuta ushawishi wa taifa lao. Huku upande mwingine wa matukio ujumbe kutoka Urusi ilikuwa ni wito wa Nkrumah kutembelea Moscow haraka iwezekanavyo
Nkrumah aliendeleza kukuza utamaduni wa Pan-African katika utawala wake wito huu mwake kwa Afrika ilikuwa ni kuhakikisha AFRIKA inakuwa huru. Katika kuhakikisha anajenga fikra Mpya ya AFRIKA kwa hatua ya awali alipinga hadharani mfumo wa ulaya katika elimua katika nchi yake ikiwa ni pamoja na kuondoa vitabu vyenye kuunga mkono na kutimiza dhana za ulaya (Eurocentrism) katika maktaba zote nchini mwake ikiwa ni pamoja na kuunda vyama vya ushirika kwa kujifunza historia na utamaduni wa kiafrika (Afrocentrism). Yeye alilaani kanuni za (ukuu nyeupe) na (Eurocentrism) zilizowekwa katia vitabu vya kiada vya Uingereza na taasisi za kitamaduni nchini mwake.
Awali kabisa Alisimamia ufunguzi wa Makumbusho kuu ya Ghana Machi 5 mwaka 1957; akaunda Baraza la Sanaa la Ghana, akaanzisha mrengo wa Wizara ya Elimu na Utamaduni, na utalatibu huu uliigwa na mataifa mengine mengi Afrika ikiwemo Tanzania.

mwaka 1958; akazindua Library Juu ya Utafiti wa Masuala ya Afrika (Africa conceptual research) mwezi Juni, 1961; na kuzindua Ghana Film Corporation mwaka 1964. Huku Mwaka 1962, Nkrumah alifungua Taasisi ya Mafunzo ya Afrika yote hayo ilikuwa ni kuifanya dhana yake ya ujamaa wa kiafrika (Afrocentrism) iweze kufanikiwa.
Nkrumah alijaribu kwa kasi kubwa kuhalakisha uchumi wa nchi yake (economy industrialized) uchumi wa viwanda katika nchi yake ya Ghana. Alitoa wito kuwa iwapo kwamba kama Ghana ita amua kuachana na mfumo wa kutegemea ulaya hasa katika mfumo wa biashara ya kikoloni na hivyo kupunguza utegemezi wa mitaji ya kigeni, teknolojia, na vitu vya kimwili, inaweza kuwa na uhuru wa kweli.

KUPINDULIWA KWAKE MWAKA 1966.

Kutokana na siasa za Nkhurumah katika kuhimiza mapambano na halakati AFRIKA ikiwa ni pamoja na kuegemea katika siasa za USSR (Soviet) ilimjengea uadui Nkhurumah katika siasa za Ubepari na hasa marekani kitu kilichopelekea hatimae kupinduliwa kwa serekali yake.
Hatmaye Mwezi Februari 1966, wakati Nkrumah alipokuwa katika ziara yake ya kizazi nje ya nchi katika kuhakikisha anaimalisha hali ya uchumi wa Kijamaa ndio alipo kuwa nchi ya Vietnam Kaskazini na China, serikali yake ilipinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi yaliyokuwa yakiongozwa na Emmanuel Kwasi Kotoka na Baraza la lake aliloliita balaza la Taifa la Ukombozi ( Natinal Council of liberation- NCL). Pamoja na mapinduzi hayo kumekuwepo na dhana juu ya mapinduzi hayo na pia kumekuwepo na kuhusishwa kwa njama za kuhusika kwa Mapinduzi ya kuiondoa serekali yake madalakani na Ushahidi wa hilo ni kuwa wanamapimduzi kwa karibu waliweza kushirikisha Marekani katika kutekeleza mapinduzi hayo na toka kipindi hicho Marekani ilishindwa kukanusha wazi na hivyo madai hayo kubaki kuwa ni ya kweli.

Hata hivyo Mwaka 1978 John Stockwell, aliyekuwa Mkuu wa CIA nchin Angola katika Kikosi Kazi, aliandika kwamba mawakala wa kutoka CIA waliokuwa katika ubarozi wa USA nchini Ghana mjini Accra katika kituo cha Ghana alisema alipokea ujumbe wa simu ya maneno uliosema "ulinzi uiimarishwe kwa kuwa tayali kikosi cha mapinduzi kumewasiliana kwa ukaribu sana na plotters wa USA kama mapinduzi yanafanyika na lazima wawalinde na utalatibu zimeundwa tayali." Baadaye alipokea ujumbe mwingine uliosema, "ndani ya makao makuu ya CIA Kituo cha Accra alipewa taalifa kuwa sasa tayali rasmi mikopo kwa ajili ya mapinduzi ya baadaye imetoka na kikosi cha Mapinduzi kiwekwe tayali ..)
Pia Declassified ya Bunge la Uingereza walifanya upelelezi wa nyaraka za MI5 na wameonyesha kuwa Uingereza walifanya upelelezi wa walaka inayojulikana kama "Swift" ambayo ilionyesha kuwa M15 na M16 walikuwa wameweza kujipenyeza duru zao za ndani katika serikali ya Nkrumah.
Nkrumah baada ya Mapinduzi hakurudi Ghana, lakini aliendelea kushinikiza kwa maono yake juu ya umoja wa Afrika. Nkhurumah mwenye aliishi uhamishoni katika mji wa Conakry, Guinea, kama mkimbizi wa kisiasa na mgeni wa Rais Ahmed Sékou Touré, ambaye alifanya naye heshima na kupeana ushirikiano wa Karibu na rais wa nchi. Nkhurumah aliendelea na kusoma, pamoja na kuendelea na kuandika vitabu mbali mbali pia aliendelea na mawasiliano na viongozi mbali mbali wa Afrika ikiwa ni pamoja kushilikishwa katika makongamano ya kimataifa pamoja na hayo yeye aliweza kuwakaribisha wageni Licha ya kustaafu kutoka ofisi ya umma.

Pamoja na kuishi uhamishino bado njama za kumuua ziliendelea kupangwa na hata wakati moja kurilipotiwa kuwa mpishi wake aliandaa kumuua kwa kumwekea sumu katika Chakula kitu kilichokuja kugunduliwa baada ya mpishi mwingine kula Chakula kile Kabla ya Nkhurumah kukila Chakula kile kitu kilichopelekea mtumishi yule kufa. Na ikagundulika kuwa Chakula kile nilikuwa na sumu, hivyo kupelekea Nkhurumah akaanza kuhodhi chakula katika chumba chake bila mfanyakazi wa kuandaa Chakula chake. Yeye Nkhurumah aliendelea kuwatuhumu mawakala wa kigeni hasa marekani na Uingereza walikuwa wanapanga njama za kumuua na hata kuwalaumu kuwa alipewa sumu ya kuvuta katika harufu walikuwa wamemuwekea katika njia ya barua,

Na baadae alipata alianza kusumbuliwa na matatizo ya moyo kitu kilichopelekea kwenda Bucharest, Romania, kwa Matibabu na hatimae mwaka 1972 alipoteza maisha.

"Mungu ilaze roho ya marehemu Kwame Nkhurumah pema Amini"

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Kwa Msumbiji (Mozambique)
+27 874791033.
Email- Mbwanaallyamtu990Gmail.com
0ccf3b456ad2e8425c326adfe9f15cf0.jpg
 
Back
Top Bottom