Kwenye meza ya usuluhishi na mazungumzo ya mapatano, ogopa sana mtu mwenye ndimi mbili. Mtu akiwa "prescient, prejudiced, biased & having preconceived ideas" kwa maslahi ya chama chake na cheo, hawezi kwa vyovyote vile kuaminika kuongoza mchakato.
CCM imeonyesha rangi halisi waliyokuwa nao. Hawana dhamira njema juu ya mustakabali mwema wa taifa letu. Wao hufikiri neno "utulivu" lina maana sawa na lile la "amani".
Mfumo huchoka, taasisi huchoka, vyombo vya dola navyo huchoka, na hapo ndipo mwanzo wa mbeleko kuchanika. Siku yaja, nayo i karibu, chama hiki kikongwe kitasambalatika na kutokomea kabisa.