Ben R. Mtobwa..
Je hiki ndicho..
Rukia betrachtet sich im Spiegel.
(Rukia) Alimtazama kwa makini msichana huyo aliyesimama mbele yake katika kioo, akimkabili. Kikiwa kioo chenye zaidi ya urefu wake, aliweza kumtazama tangu miguuni hadi utosini. Akaviusudu vidole vyake vyembamba, akautamani mguu huu laini ambao kwa juu ulibebwa na paja nene jekundu, akaridhika na wingi wa nyama iliyojaa kiungwana nyuma ya mapaja hayo. Kiuno chembamba kilichokatika kama anavyotaka kila mwanamume kikamfanya atabasamu, matiti yaliyoshiba ambayo yalikita kifuani kama yanayoukebehi umri kwa kutokuwepo kwa dalili yo yote ya kuusujudia yakamfanya ajipongeze, sura nzuri yenye dalili zote za msichana asiye na hatia ikamfanya achekelee na nywele ndefu laini zilizozingira sura hiyo kama bustani nyeusi zikamfanya ajikute akitabasamu. Tabasamu jepesi, tamu, kitu kingine ambacho ni tunu kwani kingeweza kumroga (loga) mwanamume ye yote. (Uk. 1).
Sie befindet sich allein im Prachtzimmer eines Luxushotels in Dar-es-Salaam. Ein Mann, den sie auf der Straße kennengelernt hatte, hat sie hierher gebracht, die Nacht mit ihr verbracht, mit Geld versorgt und allein zurückgelassen. Drei Tage sind seither vergangen. Sie ärgert sich.
Ni hilo ambalo lilimfanya Rukia akiacha kitanda laini, na kutupa shuka (Frauenkleid) zote hata akasimama mbele ya kioo hiki, kama alivyozaliwa akijitazama kwa hasira. Pengine ameanza kuzeeka? Uzuri wake unatoweka? Mara hii!, ... Alijiuliza wakati akijitazama. Hasira ambazo zilitoweka baada ya kujitazama sana na kuona tena kuwa yeye bado ni tunu yenye thamani sana machoni mwa wanaume. Pengine bwana huyo ni „jeuri“ au „ana kasoro.“
„Awe jeuri ... awe na kasoro ... hapa ametua,“ Rukia alinong’ona. “Nitamwonyesha kuwa Rukia si mtu wa kurukia ovyo. Jasho linamtoka. Asipojihadhari hata chupi ataiuza … Awe waziri, awe balozi …” alisisitiza tena akimtazama msichana huyo ambaye alikuwa akiafikana naye katika kioo. “Ndiyo … usiku …,” alifoka kwa mnong’ono.