Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,109
- 1,648
Bila shaka hamjambo wana JF, bila kupoteza muda kama ambavyo kichwa cha habari kinacho jieleza niingie moja kwa moja kwenye kero hii.
Hospitali hii imekuwa ikilalamikiwa na watu wengi sana kutokana na huduma ambazo zinatolewa na wahudumu wake baadhi yao, kuwa wana maneno/ kauli mbaya kwa wagonjwa.
Mwaka jana mfanyakazi mwezangu alipata ajali akapelekwa hospitalini hapo, vipimo vya X- ray vilionyesha amevunjika kidole kidogo cha mkono wa kushoto, matokeo yake mkono mzima akafungwa P.O.P amekaa nalo karibu mwezi mzima, kwenda kutolewa mkono umebadilika rangi umekuwa na rangi kama ya blue.
Baada ya kutolewa alikataa kupata huduma tena kwenye hospitali hii ilibidi aende ya Private huko alifanyiwa operesheni ndogo ya kidole na baada ya wiki mbili akapona.
Mgonjwa mwingine alipekwa Mnazi Mmoja mwaka jana akiwa anatapika damu, alipelekwa Jumapili lakini hakupewa huduma yoyote hadi kesho yake alasiri tena mgonjwa baada ya kukasirika na kuwatolea maneno wahudumu ndipo wakamhudumia.
Mama mmoja mjamzito alihamishiwa hospitali ya Mnazi Mmoja, mwaka huu Mwezi wa Aprili ili akajifungue, alijifungua mapacha ambao umri wao miezi ilikuwa bado, watoto wale wote walifariki kwa sababu ya uzembe wa wahudumu wa afya.
Hospitali hii inalalamikiwa kuwatumia wanafunzi ambao wapo field ambao bado wanahitaji usimamizi wa karibu wa wenye ujuzi.
Kijana mmoja kaenda kwenye hospitali hii kwenye kitengo cha macho na masikio, anaambiwa tiba yake kutibiwa hospitalini hapo hadi mwezi wa kumi 2020 au aende hospitali ya binafsi ya Al-rahma akatajiwa siku ya kliniki kwa wagonjwa wa masikio hospitalini. Al-rahma na bei yake ya matibabu, jamani kweli Mnazi Mmoja hospitali kuu ya rufaa imwambie mgonjwa wa sikio asubirie matibabu miezi minne?
Au Dr huyu anapata asilimia fulani akipeleka wagonjwa kutoka Mnazi Mmoja kwenda Al-rahma? Malalamiko ni mengi mtaani kuhusu hospitali hii, hadi nina maswali mengi sipati majibu.
1. Hivi hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar ina Daktari mkuu?
Kama inaye anajua matatizo ya wafanyakazi walio chini yake, kachukua hatua zipi?
2. Je hospitali hii ina Management (Uongozi)? Kama ina uongozi wahudumu wao wenye kauli chafu kwa wagonjwa wanazijua?
3. Je Waziri wa Afya Zanzibar anajua malalamiko ya wagonjwa wanayopitia?
Kama anajua kachukua hatua zipi?
Swali langu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayajua matatizo ya baadhi ya wahudumu wa hii hospitali?
4.Je kwenye hii hospitali hamna mashushushu wa kuwasilisha taarifa sehemu husika?
5. Je wengi wao madaktari wa Mnazi Mmoja sifa za kuwa kwenye kuajiriwa wamekidhi au wameingizwa wakiwa CV hazitoshelezi?
Hawa wafanyakazi kuwa na kauli mbaya na uzembe wa aina mbali mbali kwani wanafanya kazi bure, kwani wanafanya kazi ya kujitolea, hawalipwi mishahara ambayo ni kodi ambazo tunakatwa sisi wananchi?
Nitoe ombi kwa Rais mpya Serikali mpya ijayo Hospitali ya rufaa Mnazi Mmoja waitupie darubini na wafanye mabadiliko mbalimbali na ufuatiliaji kwenye hospitali hii ikiwezekana na safari za kuwashtukiza kwenye hospitali hii, mbona kipindi Juma Haji Duni akiwa waziri wa afya walinyooka?
Hospitali ina majengo mazuri, vifaa vizuri na vya kisasa lakini inaangushwa na wafanyakazi wazembe wachache.