Wana jamvi naomba mnisaidie, mke wangu alikuwa mjamzito. Alianzia kliniki Temeke hospital, akaambiwa atajifungua watoto mapacha baada ya vipimo vya ultra sound. Akahamishiwa hospitali ya Muhimbili ambako pia akaambiwa atajifungua watoto mapacha. Na alijifungua kwa oparesheni mtoto mmoja. Je hapa hakuna uchakachuaji au inawezekana vipimo vikakosea katika hospitali mbili tofauti?